Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Hata mke wake nasikia anataka kurudia kazi yake ya ualimu kwasababu ya visa vya jamaa. Akirudi home eti anataka akute pilau kuku wakati hela ya matumizi haachi.
Unaushahidi na family issues!!?;au unatafuta gate la segerea!?
 
Mimi binafsi nimeshatosheka nae kabisa....mtu gani anafanya kazi za kila mtu utadhani yeye ndiyo mtanzania pekee, wengine kama wakimbizi tu.
Nahisi hii yote ni kwa sababu ya ukurupukaji, hata kugombea nahisi ilikuwa kama kukurupuka tu.
Haya ngoja tumuone "rais wetu mwema
 
Ili uthibitishe haya maneno yako kuwa Magufuli kachuja au lah nenda mtaani alafu ukikuta kikundi cha watu tamka haya maneno kuwa "Magufuli hafai".. Kitachokutokea kutoka kwa wananchi usisite kuja kutuambia ata kama ukiwa ICU.
Thubutuuu!!;sema wanajimwayamwaya humu na kutoa maneno ya shombo!;tangu walipokua wanazungusha mikono ka machizi akili hazijawarudia ndo maana!!
 
Hayo ni mawazo yako, watanzania wapenda hakhi bado tuna imani na JPM. Tunamuombea kwa Mungu adumu adumu adumu. Na ninyi mnaomtabiria mabaya mnyong'onyee kabla adhma zenu hazijatimia.
 
Mlilipwa kumshambulia JPM kipindi cha kampeni mkashindwa,mlivyo na akili fupi mnadhani mtafanikiwa na mtu ameshakuwa Raisi??,kweli akili zenu fupi sana,ndo maana Mzee Mkapa aliwaita WAPUMBAVU NA MALOFA.,ndo maana Mlikuwa mkizungusha mikono kama wendawazimu,nimeanza kuelewa.

Kwa akili hii wacha tuendelee kuisoma namba, hakuna namna!
 
Alichokosea alituhaidi kukamata majizi na mafisadi badala yake anatumbua majipu kitu ambacho hakutuahidi, hivyo hatumuelewi.
Subir utaelewa tu!!;na ukielewa pia useme sasa umeelewa!
 
Kuna sababu kama 4 hivi naziona ndizo zinazomfanya achuje haraka hivi:

1. Kushindwa kwake kudili na majipu (wala rushwa wakubwa) na kubaki kuangaika na kesi za kuku. Hii imejionyesha kwa yeye kunywea kwenye swala la Lugumi, Wezi wa Escrow (kutekeleza maamuzi ya Bunge), kuendelea kukumbatia viongozi majizi, HSC na mambo kama hayo.

2. Kuendesha nchi pasipo kufuata utawala wa sheria. Anajiona yeye ndio ultimate decision maker wa kila kitu na hakuna anayejua zaidi yake. Sasa watu wameamua kumuacha afanye kazi zoootee peke yake.



3. Nchi kukosa muelekeo wa kiuchumi. Hii inapelekea kuwa na hali ngumu pasipo sababu. Bado anaangaika na kodi za machinga na mama Ntilie, wakati kule kwenye madini wanawaanchia wazungu wanachukua madhahabu na Almasi bureee kabisa. Hana vyanzo vipya vya kodi zaidi ya kumbana mwananchi wa kawaidi.

4. Kunyima Uhuru wa habari. Hii imejionyeshwa kupitia kukataa kuonyesha Bunge Live kwa sababu ya kuogopa wananchi kuona serikali yake ikikosolewa. Yeye anataka kusifiwa tu, ukimkosoa ni shida.
#4 ni ya wazi zaidi aisee.
 
****
NINGEKUWA MAGUFULI VYOMBO VYA HABARI NINGEVIPA UHURU ZAIDI NA ULINZI MAALUM, MAANA NDIVYO VINAVYOFUNUA UOVU ULIO CHINI KABISA / AU KUJIFICHA.

unless otherwise tunashindwa tambua dhamira yake ya ndani.
Kama akina kubenea eti ehe!!?
 
Mbona mtoa post na wachangiaji hamjielewi? kwa miezi 7 aliyoyafanya ni makubwa sana, lakini ni muda mfupi kubadilisha nchi na watu kufaidi au kupata ahueni ya maisha, halafu budget ndo hiyo kwanza hata haijapita mmeanza kelele, kumbukeni wafanyabiashara pia wanataka kua juu ya serikali kwa kuficha sukari ili wajipangie bei, JPM bado anajipanga kwa mambo mengi , utumbuaji ( kuwasimamisha watu Kazi) lazima iwe kazi endelee mpaka tuheshimiane.
Safi sn!!;Espiga deki highway utawaweza!!?
 
Sasa hapa sijakuelewa, amechuja kwa sababu haonekani kwenye magazeti au amechuja kwa kutotumikia taifa? Wakati mwingine sio kila kitu kiwe kisiasa, kuna mengine tuyatazame kama binadamu. Hivi wewe ulitaka watumishi wa uma waendelee na uzembe? Majizi serikali yaendelee kula na hao wafanyabiashara waendelee kutunyonya? Huyu unae mpondea ndio atakae boresha maisha yako, maisha ambayo mzazi wako alishindwa kukuboreshea.
Hwawezi kukuelewa!!;tangu wlipozungusha mikono akili haijakaa sawa!!
 
1. Mahakama ya kushughulikia Mafisadi wote
2. Tanzania yenye uchumi wa Viwanda
3. Tanzania yenye uchumi wa kati

Tunamwombea JPM afanikiwe tu katika hizi ahadi tatu alizozitoa wakati wa kampeni!
 
Ngosha amechemka bado mapema sana, hili ni kosa la kuwapa watu matumaini makubwa wakati huna uwezo wa kuyatekeleza.

Halafu kiongozi lazima ujinasibu kuwa unaongoza vikundi vyote vya watu. Unapojinasibu na U ccm tayari umewapoteza wapinzani, OK unabaki na hao CCM. Na penyewe unajinasibu na masikini, tayari umewapoteza matajiri. Isitoshe unapambana na matajiri na watumishi ukiwaaminisha wananchi kama hawa ni watu wabaya sana bila kujua hii ni sehemu ya jamii inayotegemewa na hao masikini na yenye ushawishi mkubwa kwa masikini kuliko wewe.
Namalizia na maneno kuntu ya Kasheku Msukuma mbunge wa geita mjini kwa tiketi ya ccm. 'wasukuma wanavuta bangi kabla ya kufanya kazi, na wanafanya kazi kwa nguvu sana baada ya kuvuta'
 
Nadhani Watanzania tu wasahaulifu kweli kweli na ni wepesi kudanganyika hata kwa mambo ambayo hata kwa tafakuri ya kawaida tu tungeweza kung'amua hayana msingi. Kwa miezi yake sita ya kwanza mwaka 2005 baada ya kuapishwa Jakaya Mrisho Kikwete, chaguo la Mungu, hakuna ambaye angethubutu kumsema vibaya mitaani akabaki salama.

Aliitwa tumaini lililokuwa linasubiriwa toka enzi lakini hii leo hata waliokuwa washikaji wake hawathubutu kukubali kuhusishwa naye kwa sababu ya Magufuli, kipya kinyemi. Tunachosahau ni kwamba wote hawa wanatoka kambi ile ile na walipata malezi yale yale...kila baada ya miaka mitano tunapanda mchicha tukiwa na matumaini ya kuvuna ngano.

Yafaa tujiulize, ni kitu gani kinawaunganisha hawa manabii wetu wa uongo? Je wanazaliwa wakiwa hivyo ama malezi na mazingira wanayokulia ndiyo yanafanya mioyo yao kuwa migumu? Jibu ni rahisi sana na liko mbele yetu likituchungulia lakini masikini wadandanyika, mahaba yametunyima uwezo wa kulitambua hata tukikutana nalo uso kwa uso.

Adui mkubwa wa taifa hili ni CCM, period. Tutazungukazunguka, tutaenda kwa waganga na kutambika lakini tukae tukijua tunajidanganya. Akili zile zile zilizotufikisha hapa tulipo haziwezi kutukwamua hadi mbingu zishuke na kudhani tofauti ni uenda wazimu kama walivyosema wahenga...watu kama Magufuli ni kielelezo halisi cha matatizo yetu.
 
Rais Magufuli hajachuja na asikubali kuchuja! Alichofanya ni kuonyesha anachoweza kufanya na style yake ya utendaji. Magazeti na vyombo vingine vya habari vimeshampa umaarufu wa kutosha sana. Sasa Rais Magufuli anayo kazi ya kuwashughulikia kimyakimya wale wanaojaribu kumkwamisha asiweze kuwafanyia wananchi mema aliyodhamiria!
 
Wanopiga mayowe humu ni wezi tu!!;ka c mkwepa kodi basi ni vitumishi vibabaishaji vilivozoea kutengeneza zabuni fake
 
Mlilipwa kumshambulia JPM kipindi cha kampeni mkashindwa,mlivyo na akili fupi mnadhani mtafanikiwa na mtu ameshakuwa Raisi??,kweli akili zenu fupi sana,ndo maana Mzee Mkapa aliwaita WAPUMBAVU NA MALOFA.,ndo maana Mlikuwa mkizungusha mikono kama wendawazimu,nimeanza kuelewa.
Nyie mlikua mnapiga pushapu
 
Wanopiga mayowe humu ni wezi tu!!;ka c mkwepa kodi basi ni vitumishi vibabaishaji vilivozoea kutengeneza zabuni fake
Unapaniki sasa, punguza mapenzi angalia hali halisi, haswaa sukari na uhuru w vyombo vya habari
 
Back
Top Bottom