Magazeti yaipa kisogo ndege ya Rais Magufuli

Magazeti yaipa kisogo ndege ya Rais Magufuli

Hapana kuijadili haikua chuki bali tulikuwa tunatoa tahadhari kwa serikali kuwa makini katika manunuzi hayo kwa sababu serikali yetu ina uzoefu wa kununua vitu vibovu sana ambavyo ni hatari kwa usalama wa wananchi.Uzoefu tulioupata katika vivuko chakavu na mabehewa,ulitosha kutumika kama tahadhari na kuikumbusha serikali yetu iwe makini yasije yakatokea yaliyotupata katika manunuzi ya vivuko na mabehewa.

Mjadala pia ulijikita zaidi katika kuionya serikali iwe makini isije ikaingizwa mjini na wajanja kwa kupigwa "cha juu" kama ilivyopigwa kwenye RADA.Mjadala ulikuwa wa kizalendo wenye kuonesha kujali maslahi ya Taifa na uhai wa watanzania,bora treni bovu linaweza kuharibika safarini likasimama na watu wasipate madhara makubwa,hali itakuwaje kwa "pangaboi" zetu ikiwa zikiwa na hitilafu na kuzifanya zihalibikie angani?

Maisha yetu yana thamani sana zaidi ya hizo "pangaboi" hakuna mtanzania yeyote awezaye kufa kwa sababu ya kutopanda "pangaboi" ila "pangaboi" mbovu zinaweza kuwa chanzo cha mauti yetu!Hili ni jambo la kuogofya sana.
Mkuu wacha utani nimekuvulia kofia kwa kutema madini.hongera sana na mwenye macho anaona
 
Hayo ni majarda tu wanayoyasoma ni kikundi tu cha watu....waandishi wake ni so subjective na biased!!!.

.....

Ustegemee gazeti la uhuru au tbc kurusha hbr unayotoa taarifa isiyo isifia serkali....kwani srrkali inafanya mema tu?
Hivi ile habari za Tanesco kutakiwa kuilipa Iptl haya magazeti yaliandika kweli?
 
Kwani habari na uhuru sio magazeti we mbulula?
Watanzania kadhaa wanasema Habari Leo na Uhuru sio magazeti, bali ni vipeperushi vya propaganda za magamba.
Kwa sasa hayauziki wala hayanunuliki kabisa. Serikali ianze tu utaratibu wa kuyagawa bure.
 
Dkt Magufuli hatoshishindwa kwa sababu ktk maisha yake hajawahi kushindwa! Nyie wanafiki wa chama mfu chandomo mnaweza kupiga mayowe na makelele ila lazima ashinde tu! Dkt Magufuli ni mkono wa Mungu, ndiyo maana kila goti lazima lipgwe, kila jiwe lazima lipinduliwe! Poleni sana kama mnasubiri ashindwe kwani mtakufa kwa presha enyi wanafiki na waongo
Huna ujuwalo zaidi ya ujuvi tu
 
Huko siyo kushindwa. Kwenye samaki alishinda kwa kuwakamata wahusika, kwenye kivuko alishinda kwa kukinunua, kwenye sukari alishinda kwa kufanikisha upatikanaji wa sukari, kwenye nyumba alifanikisha kuipunguzia serikali mzigo wa ukarabati (ndiyo maana hata akina Mzee Lowasa na Sumaye wanazo hizo nyumba).
00000
 
Bora tungewekeza kwenye usafiri wa reli ambao wananchi wengi wanatumia ndege waachie mashirika binafsi kama precision fastjet nk
Watanzania huwa nawashangaa sana kiukweli..kuna wakati watu walilaani kwanini serikali inashindwa kuwa na ndege zake leo hii ndege zimenunuliwa hao hao wanaanza kugeuka na kusema wasingenunua na badala yake wangeimarisha usafiri wa reli...kisa eti ni watanzania wachache wenye uwezo wa kupanda kwani hyo reli itapita mikoa yote?
Je wa Mtwara nae si atakuwa anaonewa?

Tuache kutafuta kuikosoa serikali tu kwa kila jambo...basi hata lile daraja la kigamboni lisingejengwa kwakuwa linatumiwa na watanzania wachache tu na badala yake wangenunua dawa wakagawa mahospitalin naamini wengi tungenufaika nazo
 
Hii ndege wanajitahdi kuipamba ila behind the scene kuna mtu kapiga pesa hapa. Ngoja time will tell
 
Haujui zile Dreamliner za Kenya zilivyokuwa zinawasili zilipewa promo hadi wa Tz tulijua. Nyie ni kama vichawi kazi yenu ni kuiombea mabaya nchi yenu halafu mnajiita wazalendo, hasara hii kwa taifa.
Dream Liner! You can say the name again. Hiyo ilikuwa news kwa mashirka yote makubwa yalipozinunuwa!

Ikiwa kisima cha kamba na dumu ni news worthy katika hii nchi, sishangai kwa ndege hata kidogo.
 
Watanzania kadhaa wanasema Habari Leo na Uhuru sio magazeti, bali ni vipeperushi vya propaganda za magamba.
Kwa sasa hayauziki wala hayanunuliki kabisa. Serikali ianze tu utaratibu wa kuyagawa bure.
Mimi hata nikikuta wanayagawa nageuza njia
 
Aisee jo nasikia ndage yenyewe ni Mtumba....
 
Back
Top Bottom