Ingekuwaje kama Mandela asingeandika historia ya maisha yake?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
INGEKUWAJE KAMA MANDELA ASINGEANDIKA TAWASIFU YAKE "LONG WALK TO FREEDOM?

Mimi ni mpenzi mkubwa wa vitabu vya tawasifu na wasifu hasa za watu maarufu awe mwanasiasa kama Nelson Mandeala au mwanamuziki kama Harry Belafonte (My Song) na wengine ambao hwafahamiki sana kama Maulid Mshangama (Sowing The Wind).

Ninajua elimu iliyo ndani ya vitabu kama hivi na faida yake.

Sasa ninaposikia kuwa kuna kiongozi anadai kuwa hana muda wa kuandika tawasifu yake maswali mengi yananijia na nataka kujua kwa nini hataki au hapendi maisha yake yafahamike.

Maisha ya viongozi na watu mashuhuri popote pale duniani ni muhimu kwani ni chuo tosha cha kusomesha watakaokuja baada yake kwa kuijua historia yake na mchango wake katika jamii.

Hapa utawakuta watu kama George Washington, Field Marshall Josip Tito, Kwame Nkrumah, Mahatma Gandhi, Muhammad Ali kwa kuwataja wachache.

Na kawaida watu hawa hawawi peke yao katika yale makubwa waliyoyafanya.

Ukiwasoma utawasoma na wale aliokuwanao.

Hatajiki peke yake wala hathubutu kama ataandika kujitaja peke yake.

Ukiwa unatoka New York unakweda New Jersey kuna daraja linaunganisha miji hii miwili.

Pembeni yake kuna sanamu ya George Washington kapanda farasi wake.

Sanamu ile inamuoyesha George Washington juu ya farasi wake anayatoroka majeshi ya Waingereza yaliyokuwa yamemzingira wakati wa vita vya kupigania uhuru wa Marekani.

Mmarekani ukipitanae hapo atamuadhimisha George Washington na atamuadhimisha na farasi wa George Washington.

Hata farasi anakumbukwa kwa mchango wake.
Katika nchi za Kiafrika wazalendo waliopigania uhuru wanafutwa katika historia bila kupepesa jicho.

Kiongozi anaekataa kuacha historia yake kutoka kwenye kinywa chake na kalamu yake anaacha mswali mengi.

Labda kuna kinachomtia hofu.

Nani sasa atawataja wale wenzake aliokuwanao ikiwa yeye hatoandika?

Hatari ya maswali haya ni kuwa yanakuwa mpata mpatae yaani kila mtu atakuja na jibu lake na pengine majibu haya hayatawapendeza baadhi ya watu katika jamii na wakati mwingine chama chake na serikali yenyewe.

Hapo chini nimeweka badhi ya vitabu vyangu vilivyonisomesha maisha ya watu maarufu vilivyo kwenye maktaba yangu kuanzia Nelson Mandela hadi Maulid Mshangama.

Maarifa niliyopata katika vitabu hivi ni makubwa sana kama nitasema niandike niliyojifunza basi itabidi niandike kitabu.

Ndipo nikasema ingekuwaje kama Mandela asingeandika ''Long Walk to Freedom,'' tungejuaje yale aliyopitia Robben Island yeye kama kiongozi na Afrika Kusini kama nchi?

Mandela anasema kitabu hiki alianza kukiandika akiwa kifungoni lakini kwa bahati mbaya ilipogundulika kuwa alikuwa anaandika kitabu uongozi wa gereza ulimnyang'anya makaratasi yake yote aliyokuwa ameandika.

Kwa upande wake bila shaka huu ulikuwa ni msiba usioelezeka kwa kuwa maana yake ni kuwa kapoteza kazi nzima ambayo hawezi kurudia kuandika upya.

Mwandishi yeyote anafahamu hakuna kitu kigumu kama kurudia kuandika mswada uliopotea.

Kupoteza mswada ni balaa na mkosi mkubwa usio na kifani hasa ikiwa mswada wenyewe ni kutoka kalamu ya mtu kama Nelson Mandela.

Kwa sifa tulizokuwa tunazisikia za Makaburu ni wazi kabisa mswada huu wa Mandela hukumu yake ni kupambana na kibiriti ukachomwa moto na kubakia majivu.

Haikuwa hivyo.

Mandela katika kitabu hiki anasema alipotoka jela Makaburu walimkabidhi mswada wake salama salmin.

Unaweza ukafikiria furaha yake kwa kushika mikononi mwake mswada wa kitabu cha maisha yake alionyang'anywa jela miaka mingi nyuma.

Hii ni sehemu ya kupendeza ya Makaburu ambayo sisi hatukuijua kuwa wana ubinadamu si kuwa walikuwa watu katili na waovu moja kwa moja.

Haya tusingeyajua kama Mandela asingenyanyua kalamu na kuandika.

Dunia ingemshangaa sana Mandela kama angesema baada ya kutoka kifungoni kuwa yeye hana muda wa kuandika.

Mandela katika kitabu hiki kaiachia dunia hazina na urithi mkubwa sana.

''Long Walk to Freedom,'' kina kurasa 768.
IMG_20220318_235101_071.jpg
 
Nimesoma hicho kitabu vol.1 na vol.2 aisee kuna mambo mengi aliyopitia mandela ya kusisimua mno ila kisa kimoja tu ya kwamba kuna askari ambae alikuwa anampelekea chakula kipindi yupo gerezani basi huyo askari ilikuwa lazima atemee makohozi kila chakula ndio anampa mandela ale.Basi mandela anasema baada ya kuapishwa kuwa Rais alimuita yule askari ikulu na walikaa wakala meza moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom