Maggid mjengwa umepata wapi kibali cha kutafasiri kitabu cha mandela cha long walk to freedom?

Mzee Jasusi; nadhani unajua kuwa translation ya maandiko ni tofauti kabisa na authorship ya maandiko hayo.

Kutumia kitabu cha marejeo ili kuandika cha kwako ni sahihi lakini ni lazima pia uonyeshe kuwa cha kwako ni tofauti ni kile ulichotumia kwenye marejeo, yaani ujumbe wako siyo copy cat ya ujumbe ulio kwenye marejeo. Tena kwa kawaida marejeo yako yanakuwa na vitabu vingine au maandiko mengine siyo marejeo ya kitabu kimoja tu.

Iwapo unaandika kitabu ambacho marejeo yake ni kitabu kimoja tu basi ni lazima uonyeshe kuwa unakichambua kitabu hicho siyo kuwa unatuma ujumbe ule ule ulio kwenye kitabu hicho. Na kama unataka kutoa summary ya kitabu hicho ni lazima uwe makini kwa sababu kwanza unatakiwa kupata kibali cha copyright owner kabla hujatoa summary yako kwa vile inaweza ama kudistort au kudilute content za kitabu original. Halafu summary yako inatakiwa kutoa big picture tu ya kitabu ili kuacha wasomaji wakatafute kitabu original kupata details. Ukiandika details zote za muhimu inakuwa siyo summary tena, na hapo utakuwa na tatizo ama la plagiarism au la copyright infringement!

Niliwahi pia kuona kitabu cha Maisha ya Baraka Obama nikashindwa kukitofautisha na kile alichaondika Obama mwenyewe.
 
Sijui mwenzangu unaongelea uandishi gani? Umesema vizuri kabisa kuwa alichofanya Prof. Mbele ni 'kuchambua' kwa maana hiyo alifanya 'critical review' ya maandishi ya Chinua. Alichofanya Mjengwa si analysis/review bali kutafsiri. Soma kitabu chenyewe na Makala za mjengwa ktk magazeti utaona. Mimi naomba usome sheria ya copyright popote ulipo uone inavyosema kisha soma plagiarism inavyosema then upimwe mwenyewe ukweli uko wapi?
Makologoto,
Sijakisoma kitabu. Lakini kama ni mkusanyo wa insha zake alizokuwa anachapisha kila siku kwenye blog yake hajatafsiri neno kwa neno kitabu cha Nelson Mandela. Alichofanya Maggid ni kuwaeleza wale ambao hawajasoma kitabu ha Mandela kilichomo katika kitabu hicho kama simulizi, akinukuu kauli za Mandela. Hakuna plagiarism hapa kwa sababu plagiarism ni kuchukua maandiko ya mtu mwingine bila kutoa acknowledgement. Ukisoma masimuizi ya Maggid bni dhahiri kuwa yametoka kwenye kitabu cha Mandela.
 
Hao ndio Waandishi Kanjanja wa Bongoland hata hawanaga aibu kabisa,yaani wana njaa sana na kutaka umaarufu kuliko uwezo wao,huyu simtofautishi na yule Mwizi Mkuu wa kazi za Watu,Erick Shigongo.
 
Mzee Mandela ni World Public Figure hakuna cha hati miliki kuandikwa kwake.

Ondoeni upuuzi wenu, mkitaka kinunueni kitabu cha Maggid mkisome mkitaka msikinunuwe.

Maggid Mjengwa, usiwajibu lolote hawa, hawana kazi za kufanya na waonapo wenzao wamethubutu wao huleta roho korosho, hawa si hasha ukakuta ndio wanga wenyewe.
 
Mzee Mandela ni World Public Figure hakuna cha hati miliki kuandikwa kwake.

Ondoeni upuuzi wenu, mkitaka kinunueni kitabu cha Maggid mkisome mkitaka msikinunuwe.

Maggid Mjengwa, usiwajibu lolote hawa, hawana kazi za kufanya na waonapo wenzao wamethubutu wao huleta roho korosho, hawa si hasha ukakuta ndio wanga wenyewe.

......ninahisi na wewe huna tofauti sana na Maggid Mjengwa kifikra........keep it up!
 
Makologoto,
Sijakisoma kitabu. Lakini kama ni mkusanyo wa insha zake alizokuwa anachapisha kila siku kwenye blog yake hajatafsiri neno kwa neno kitabu cha Nelson Mandela. Alichofanya Maggid ni kuwaeleza wale ambao hawajasoma kitabu ha Mandela kilichomo katika kitabu hicho kama simulizi, akinukuu kauli za Mandela. Hakuna plagiarism hapa kwa sababu plagiarism ni kuchukua maandiko ya mtu mwingine bila kutoa acknowledgement. Ukisoma masimuizi ya Maggid bni dhahiri kuwa yametoka kwenye kitabu cha Mandela.

.....Mkuu Jasusi.....ninakusihi ukisome kwanza kitabu cha Hayati Nelson Mandela..."Long Walk to Freedom"..halafu uje uangalie simulizi za huyu Maggid Mjengwa.......ndio utaelewa watu wanachoandika hapa........sidhani kama ni vema kwako ku-draw conclusion wakati hujakisoma kitabu halisi............
 
kwenye facebook post yake nilimuuliza hili swali kuhusu issue ya hakimiliki lakini alilikwepa hakulijibu ila pamoja sina ujuzi mkubwa kuhusu copyright straight away niliona kuna issue apa!!!
 
Ametusaidia sana sisi tusiojuwa kiingereza la mhimu aandike tu kuwa kitabu hiki kimetafsiriwa kutoka ... basi, mengine yote ni umbeya tu. Keep it up Maggid!
 
Kwa maana hiyo unataka kusema ukiona uharifu unatokea unaacha tu kwa vile wewe siyo polisi? Basi huo utakuwa ni uwendawazimu!!!

Huyu Chris Lukosi ndio maana upolisi ulimshinda...hajitambui...nahisi alikuwa anajisahau na kuwasaidia vibaka kukwapua as long as vibaka wanatafuta chakula cha siku....
 
Majid alichofanya ni sawa na hakuna ubaya. Hebu acheni vitu ambavyo havina maana.

Mkuu umepotea sana aisee......Heri ya siku kuu na ninakutakia mwaka mpya 2014 mwema.......

.....Ubaya wa kuhusu kazi aliyoifanya Maggid inaweza kuwa na tafsiri mbali mbali......yeye Maggid katika blog yake anasema hivi........

.....Ni moja ya malengo yangu ya kuandika kitabu cha ' Simulizi Za Mzee Madiba'. Kwamba watu watafute vitabu zaidi vya kusoma....

.....wengine wanamshukuru kwa kuwa amewatafsiria kiingereza na hivyo maisha yaokuwa rahisi......kutafsiri kazi ya mt uhakuna ubaya ila kuna taratibu zake.......swali hapa ameulizwa, je alipewa kibali cha kutafsiri kazi ya Hayati Mandela?

....unless hapa tunaongea na watu wasioelewa maana ya uandishi wa vitabu.......yaani wee Mtanganyika uandike kitabu chako kwa kiswahili ukakiweka sokoni/mauzoni....halafu siku ya siku unakutana na tafsiri ya kitabu chako kwa lugha ya "Kishona" kule Zimbabwe halafu kinauzwa mtaani......
 
Back
Top Bottom