- Thread starter
- #41
Mbowe na Lowassa wanaongoza nchi gani?Lowassa vipi anaandikwa?? Mboowe je
Mbowe na Lowassa wanaongoza nchi gani?Lowassa vipi anaandikwa?? Mboowe je
Kwa kweli hali ni mbaya sana kwa wananchi wa kawaida.....BAHATI mbaya bajeti asilimia 46 yote anaenda kuwalipa wachina ambao ni wakandarasi....wachina nao watazichukua na kupeleka kwao ukiacha vimanunuzi vidogo vidogo,mtaani pesa itaendela kuadimikaHuwezi kuendesha nchi kwa ufanisi ukitengeneza sifa binafsi. Tatizo la kupenda sifa sana ndilo linaiangusha serikali hii, kukosolewa ndio nafasi nzuri ya kuendesha mambo smoothly. Awamu ya nne pamoja na ubovu wake wote lakini ile hali ya kukubali kusemwa hadharani ilikuwa inawapa watu nafasi ya upunguza machungu yao.
Magu kaona Nape anafunga magazeti, anazuia matangazo ya Bunge na anakataa kusemwa akadhani itamsaidia lakini inammaliza kabisa, miezi sita hali iko hivi jee miaka miwili?
Mbegu imefukiwa chini ya zegeNi lazima mbegu ifukiwe kwanza ili kuweza kuchipua tena, safari bado inaendelea ngoja tusubiri muda sahihi wa kutoa hukumu
Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.
Ghafla upepo ukabadilika, watumishi wakaanza kukosoa utumbuaji majipu, wafanyabiashara wakakosoa mbinyo wake kwenye kodi, wanasiasa wakahoji style yake ya uongozi. Wananchi wa kawaida wakanigwa na maisha magumu (ingawa hawa bado wamebakiza kaimani fulani). Vyombo vya habari wanalalamikia kuminywa uhuru wao.
Kiujumla upepo unavuma vibaya kwa JPM naye ameshakiri ugumu wa kiti chake mpaka akasema angejua asingegombea urais. Je, rais wetu amekosea wapi mpaka hali imegeuka mapema hivyo?
Nguvu tembo akili sungura!!!
hivi ndivyo majibu ya wanajaami forum wote wanaopaswa kuchangia uzi huu,,,ile unapinga au kusapoti,,,toa hojaa,,,,asante mkuu na wengine,,matusi peleka tandaale na uvinza mkachezeshane churaKuna sababu kama 4 hivi naziona ndizo zinazomfanya achuje haraka hivi:
1. Kushindwa kwake kudili na majipu (wala rushwa wakubwa) na kubaki kuangaika na kesi za kuku. Hii imejionyesha kwa yeye kunywea kwenye swala la Lugumi, Wezi wa Escrow (kutekeleza maamuzi ya Bunge), kuendelea kukumbatia viongozi majizi, HSC na mambo kama hayo.
2. Kuendesha nchi pasipo kufuata utawala wa sheria. Anajiona yeye ndio ultimate decision maker wa kila kitu na hakuna anayejua zaidi yake. Sasa watu wameamua kumuacha afanye kazi zoootee peke yake.
3. Nchi kukosa muelekeo wa kiuchumi. Hii inapelekea kuwa na hali ngumu pasipo sababu. Bado anaangaika na kodi za machinga na mama Ntilie, wakati kule kwenye madini wanawaanchia wazungu wanachukua madhahabu na Almasi bureee kabisa. Hana vyanzo vipya vya kodi zaidi ya kumbana mwananchi wa kawaidi.
4. Kunyima Uhuru wa habari. Hii imejionyeshwa kupitia kukataa kuonyesha Bunge Live kwa sababu ya kuogopa wananchi kuona serikali yake ikikosolewa. Yeye anataka kusifiwa tu, ukimkosoa ni shida.
M mwanzon nliamin kua amejitoa mhanga na kuamua kuweka Chama pemben IL kuwakomboa wananchi ila mhhh naanza kupata mashaka ni kma vile Chama kimeanza kumbinya hiv hata waziri mkuu na vice n kama vile wamerud nyuma katika mapambano na kubaki neutral.
Kuna sababu kama 4 hivi naziona ndizo zinazomfanya achuje haraka hivi:
1. Kushindwa kwake kudili na majipu (wala rushwa wakubwa) na kubaki kuangaika na kesi za kuku. Hii imejionyesha kwa yeye kunywea kwenye swala la Lugumi, Wezi wa Escrow (kutekeleza maamuzi ya Bunge), kuendelea kukumbatia viongozi majizi, HSC na mambo kama hayo.
2. Kuendesha nchi pasipo kufuata utawala wa sheria. Anajiona yeye ndio ultimate decision maker wa kila kitu na hakuna anayejua zaidi yake. Sasa watu wameamua kumuacha afanye kazi zoootee peke yake.
3. Nchi kukosa muelekeo wa kiuchumi. Hii inapelekea kuwa na hali ngumu pasipo sababu. Bado anaangaika na kodi za machinga na mama Ntilie, wakati kule kwenye madini wanawaanchia wazungu wanachukua madhahabu na Almasi bureee kabisa. Hana vyanzo vipya vya kodi zaidi ya kumbana mwananchi wa kawaidi.
4. Kunyima Uhuru wa habari. Hii imejionyeshwa kupitia kukataa kuonyesha Bunge Live kwa sababu ya kuogopa wananchi kuona serikali yake ikikosolewa. Yeye anataka kusifiwa tu, ukimkosoa ni shida.
hahahahaa ngoja tusubiri mkuu coz hata dhahabu hupitishwa kwenye moto kwanzaMbegu imefukiwa chini ya zege
TB Joshua alikuja Tanzania akatembea peku....kibiblia hii ni mbaya sana.....ni sawa na wale manabii waliovaa magunia kulaani wafalme ambao baadae falme zao zilipigwa mapigo makali
ahahaha,kwa hio akili imeshindwa kuendesha mwili?
Tanzania zaidi ya unavyoijua.
Niliandika mapema sana hapa wakati serikali hii ikiwa na miezi miwili tu kuwa utawala wa nchi za kiafrika umejengwa katika kumuangalia Rais anataka nini?
Hilo ni kosa namba moja, mawaziri wakaanza kufanya kazi kwa namna ambavyo rais anataka.
Hivi uzembe umeisha kwenye taasisi na idara za umma?
Kilichotokea uwanja wa ndege ni ushahidi/ishara tosha kuwa serikali haiwezi kututoa hapa tulipo kwa ziara za kushutukiza.
Kuna shida gani tukiwa na aina ya serikali na utawala ambao kila kiongozi anakuwa na majukumu ambayo yapo wazi?
Unaweza kuona issue ya machinjio tu pale Vingunguti wanakwenda mawaziri watatu.
Narudia kusema Mheshimiwa Rais Kama Ana nia ya dhati ya kuboresha hali ya maisha ya mtanzania lazima awe na serikali ambayo kila kiongozi/cheo linakuwa "defined" kwa majukumu yake.
Utashangaa mkanganyiko uliopo,
1. Mkuu wa mkoa anakuwa na kazi ya kukagua shule, afisa elimu anafanya nini?
2. Mkuu wa mkoa anajivika jukumu la kutafuta wafanyakazi hewa? Wakurugenzi na maafisa rasilimali watu, maafisa tawala wanafanya nini?
Ikifika siku tukawa na serikali ambayo kila mtu ana majukumu yake yanayoeleweka na akayatekeleza ipasavyo basi tutafika mbali.
Tusimwachie mzigo huu Rais peke yake hawezi kufanya ziara za kushtukiza kila mahali hata kama atatawala miaka 100.
Tuwajibike.
Duh! Kweli wewe ni Great Thinker!Mlilipwa kumshambulia JPM kipindi cha kampeni mkashindwa,mlivyo na akili fupi mnadhani mtafanikiwa na mtu ameshakuwa Raisi??,kweli akili zenu fupi sana,ndo maana Mzee Mkapa aliwaita WAPUMBAVU NA MALOFA.,ndo maana Mlikuwa mkizungusha mikono kama wendawazimu,nimeanza kuelewa.