Maggid mjengwa umepata wapi kibali cha kutafasiri kitabu cha mandela cha long walk to freedom?

makologoto

Member
Sep 21, 2013
38
0
Ndugu yangu Maggid Mjengwa nimeona tangazo lako la uzinduzi wa kitabu unachodai umekiandika au umekitafsiri na kukiita jina la "SIMULIZI ZA MZEE MADIBA". Simulizi hizi kwa asilimia zote umezitohoa au umezidurufu kutoka kitabu cha Mzee Mandela kiitwacho "LONG WALK TO FREEDOM" cha mwaka 1995 kilichochapwa na Kampuni ya Abacus. Lakini katika tangazo lako hujasema kama umepata kibali cha kutafsiri kazi ya marehemu Nelson Mandela kabla hajafa, kutoka kwake mwenyewe, au kutoka kwa wanafamilia ama wachapishaji, au mwenye kushikiria haki miliki (kampuni au mtu binafsi).

Assurance ya haki miliki ni swala muhimu sana kwa sasa ili kulinda kazi za wabunifu, ili kazi zao zisidurufiwe (copied) au kutafsiriwa hovyo hovyo kwa ajili ya kuwanufaisha watu wengine nje ya mbunifu/wabunifu au mwenye haki miliki. Sasa najiuliza hivi mauzo ya kitabu ulichokichapisha cha "Simulizi za mzee Madiba" utawafikishia wanafamilia wa mzee Mandela au unakusudia kufanyia nini mapato yatakayotokana na kazi ya marehemu Nelson Mandela ambayo sasa wewe umetumia uwezo wako wa kuihamisha kwa namna kutoka kiingereza hadi kwenye kiswahili? Nitapenda nipate uwazi wa dukuduku zangu hapo juu ili hata kama nahudhuria uzinduzi wako nakuja kwa moyo mweupe, ili nisije kuendeleza plagiarism au copyright violation!!!
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,202
2,000
Swali zuri sana hili, ngoja tusubiri majibu yake.
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,524
2,000
Ngoja nimtetee Maggid. Alichofanya ni kutumia kitabu cha Mandela Long walk to freedom kama hadidu ya simulizi zake.
Hii inaruhusiwa katikia tasnia ya uandishi. Profesa Joseph Mbele amewahi kuandika kitabu kinachochambua maandishi ya Chinua Achebe. Alichofanya Maggid ni kuelezea katika lugha rahisi zaidi simulizi za Mzee Mandela kutoka kitabu chake. Kama ni kutafsiri angefanya hivyo neno kwa neno.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Sijui mwenzangu unaongelea uandishi gani? Umesema vizuri kabisa kuwa alichofanya Prof. Mbele ni 'kuchambua' kwa maana hiyo alifanya 'critical review' ya maandishi ya Chinua. Alichofanya Mjengwa si analysis/review bali kutafsiri. Soma kitabu chenyewe na Makala za mjengwa ktk magazeti utaona. Mimi naomba usome sheria ya copyright popote ulipo uone inavyosema kisha soma plagiarism inavyosema then upimwe mwenyewe ukweli uko wapi?
 
Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,238

Mkuu Jasusi,

Kuchambua na kutafsiri ni vitu viwili tofauti.....tena TOFAUTI ipo KUBWA.........kutafsiri ni KUTAFSIRI tu....iwe kwa lugha nyepesi ya Kiluguru, Kikurya au Kiswahili in this case.......
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,202
2,000
Kuna haja ya huyu jamaa kuja kutoa ufafanuzi wa hii kitu.

Sijui mwenzangu unaongelea uandishi gani? Umesema vizuri kabisa kuwa alichofanya Prof. Mbele ni 'kuchambua' kwa maana hiyo alifanya 'critical review' ya maandishi ya Chinua. Alichofanya Mjengwa si analysis/review bali kutafsiri. Soma kitabu chenyewe na Makala za mjengwa ktk magazeti utaona. Mimi naomba usome sheria ya copyright popote ulipo uone inavyosema kisha soma plagiarism inavyosema then upimwe mwenyewe ukweli uko wapi?
 
IDRISOU

Member
Nov 17, 2012
26
45
Napata raha sana kuona nijinsi gani watu mnaelekezana kwa utaratibu kwa facts zenye msingi. Naona tamaa sana maana mm nipo nasoma certificate in law. Hongeren sana na mungu awapeni mioyo yakutakiana mema katika maisha yenu. Tuendelee na mada.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Ndugu yangu Maggid Mjengwa nimeona tangazo lako la uzinduzi wa kitabu unachodai umekiandika au umekitafsiri na kukiita jina la "SIMULIZI ZA MZEE MADIBA". Simulizi hizi kwa asilimia zote umezitohoa au umezidurufu kutoka kitabu cha Mzee Mandela kiitwacho "LONG WALK TO FREEDOM" cha mwaka 1995 kilichochapwa na Kampuni ya Abacus. Lakini katika tangazo lako hujasema kama umepata kibali cha kutafsiri kazi ya marehemu Nelson Mandela kabla hajafa, kutoka kwake mwenyewe, au kutoka kwa wanafamilia ama wachapishaji, au mwenye kushikiria haki miliki (kampuni au mtu binafsi).

Assurance ya haki miliki ni swala muhimu sana kwa sasa ili kulinda kazi za wabunifu, ili kazi zao zisidurufiwe (copied) au kutafsiriwa hovyo hovyo kwa ajili ya kuwanufaisha watu wengine nje ya mbunifu/wabunifu au mwenye haki miliki. Sasa najiuliza hivi mauzo ya kitabu ulichokichapisha cha "Simulizi za mzee Madiba" utawafikishia wanafamilia wa mzee Mandela au unakusudia kufanyia nini mapato yatakayotokana na kazi ya marehemu Nelson Mandela ambayo sasa wewe umetumia uwezo wako wa kuihamisha kwa namna kutoka kiingereza hadi kwenye kiswahili? Nitapenda nipate uwazi wa dukuduku zangu hapo juu ili hata kama nahudhuria uzinduzi wako nakuja kwa moyo mweupe, ili nisije kuendeleza plagiarism au copyright violation!!!

ARE MODES BIAS? Wana Ubaguzi? Issue ya KITABU cha MANDELA ni POLITICAL NEWS ya kudiscuss Umati Mzima Jamani?

Au ndio tunaamua kuvunja heshima yake kiupendeleo??? is this a one sided entity now...???
 
makologoto

Member
Sep 21, 2013
38
0
ARE MODES BIAS? Wana Ubaguzi? Issue ya KITABU cha MANDELA ni POLITICAL NEWS ya kudiscuss Umati Mzima Jamani?

Au ndio tunaamua kuvunja heshima yake kiupendeleo??? is this a one sided entity now...???
That is the then politician's book i.e. Nelson Mandela lakini km hauna hoja au hauelewi maana ya copyright au plagiarism hulazimishwi kujadili, soma nenda zako. Basi yaishe kwa maana wewe huna mamlaka ya kumsemea kila mtu humu JF, hili ni jukwaa huru.
 
Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,238
2,000
Ngoja nimtetee Maggid. Alichofanya ni kutumia kitabu cha Mandela Long walk to freedom kama hadidu ya simulizi zake.
Hii inaruhusiwa katikia tasnia ya uandishi. Profesa Joseph Mbele amewahi kuandika kitabu kinachochambua maandishi ya Chinua Achebe. Alichofanya Maggid ni kuelezea katika lugha rahisi zaidi simulizi za Mzee Mandela kutoka kitabu chake. Kama ni kutafsiri angefanya hivyo neno kwa neno.

....zaidi ya hapo Mkuu Jasusi......the fact of the matter is.....kama unatafsiri kutoka lugha moja hadi nyingine si lazima utafisiri "neno kwa neno"........ukifanya hivyo inawezekana isilete maana katika lugha unayotaka kutafsiri......
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,443
2,000
Ndio uwezo wake ulipofikia na nina uhakika hata wanaompa nafasi ya kutoa makala gazetini hawazingatii uwezo au uzito wa hoja, anafaa kwenye magazeti ya shigongo
 
Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,238
2,000
Ndio uwezo wake ulipofikia na nina uhakika hata wanaompa nafasi ya kutoa makala gazetini hawazingatii uwezo au uzito wa hoja, anafaa kwenye magazeti ya shigongo

.....kama kuna watu wanaokuwa overrated......basi huyu ni mmoja wapo.......watu kama hawa ni hatari sana kwani hukuta wamepenya kwenye systems zilizo juu ya uwezo wao simply kwa sababu huku kwenye magazeti amekuwa......overrated......kama "mwandishi mchambuzi mwandamizi" wa mambo ya kisiasa na kijamii........
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom