Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,186
- 37,501
Kuna sababu kama 4 hivi naziona ndizo zinazomfanya achuje haraka hivi:
1. Kushindwa kwake kudili na majipu (wala rushwa wakubwa) na kubaki kuangaika na kesi za kuku. Hii imejionyesha kwa yeye kunywea kwenye swala la Lugumi, Wezi wa Escrow (kutekeleza maamuzi ya Bunge), kuendelea kukumbatia viongozi majizi, HSC na mambo kama hayo.
2. Kuendesha nchi pasipo kufuata utawala wa sheria. Anajiona yeye ndio ultimate decision maker wa kila kitu na hakuna anayejua zaidi yake. Sasa watu wameamua kumuacha afanye kazi zoootee peke yake.
3. Nchi kukosa muelekeo wa kiuchumi. Hii inapelekea kuwa na hali ngumu pasipo sababu. Bado anaangaika na kodi za machinga na mama Ntilie, wakati kule kwenye madini wanawaanchia wazungu wanachukua madhahabu na Almasi bureee kabisa. Hana vyanzo vipya vya kodi zaidi ya kumbana mwananchi wa kawaidi.
4. Kunyima Uhuru wa habari. Hii imejionyeshwa kupitia kukataa kuonyesha Bunge Live kwa sababu ya kuogopa wananchi kuona serikali yake ikikosolewa. Yeye anataka kusifiwa tu, ukimkosoa ni shida.
Mkuu Nkuba25 hakika wewe umeirejesha JF ya wakati uleee mdau kauliza swali zuri,nilitegemea wachangaji wangekuja na hoja nzito badala yake wengi wamekuja na viroja badala ya hoja.
Kiasi fulani nakubaliana na hoja zako hasa hili la kukosa utawala wa sheria nililiona tangu mwanzo nikajisemea Dr Magufuli yeye Rais hapo hapo anafanyakazi za kibunge,wakati mwingine anakuwa yeye mshitaki na yeye Jaji.
Hili la kuminya uhuru wa habari ndio limeniacha hoi bin taabani.Fikiria bila uhuru wa habari hata yeye asingejulikana hata kidogo.Kibaya zaidi anapenda kutumia vyombo vya habari hata mahali pasipo stahili.Mfano unatimua maafisa wa Serekali mbele ya Media tena pasipo kuwapatia nafasi ya kujitetea ?.Kila anachokifanya lazima atumie media sana tena kwa nguvu kubwa lakini Bunge hataki lionekane live ?hataki tuhukumu utendaji wa wabunge wetu tuliowachagua.
Suala la uhaba wa Sukari ni tatizo alilolitengeneza Dr Magufuli lakini lawama anawarushia wafanyabiashara tena anawatuhumu pasipo ushahidi wa uhakika eti walikuwa wakileta sukari ili expire.TBS walikuwa wako wapi,ipo kesi mahakamani kuhusiana na suala hilo kama hakuna basi hapakuwa na sababu ya kuliongelea hata kidogo hasa ukizingatia level yake kama Rais wa JMT.
Suala la Mke wa Dr Mahiga na trafic police hakuwa sawa kumpandisha askari cheo kisa kabisaha na mke wa waziri.Pili Mke wa waziri ni mtu mzima mwenye kuwajibika kwa matendo yake binafsi kumwingiza waziri tena katika mkutano wa wakuu wa jeshi la polisi haikuwa sawa hata kidogo.
Mwisho naanza kuingiwa na woga iwapo hali hii itaachwa kuendelea bila wadau mbali mbali kupaza sauti ya kuonya na kukemea ukiukwaji wa sheria,kanuni na taratibu za kuongoza nchi.