Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Shinikizo linakuja kwa kasi,nawaza miaka miwili ijayo itakuwaje na ukichukulia jamaa huwa ana hasira na maamuzi ya jazba....wapinzani wanamsubiri akianza jazba wampigie hapohapo
Mkuu jana wamemtisha PM kama hatochukua hatua stahiki dhini ya wale Lugumi &Family watamng'oa.
 
Mimi kuna sehemu nasalia, ilikuwa kabla ya ibada lazima aombewe mh Raisi mwema sana, lakini siku hizi naona wameacha kumuombea sijui kwanini
 
Mimi kuna sehemu nasalia, ilikuwa kabla ya ibada lazima aombewe mh Raisi mwema sana, lakini siku hizi naona wameacha kumuombea sijui kwanini
Ila nchi hii bwana! tunaambiwa tuwaombee na sisi tunaomba kama mazuzu?
 
Ili uthibitishe haya maneno yako kuwa Magufuli kachuja au lah nenda mtaani alafu ukikuta kikundi cha watu tamka haya maneno kuwa "Magufuli hafai".. Kitachokutokea kutoka kwa wananchi usisite kuja kutuambia ata kama ukiwa ICU.
Labda wananchi wa chato na mtaa wa Lumumba, nilipo mimi watu wanamuona ni mkurupukaji tu asiye na vision
 
Alichokosea alituhaidi kukamata majizi na mafisadi badala yake anatumbua majipu kitu ambacho hakutuahidi, hivyo hatumuelewi.
Wakati jipu namba 1 ni mwenyekiti wa chama chake ambaye wanakunywa chai pamoja kila siku
 
Kuna sababu kama 4 hivi naziona ndizo zinazomfanya achuje haraka hivi:

1. Kushindwa kwake kudili na majipu (wala rushwa wakubwa) na kubaki kuangaika na kesi za kuku. Hii imejionyesha kwa yeye kunywea kwenye swala la Lugumi, Wezi wa Escrow (kutekeleza maamuzi ya Bunge), kuendelea kukumbatia viongozi majizi, HSC na mambo kama hayo.

2. Kuendesha nchi pasipo kufuata utawala wa sheria. Anajiona yeye ndio ultimate decision maker wa kila kitu na hakuna anayejua zaidi yake. Sasa watu wameamua kumuacha afanye kazi zoootee peke yake.



3. Nchi kukosa muelekeo wa kiuchumi. Hii inapelekea kuwa na hali ngumu pasipo sababu. Bado anaangaika na kodi za machinga na mama Ntilie, wakati kule kwenye madini wanawaanchia wazungu wanachukua madhahabu na Almasi bureee kabisa. Hana vyanzo vipya vya kodi zaidi ya kumbana mwananchi wa kawaidi.

4. Kunyima Uhuru wa habari. Hii imejionyeshwa kupitia kukataa kuonyesha Bunge Live kwa sababu ya kuogopa wananchi kuona serikali yake ikikosolewa. Yeye anataka kusifiwa tu, ukimkosoa ni shida.

This can be the best answer.

Wananchi wamemuona ni yuleyule tu.
 
Mlilipwa kumshambulia JPM kipindi cha kampeni mkashindwa,mlivyo na akili fupi mnadhani mtafanikiwa na mtu ameshakuwa Raisi??,kweli akili zenu fupi sana,ndo maana Mzee Mkapa aliwaita WAPUMBAVU NA MALOFA.,ndo maana Mlikuwa mkizungusha mikono kama wendawazimu,nimeanza kuelewa.
Hii haina mambo ya uchama ndugu kama kuumia ni watanzania wote na kama kufaidika ni watanzania wote si chamama fulani elewa mada as a great thinker sio kiushabiki mtakapo isoma namba kama mlivoimba ndo kitaeleweka street stay tuned usiandikie mate.Time will tell.
 
Unapochangia hoja jaribu kutumia lugha ya staha hasa inapokuwa mhusika ni mheshimiwa. Ustaarabu na heshima ni kitu cha bure. Usiwatukanishe waliokuzaa na kukulea kuwa hawakutimiza wajibu wao ulipokuwa mtoto hadi ukikua.
Mkuu mbona umepanic huyo mwenye comment katumia lugha ya picha hujui fasihi au?
 
Hii haina mambo ya uchama ndugu kama kuumia ni watanzania wote na kama kufaidika ni watanzania wote si chamama fulani elewa mada as a great thinker sio kiushabiki mtakapo isoma namba kama mlivoimba ndo kitaeleweka street stay tuned usiandikie mate.Time will tell.
Kweli, kama kuumia tunaumia sote
 
Hata EL katokea fisiem ni bora angekua rais kupitia upinzani au fisiem japo fisiem wangempitisha nisingempa kura kama ambavyo sikumpa JP lakini afadhari yule licha ya madudu yake angefaa zaidi kuliko huyu coz anabusara,mvumilivu,hana pupa na ni bingwa wa organizational leadership na ana mahusiano mazuri na watu lakini kwangu kubwa zaidi ni mfanyabiashara aliyefanikiwa so angekua kwenye nafasi nzuri ya kucheza karata za uchumi vyema huku upinzani ukifanya constructive critics tungefika mahala lakini huyu mkomunist mwenye hasira na matajiri simuelewi labda tanzania ya viwanda watajenga walalahoi.Endapo itafika june 2017 uchumi ikiendelea kudorora nitafikia hitimisho kua kama taifa tumepata hasara.Acheni kabisa kushabikia sera za ujamaa hazina maana kabisa hua zinaleta umaskini kuliko kuondoa na ndizo zimetufikisha hapa tulipo leo
 
Back
Top Bottom