Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

ILE MICHORO YA JANAURY MAKAMBA INA MAANA LUGHA YA PICHA ILE INATIMIA TARATIBU KUONESHA UHALISIA WA CCM MWENYE NAYO ATUPIE HAPA.
 
Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.

Ghafla upepo ukabadilika, watumishi wakaanza kukosoa utumbuaji majipu, wafanyabiashara wakakosoa mbinyo wake kwenye kodi, wanasiasa wakahoji style yake ya uongozi. Wananchi wa kawaida wakanigwa na maisha magumu (ingawa hawa bado wamebakiza kaimani fulani). Vyombo vya habari wanalalamikia kuminywa uhuru wao.

Kiujumla upepo unavuma vibaya kwa JPM naye ameshakiri ugumu wa kiti chake mpaka akasema angejua asingegombea urais. Je, rais wetu amekosea wapi mpaka hali imegeuka mapema hivyo?
Hayo ni maoni yako binafsi, ni haki yako kuwa nayo na kwa hiyo hakuna haja ya kuyajadili hapa!
 
Kufanya mambo kwa sifa ni hatari sana.tulianza kwa kusomewa taarifa za mapato na TRA kila mwezi kwenye TV Leo huu mwezi wa pili huu kimyaa .kuendesha nchi hakuhitaji mbwembwe.
Hivi wewe na Salary Slip ni ndugu? Mwenzako alianzisha mada eti TRA haijatoa taarifa ya mapato ya mwezi Aprili. Tulivyoweka hiyo taarifa akatoka nduki
 
image.jpg


Waione Misukule wote akiwemo Salary Slip
 
Nadhani pailikosekana strategy za uongozi. Uongozi una techiques zake ambazo kama hukusomea basi unapswa kufundishwa na magwiji wliobobea. unfortunatelly wahandisi wengi hawakusomea management na hawapendi maana waniita ungwini. U preso ni utaalam wa uongozi, ushirikishaji, vikienda na stategies bila kusahau wadau wakiwemo wafanya biashara.
 
Kwa Hasara hii Kwanini asichuje


Hii hasara ya Sukari kupanda


Mwanzoni ilikuwa 2000 sasa ni wastani wa 3500

Hivyo ni ongezeko la 1500

Watanzania 10 Milioni walikununua sukari Kilo 2 kila mwezi

2*1500*10,000,000

Jumla ni 30,000,000,000,

Sawa na 30 Bilioni


Haya ni makadirio ya Chini kabisa.
 
Kuondoa wananchi kuona Bunge Live na kutoonekana mwelekeo wa kujenga strong institutions.
 
TB Joshua alikuja Tanzania akatembea peku....kibiblia hii ni mbaya sana.....ni sawa na wale manabii waliovaa magunia kulaani wafalme ambao baadae falme zao zilipigwa mapigo makali
Hapa nimekumbuka kitu
 
Haya yanayotokea ni matokeo ya mifumo mibovu iliyowekwa kwa watu wenye fedha zao kuwa na maamuzi ikitokea mabadiliko kama haya anayoyafanya JPM ni lazima waathirika watakuja huku wataka hali iliyozoeleka iendelee.

lkn wananchi walinganishe na namna gari ukipaki mlimani wakati wa kuondoka itaonekana kurudi nyuma na baada ya hapo itaendelea na safari hivyo kwa juhudi hizi za makusudi nataraji kuona maisha bora muda si mrefu ingawa lazima kwa kuanza mikono itaota sugu kiasi
Kwa hiyo tulosema tatizo ni mfumo tuko sahihi?
 
wewe ndiyo ubongo wako umechuja.....mara nyingi wanaolalamika ni wale ambao walizoea njia za mkato...sisi wananchi maisha magumu huwa tunayo kila siku na tunakomaa nayo...lkn wafanyakazi ,wanasiasa na wafanyabiashara acheni awanyooshe......Magufuli mbele kwa mbele.
 
Hii nchi angeiweza Lowasa.Kichwa kimejaa busara na uvumilivu
Hilo zigo lenu halitakaa lipate uraisi maishani mwake,labda raisi wa mioyoni yenu baraza la vichaa,Huyu Huyu tu na Hata muanzishe thread 800 kumpinga,mtachemka tu na nchi itasonga tu,nyie mtabaki na hasira zenu humu JF Lakini zitagonga mwamba tu.
 
Jamaa,kapoa saana.mpka,namuhurumia,,,siku ile ameshtukiza airport nlitegemea mtu atumbuliwe..maana yule maza alimdanganya lkn hakufanya hvo.asa nkajiuliza,mbona Mama Kilango alidanganyq na yy lkn akatumbuliwa
Mimi mwenyewe nilishangaa aliyokuwa anaongea kiupole siku hiyo
 
Nkuba25,
hapa umenena.
--->>
Bado
anaangaika na kodi za
machinga na mama
Ntilie, wakati kule
kwenye madini
wanawaanchia
wazungu wanachukua
madhahabu na Almasi
bureee kabisa. Hana
vyanzo vipya vya kodi
zaidi ya kumbana
mwananchi wa kawaida...
 
Back
Top Bottom