Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Mimi tangu siku ile alopowaambia wafanyabiashara eti yeyote aliyenisaidia kwenye uchaguzi anyooshe mkono nikajua tu kuwa jamaa kweli kama mdau mmoja alivyosema hapo juu "NGUVU TEMBO, AKILI SUNGURA"
 
wengi wanaokosoa wameguswa kimaslahi, Imagine wafanyakaz wengi walioharibiwa dili zao za kupiga hela, wengi ni wasomi haswaaa, wanajua kucheza na kalamu na wanajua kuongea haswa, wana wafuasi waliokula nao bata, zaidi ya yote wanasikilizwa balaa.
Uje wafanyabiashara nap wameguswa haswaa, biashara yao imeyumba sababu walizoea mkato, hawajazoea kufuata taratibu, wamejaribu mbinu nyingi lakini mkono wa serikali umeonekaumeonekana kuwafikia.
Tunalalamika Mizigo imeshuka bandalini but nani amefuatilia jinsi mizigo ilivyoshuka Kenya Mombasa? Na hali itakuwa mbaya coz juzi waziri wa biashara Rwanda kafunga mjadala na kuwa mizigo yao itapita zaid Far ports
wananchi wengi tulikuwa tunalia lia Matajir wakikwepa kodi, sisi wenyewe hatujazoeshwa lipa kodi, hatutaki kulipa kodi sababu hatuoni hela zetu zinavyoenda tumika kutusaidia.
Tutajifunza na kuelewa halitakuwa tatizo tena na wale wenzetu watakao pita njia za mkato tutawaona ni wabaya na wahujumu uchumi.
ni swala la muda tu kila kitu kitarudi kwenye mstali, Trust Magufuli

Magufuli hakosolewi kwa nia na adhma ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu, bali kwa mikakati na mienendo iliyo na mwelekeo wa ubaguzi na kufifisha badala ya kuimarisha nguvu za mfumo wa dola. Ukiona mtu anapinga wezi kuchukuliwa hatua basi huyo ana tatizo kubwa.

Lakini mapambano haya hayatafika mbali endapo yataendelea kutegemea maamuzi ya mtu mmoja tu. Alianza vyema kwa kutikisa mfumo. Sasa aongeze na utashi wa kuimarisha mfumo imara usiojali mtu au chama. Kwa mfano, alichofanya kwenye uchaguzi wa meya DSM unaweza kukiita "real statesmanship". Ingawa inasikitisha kwamba CCM haijali kukiuka sheria na taratibu hadi "rais aseme". Hicho ndicho hatukitaki.
 
mkuu,nimekurushia pesa kwa m-pesa,uninunulie na mie,chenji itakayo baki ninulie mafuta ya kupikia,maana nayo yako mbioni kupanda bei...
Mkuu umesahau pia bei ya simu za mkononi inatarajiwa kupanda ifikapo 31 mwezi juni maana zile wanazoita feki zitazimwa. Bei ilishuka sana mpaka 15000 unapata simu sasa wakizima inamaana kariakoo watabakia na zile original hata kama nazo ni feki fresh ila watapandisha bei, sijui kama nalo hilo wanaliangalia au bado tupo kwenye kukamata sukari?????
 
Hapo unapotoka. Hicho ulichoandika ni nje ya UTAWALA WA SHERIA.Kwa hilo mimi nampongeza Mh kwa kuvumilia na kuchukua muda kujiridhisha. Tuache kulaumu kila mahali!
Vipi alivyomfukuza Kabwe hadharani?
 
Kuna sababu kama 4 hivi naziona ndizo zinazomfanya achuje haraka hivi:

1. Kushindwa kwake kudili na majipu (wala rushwa wakubwa) na kubaki kuangaika na kesi za kuku. Hii imejionyesha kwa yeye kunywea kwenye swala la Lugumi, Wezi wa Escrow (kutekeleza maamuzi ya Bunge), kuendelea kukumbatia viongozi majizi, HSC na mambo kama hayo.

2. Kuendesha nchi pasipo kufuata utawala wa sheria. Anajiona yeye ndio ultimate decision maker wa kila kitu na hakuna anayejua zaidi yake. Sasa watu wameamua kumuacha afanye kazi zoootee peke yake.



3. Nchi kukosa muelekeo wa kiuchumi. Hii inapelekea kuwa na hali ngumu pasipo sababu. Bado anaangaika na kodi za machinga na mama Ntilie, wakati kule kwenye madini wanawaanchia wazungu wanachukua madhahabu na Almasi bureee kabisa. Hana vyanzo vipya vya kodi zaidi ya kumbana mwananchi wa kawaidi.

4. Kunyima Uhuru wa habari. Hii imejionyeshwa kupitia kukataa kuonyesha Bunge Live kwa sababu ya kuogopa wananchi kuona serikali yake ikikosolewa. Yeye anataka kusifiwa tu, ukimkosoa ni shida.
Point! Unamwaga point baada ya point!
 
Nimekupata mkuu.

Ule ni udhaifu wa kukusa Leadership Skills. Kama Leader hakutakiwa kabisa ku act namna hile.

Kwenye Leading and influencing hatushauriwa tuwe tunawa reprimand subordinate wetu mbele ya halaiki ya watu - hilo ni moja, pili waziri Mahiga hakuwa na kosa lolote alilolifanya yeye kama yeye, yale yalikuwa ni mambo ya mkewe kugombana na traffic, sasa kwa nini umfokee waziri wako mbele ya umma? Je ulishindwa kumsema mkiwa wawili?
Kweli, ile approach sikuipenda. Rais anasimama hadharani kusema nimemuonya waziri........mkewe....! Haya mambo ya barabarani ni yakawaida na wakati mwingine hawa traffic wanakera sana unakuta kosa la kawaida anakuharasi sana hadi mimi saa nyingine huwa najiuliza au hawa polisi wanaonea wivu wenye magari? Rais ni amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama anakaa na waandishi wa habari kuzungumza habari za koplo? Dah!
 
Mkuu umesahau pia bei ya simu za mkononi inatarajiwa kupanda ifikapo 31 mwezi juni maana zile wanazoita feki zitazimwa. Bei ilishuka sana mpaka 15000 unapata simu sasa wakizima inamaana kariakoo watabakia na zile original hata kama nazo ni feki fresh ila watapandisha bei, sijui kama nalo hilo wanaliangalia au bado tupo kwenye kukamata sukari?????
mamawe!dah,kibano kila angle!
 
Nadhani aliambiwa kuwa haikua sawa, ndiyo maana issue ya Airport hakufanya kama alivyofanya pale Darajani. Haikua sahihi kabisa!
Sasa si atanywea. Kwasababu jamaa alizoea kuzoa sifa kwa kufukuzafukuza hadharani.
 
Hata Lowasa mliambiwa muachane nae hana nguvu yoyote ya kuipasua ccm , mkakomaa ataipasua ccm.

Nilifikili mmejifunza kuwa siasa za kwenye mitandao hazina nafasi , kumbe bado. Nyumbu bwana ,subilini kuumia tena 2020.
 
Ni mazuri hayo ila gharama sasa.
Ila mlizoea sana kuishi kama malaika sasa mtaishi kama mashetani
Mimi naona kauli hii ya JPM imekaa kinyume. Nadhani majizi, mafisadi, wahujumu uchumi ndo Mashetani. Malaika ni wapole na hawaibi na si mafisadi. Sasa taifa la mashetani ni zuri kweli? Naona taifa la malaika ndo linafaa kuishi.
 
Back
Top Bottom