RRONDO
Platinum Member
- Jan 3, 2010
- 60,005
- 137,632
1.Kenyatta kama mfuatiliaji lazima ajue, hata hivyo inayonunua kama ulivyosema ni KQ si Kenyan government wakati hizi ndege mbili zimenunuliwa na serikali ya tz kwa ahadi ya JPM.Nawshukuru wahariri wa magazeti ya Tanzania, kiukweli haikuwa habari ya umuhimu kiasi hicho. Kumbuka kuna magazeti yaliyotutayarisha mwezi mmoja kabla kwamba ndege hii itwasili! Hivi Kenya Airways wakinunua ndege Kenyata anaweza kujua?
Ukiachilia mbali wananchi, hivi magazeti ya Kenya yanaweza kuiweka habari hiyo front page? Sijui hata kama yanaweza kujua Kenya Airways wamenunua ndege mpya.
Tuache kuionyesha dunia kwamba inawezekana sisi ni masikini kuazia mifukoni hadi vichwani. Tunashangilia kununua ndege ambayo watanzania 99% hawawezi kuipanda?
Ali Kessy (Mb) aliwahi kusema hawezi kushangilia mkoani kwake kujengwa uwanja wa ndege wakati inapandwa na waziri mkuu tu (Pinda wakati huo) na wananchi wake hawawezi hata kununa baiskeli.
Asante wahariri wa Tanzania isipokuwa Uhuru na Habari Leo
2.Kushangilia huko unakokushangaa ni kwasababu tumejitutumua kununua vindege viwili wakati kwa muda mrefu hatukuweza kufanya hivyo. KQ hawawezi kushangilia kama sisi kwasababu washapita hatua hii miaka mingi iliopita.
3.Walioipa hii habari kipaumbele na kuwa habari ni wale wanaoziponda hizi ndege. % kubwa ya habari zibahusu ndege hizi ni kuponda. Jivunie mafanikio yako hata kama ni madogo.