Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.

Ghafla upepo ukabadilika, watumishi wakaanza kukosoa utumbuaji majipu, wafanyabiashara wakakosoa mbinyo wake kwenye kodi, wanasiasa wakahoji style yake ya uongozi. Wananchi wa kawaida wakanigwa na maisha magumu (ingawa hawa bado wamebakiza kaimani fulani). Vyombo vya habari wanalalamikia kuminywa uhuru wao.

Kiujumla upepo unavuma vibaya kwa JPM naye ameshakiri ugumu wa kiti chake mpaka akasema angejua asingegombea urais. Je, rais wetu amekosea wapi mpaka hali imegeuka mapema hivyo?
Pale alipotangaza kuvifuta vyama vya upinzani na kumwachate bashite kwenye kiti wakati watumishi wakitumbuliwa wengne kwa kuonewa,alipozima bunge laivu,alopolazimisha tulia kuwa naibu spika,anapotumia pesa ya umma bila kufuata sheria,alipoamua kukunua korosho alafu mpaka sasa wakulima wanasota nk kiukweli namkubali magufuli ni mzalendo wa kweli kabisa hasa kwa mazuri mengi anayofanya ila sasa baadhi ya maamuzi na hatua anazochukua kusolve changamoto nyingi zinamkosti na kutuumiza watanzania kama ningepata nafasi ya kusema chochote mbele yake ningemwambie apige kazi!!!!
 
Me naona, tatizo lilianzia pale mtu anapokuwa anadanganya, au tuite kutumia propaganda nyepesi.

Kwa mf, mimi nilikuwa mfuasi namba moja wa jamaa mara baada ya kuingia madarakani.

Kiukweli aliteka sana hisia zangu, hasa kweny ziara ya kanda ya ziwa. Hotuba zake zilijaa maneno matamu matamu kuhusu maendeleo ya Tanzania. Hakika nilikuwa napenda sana kumsikiliza kila alipohutubia.

Nilikuja kuacha kumfuatilia, pale alipoanza kusema; "Tunajenga kwa fedha zetu za ndani, hatukopi" Siku nyingine akisema; "Tunakopa lakini kwa masharti nafuu". Nikawa najiuliza, nishike lipi!

Nikajiepusha naye, simfatilii kabisaaaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hofu yangu kuu ni hii hii sheria mpya ya vyama vya siasa naona kabisa wanasiasa wachache watakaojitokeza kusimamia na kutetea wanyonge
Mku hii sheria ni nzuri kwa wanaoitaka Sudani kwani watajiondoa kwenye vyama kimwili lakini moyoni wako kwenye vyama vyao na hawa watakuja kama Wanaharati wa kisiasa ndo panaanza kukucha kwa ujumla Msajili ilitakiwa angalie hii sheria ndo maana upinzani wa kweli uko kimya na hii kukaaa kimya imawaumiza sasa wadanganyaji hawajui baada ya bunge kuvunja na kuingia ktk uchaguzi wataibuka Wanaharakati wangapi na issue ya CAG na IMF halijapata mfikisha ujumbe wa elimu ya Raia.

Chama changu ccm hii sheria ni alama ya mabadiliko yaliyo yalazima tunayatafuta wenyewe chama kikae chini kiangalie namna hali ya Sudan ilivyotokea ile yote tukumbuke mbinyo waliokuwa nao hao raia wa hizo nchi zilizokutana na mabadiliko kama ya Sudan
 
"Niliahidi kuwa, kabla sijaondoka madarakani nitaongeza mishahara ya wafanyakazi. Lakini muelewe ndugu zangu kuwa, bado sijaondoka madarakani."- Rais Dkt Magufuli https://t.co/y5l95xAqvW

Mzee baba noma
 
Uwezo wa kuongoza kiti alichopewa hana uwezo huo , sasa ndio yanajidhihirisha kadri muda unavyoenda .Hata ccm wameshajua kosa lao ,ndio maana wote wako kimya ,Hanna anayeongea hata mmoja hii inathibisha kuwa wamemzilia nchi .
 
Uwezo wa kuongoza kiti alichopewa hana uwezo huo , sasa ndio yanajidhihirisha kadri muda unavyoenda .Hata ccm wameshajua kosa lao ,ndio maana wote wako kimya ,Hanna anayeongea hata mmoja hii inathibisha kuwa wamemzilia nchi .
 
CCM wenyewe wanajuta; ila hawana namna.
 
Jibu hoja utakuwa umemsaidia yeye na taifa, mashambulizi kwa mtu aliyeonyesha kile kinachoonekana hayasaidii
Hata Barack Obama alivyo ingia madarakani 2008 sivyo alivyotoka 2016 ! Lakini aliitoa shimoni Marekani. It is quite normal! Kikwete je ?
 
Back
Top Bottom