Mafanikio ya rais Samia siku 78 tangu ashike madaraka

JOYOPAPASI

Senior Member
Jan 10, 2016
175
500
YALIYOJIRI LEO JUNI 5, 2021 DODOMA, WAKATI MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MASUALA MBALIMBALI YA SERIKALI.

Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa imani yake kwangu na kuniteua kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Nawashukuru waandishi wa habari, wahariri na wadau wa wote wa habari ambao wameendelea kutekeleza jukumu la kutoa taarifa mbalimbali ambazo waandishi wa habari mmekuwa mkizihitaji.

Leo ni siku 80 tangu tuondokewe na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Na ni siku 78 tangu Mhe. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya 6.

Tunamshukuru Mungu kwa nchi yetu kuheshimu Katiba na utawala wa Sheria, baada ya kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Serikali, mchakato wa aliyekuwa Makamu wa Rais ulifanyika na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa amani na utulivu mkubwa na sasa tunaye Mhe. Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

HALI YA SERIKALI

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kuongoza nchi, kusimamia ulinzi na usalama, kusimamia rasilimali za Taifa.

Kwa niaba ya Serikali napenda kuwashukuru Watanzania wote kwa kuendelea kuwa na imani na Serikali yao, kushirikiana nayo na kutekeleza masuala mbalimbali ambayo wanapatiwa kama mwongozo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na mipango mbalimbali.

Uzalishaji mali unaendelea, pamoja na kwamba dunia inatikiswa na janga la virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Korona (Uviko-19) na uzalishaji wa maeneo mengi umetikiswa kwa kiasi kikubwa.

Serikali inaendelea kuwahimiza Watanzania wote kuendelea kuchapa kazi za uzalishaji mali kwa juhudi na maarifa huku wakichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona, zikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka.

HALI YA UCHUMI

Hali ya Uchumi wetu ni nzuri japo na sisi tumepatwa na madhara ya Korona kama ilivyo kwa nchi zingine dunia. Uchumi wetu uliokuwa unakua kwa wastani wa asilimia 6.9 umeshuka kidogo hadi wastani wa asilimia 4.7, na matarajio ni kuwa uchumi wetu utaendelea kukua vizuri kutokana na hatua madhubuti ambazo zimechukuliwa.

Mfumuko wa bei kwa sasa ni wastani wa asilimia 3.3% ambayo ni kiasi kizuri. Akiba ya fedha za kigeni ni nzuri ambazo zinatosha kununua bidhaa na huduma kwa muda wa zaidi ya miezi 4.7.

MAENDELEO YA MIRADI YA KIMKAKATI

Mhe. Rais ambaye ni Mkuu wa Serikali ameshatoa msimamo wake wa uongozi kwamba ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na watangulizi wake yaani Marais Wastaafu na waliotangulia mbele za haki na ataanzisha miradi mipya.

Reli ya kisasa/Standard Gauge Railway (Dar es Salaam – Morogoro (km 300) 91%, Morogoro – Makutupora (km 422) 61% na ujenzi wa reli Mwanza – Isaka umeanza ambapo Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 372.34 za ujenzi wa kilometa 341 za reli hiyo.

Bwawa la Julius Nyerere katika mto Rufiji ujenzi wa mradi umefikia 52% kutoka asilimia 45.

Ununuzi wa ndege ambapo ndege 8 zipo, na ndege 3 zitafika wakati wowote kuanzia sasa.

Ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi mkoani Mwanza umefikia 27% ikiwa ni mradi utakaogharimu shilingi Bilioni 712 hadi kukamilika kwake Februari 2024.

Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam daraja la Tanzanite 77.19%, Flyover za Chang’ombe na Kurasini, BRT 2 (barabara ya Kilwa), DMDP, upanuzi wa barabara ya Morogoro, huku kote kazi zinaendelea.

Ujenzi wa meli Mv- Mwanza (Hapa Kazi Tu) umefikia 74%. Na katika mwaka wa huu kuna mikataba 9 ambapo ujenzi wa meli mpya 3 zitajengwa katika maziwa makuu, meli mpya 1 katika Bahari ya Hindi. Pia kutakuwa na ukarabati wa meli 5 katika maziwa ya Victoria na Tanganyika.

HUDUMA ZA KIJAMII ZIMEENDELEA KUTOLEWA KAMA KAWAIDA

Afya, kati ya Machi na Juni, 2021, Kibali cha ajira kwa watumishi wa umma 4,127 kimetolewa kwa Wizara ya Afya.

Serikali imetoa shilingi Bilioni 121.3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa zinazokwenda katika mikoa mbalimbali na Shilingi Bilioni 43.5 zimetolewa kwa ajili ya ukamilishaji wa Hospitali za kanda, za rufaa za mikoa.

MOI imeanza kutoa matibabu ya kibingwa ya upasuaji wa ubongo bila kufungua kichwa pamoja na kupandikiza figo, kuzibua mishipa ya moyo kwa tundu dogo, upasuaji wa nyonga, magoti, kibiongo na mfumo wa fahamu.

Vifaa tiba vimeendelea kupelekwa katika hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Sekou Toure Mwanza vifaa vilivyopelekwa ni CT Scan, Ultra Sound sawa na Shilingi Bilioni 2.228; Bugando imepelekwa MRI ya Shilingi Bilioni 2.43; Mwananyamala CT Scan ya Shilingi Bilioni 1.444 na vifaa vingine vimesambazwa katika hospitali za rufaa za mikoa na hospitali za wilaya.

KUHUSU UGONJWA WA KORONA (UVIKO-19)

Mheshimiwa Rais ameamua kuimarisha juhudi za kupambana na janga la Korona kwa kutoa nafasi kwanza kwa Wataalamu wetu wakiongozwa na Prof. Said Aboud kufanya tathmini ya kitaalamu na kuishauri Serikali juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.

Mheshimiwa Rais amekabidhiwa mapendekezo hayo yenye mpango kazi wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na janga la ugonjwa wa Korona (Uviko-19).

Mapendekezo ya mpango kazi wa uratibu wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo yaliyowasilishwa na kamati ya wataalamu aliyoiunda kwa ajili ya kuishauri Serikali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Balozi na taasisi mbalimbali za Kimataifa hizi zimeruhusiwa kuleta chanjo kwa ajili ya raia wa nchi zao na watumishi wao.

UKUSANYAJI WA MAPATO

Ukusanyaji wa kodi unakwenda vizuri, na Serikali inawapongeza Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kulipa kodi. Kodi ni maendeleo.

Mwenendo wa Makusanyo ya Kodi kuanzia Januari 2021 hadi Machi 2021. Mwezi Jan 2021: malengo yalikuwa Tril. 1.68, makusanyo Tril. 1.34 sawa na asilimia 79.8; mwezi Feb 2021: malengo yalikuwa Tril. 1.61, makusanyo Tril. 1.33 sawa na asilimia 82.9; mwezi Machi 2021: malengo yalikuwa Tril. 1.99 makusanyo Tril. 1.67 sawa na asilimia 84.1; mwezi April 2021 malengo yalikuwa Tril. 1.61 makusanyo Tril. 1.34 sawa na asilimia 83.2 na mwezi Mei 2021: Malengo 1.619 makusanyo yalikuwa 1.33 sawa na asilimia 82.

Serikali inakusanya kodi kama kawaida kwa ajili ya kuendesha shughuli zake na kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo kugharamia mishahara, kuhudumia deni la Taifa, kugharamia miradi ya maendeleo.

KATIKA MASUALA YA DIPLOMASIA


Nchi yetu imeendelea kutekeleza vizuri diplomasia yake ya uchumi. Tumeona jinsi Mhe. Rais anavyochukua hatua madhubuti za kuimarisha uhusiano wetu na nchi mbalimbali dunia. Na dhamira ni kuwa Tanzania isiende pekee yake lazima kwenda na wenzetu.

Ziara 2 alizofanya nchini Uganda na ziara rasmi ya Rais wa Uganda hapa Tanzania matokeo yake ni kukamilika kwa mchakato wa kimikataba wa utekelezaji wa mradi Dola Bilioni 4.16 wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga Tanzania lenya urefu wa kilometa 1,443 ambapo kati yake kilometa 1,147 zinapita Tanzania katika mikoa 8 na Wilaya 24.

Manufaa ya mradi huu kwa nchi yetu ambayo licha ya kumiliki asilimia 15 ya hisa zote za kampuni, kutakuwa na ajira takribani 10,000 zitazalishwa, kutakuwa na mrabaha wa asilimia 60, na kutakuwa na kodi nyingi ambazo tutazipata. Mradi huu sasa upo tayari kuanza ujenzi na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 36.

Ziara rasmi ya Kenya, imeimarisha zaidi uhusiano wetu na Kenya. Hivi sasa wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya wanafanya biashara zao bila vikwazo na kupitia jukwaa la wafanyabiashara lililofanyika Jijini Nairobi.

Mchakato wa kujenga soko la pamoja mpakani ili wafanyabiashara wa Tanzania wasilazimike kuzifuata bidhaa ndani ya Kenya bali watazipata katika soko la pamoja linalojengwa na wafanyabiashara wa Kenya hawatalazimika tena kuingia vijijini kutafuta mazao watapelekewa sokoni mpakani.

Mhe. Rais ameshiriki mkutano kwa njia ya mtandao ulioitishwa na Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron kujadili juu ya athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga la Korona Barani Afrika na namna nchi zilizoendelea na mashirika ya kimataifa yanaweza kusaidia kuokoa uchumi wa nchi za Afrika.

IMF imepanga kutumia Dola za Marekani Bilioni 650 katika awamu ya pili ya mpango wa kusaidia kwa dharura uchumi wa nchi mbalimbali zinazoendelea kutokana na madhara ya janga la korona, ambapo Mhe. Rais ameagiza Wizara ya Fedha kuandaa maandiko ili nchi yetu inufaike na mpango huu.

Mhe. Rais ameshiriki mazungumzo na mtandao wa viongozi wanawake wa Afrika. Mtandao huu unaongozwa na Rais Mstaafu wa Liberia Mhe. Ellen Sirleaf, pamoja na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Antonio Gutterres.

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Mhe. Rais aliagiza kufunguliwa kwa Televisheni Mtandao na hakuagiza kufunguliwa kwa vyombo vyote kama ambavyo baadhi yetu tulikuwa tunapotosha juu ya kauli ya Mhe. Rais.

Rais alisisitiza kwamba vyombo vya habari vifanye kazi kwa uhuru na kuzingatia sheria na taratibu. Sheria ya huduma za Habari ya mwaka 2016 ipo na inaendelea kufanya kazi.

Vyombo vya habari ambavyo vimefungiwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameshatoa maelekezo kuwa wamiliki wa vyombo hivyo wawasilishe hoja zao ili zisikilizwe na kufanyiwa na utekelezaji wa agizo hili unaendelea kufanyika na baadaye Serikali itaamua.

SEKTA BINAFSI

Serikali inawapongeza na kuwatia moyo wafanyabiashara na wawekezaji wote waliojitokeza kufanya biashara na kuwekeza hapa nchini kwetu. Sekta Binafsi ni injini ya uchumi wetu, inazalishaji ajira, inaleta kipato kwa Serikali na inaimarisha ustawi wa wananchi.

Mhe. Rais Samia amekuwa kinara kwenye eneo hili na tayari ametoa maelekezo kadhaa ya kuhakikisha sekta binafsi inaimarika kwa kuondoa vikwazo vya kikodi na visivyo vya kikodi, unyanyasaji dhidi ya wafanyabiasha na kujenga miundombinu inayohitajika.

Mhe. Rais amekutana na viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) amepokea mawazo yao na ameahidi kuyafanyia kazi. Pia wakati wowote kutafanyika mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara (TNBC) ambao yeye Mhe. Rais ni Mwenyekiti na matarajio ni kuwa masuala muhimu ya kuboresha biashara na uwekezaji yatajadiliwa.

Serikali sasa imeamua kuwatelekeza wafanyabiashara wadogo (Machinga, Mama Lishe n.k) wote mmeona juzi tu Mhe. Rais alikuwa Soko la Kariakoo ambako amejionea mazingira ya wafanyabiashara wadogo na ameahidi kufanyia kazi changamoto zinazowakabili.

BANDARI YA DAR ES SALAAM


Upanuzi unaendelea katika gati namba 1 hadi 7 ambapo gati namba 1 hadi 5 ujenzi wake umekamilika na zinafanyakazi na ujenzi unaendelea katika gati namba 6&7 unaotarajiwa kukamilika mwezi wa 8, 2021.

Ufanyaji kazi wa Bandari unaongezeka ambapo idadi ya meli zinaongezeka na mapato yanakua, mwezi Aprili mapato yalikuwa Shilingi Bilioni 73.2, Mei Shilingi Bilioni 84.6 na hiki ni kiwango kikubwa ikilinganishwa na mapato ya mwezi Machi ambapo yalikuwa shilingi Bilioni 80.2.

UTALII


Nchi yetu imechukua hatua madhubuti za kuulinda utalii kwa kuzingatia miongozo na masharti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) dhidi ya ugonjwa wa Korona kwa kuwahakikishia watalii usalama wao wakiwa hapa Tanzania katika vivutio vyetu vya utalii.

Matarajio yetu ni kuwa watalii watazidi kuongezeka na mmeona watu maarufu duniani wanakuja

Imeandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO

IMG_20210605_184050_123.jpg
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,613
2,000
Sawa kazi iendelee,
Lakini Ndugu. Msigwa ungetupa na taalifa ya ajali mbaya iliyotokea kwenye mapagala na Raisi wetu kule Dodoma maeneo ya Kijiji cha Zanka,wakati akielekea Babati,Gali la polisi limegongana uso kwa uso na Basi dogo la abiria,nimeshindwa kupost tukio hilo,sababu nilikuwa kwenye basi.

Majeruhi ni wengi sana na pia Kuna vifo.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,093
2,000
Nafasi ya Ukurugenzi wa Mawasiliano Ikulu haiachii tu? Mambo ya kupeana nafasi 2 kwa mpigo sio vyema kabisa, keki ya Taifa ni yetu sote
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,290
2,000
Angalau makusanyo ya Kodi yanalidhisha, Hongera awamu ya 6, Hongera Sana Mh.SSH, Kazi na iendelee!
 

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,859
2,000
Sawa kazi iendelee,
Lakini Ndugu. Msigwa ungetupa na taalifa ya ajali mbaya iliyotokea kwenye mapagala na Raisi wetu kule Dodoma maeneo ya Kijiji cha Zanka,wakati akielekea Babati,Gali la polisi limegongana uso kwa uso na Basi dogo la abiria,nimeshindwa kupost tukio hilo,sababu nilikuwa kwenye basi.

Majeruhi ni wengi sana na pia Kuna vifo.
Hebu tulia andika vizuri taarifa haieleweki
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
718
1,000
safi ila ungegusia na lile la wezi wa mafuta wa Kigamboni, kulikoni mbona hawajakamatwa mpaka sasa wakati magari yaliyo kutwa yana usajili?
je document zilizo kutwa hazikuweza kuwasaidia kuwakamata?
Ukimia huu utafanya uvumi unao enezwa kuwa ni vigogo kuwa ni kweli.
 

Ramo

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
1,598
2,000
Hilo swala la Corona mh raisi anatakiwa asiwalazimishe watu kuchoma aisee..
 

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,882
2,000
Kipindi cha Magufuli wakitoa makusanyo watu wanalalamika changa la macho.
Leo naona kila mtu kimya!!!
 

mgoloko

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
4,786
2,000
Kweli, kumbe inawezekana bila task force, wala kutekana, kufungiana akaunti na kuchukua fedha za watu kwa nguvu kupitia kwa DPP, na bado makusanyo kwenda sawa na enzi za yule

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
Biswalo mganga ana bahati ya kuwa DPP sababu ya ile meli iliyoozea bandarini kutetea upumbavu wa Magufuri vinginevyo bila hayo madaraka angekuwa nyumbani au jela kwa kuelekezwa kupola fedha za watu
 

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,099
2,000
Msemaji mkuu wa serikali bwana Gerson Msigwa amesema kazi inaendelea kila kona na miradi yote ya kimkakati iliyoachwa na hayati rais Magufuli inaendelea kujengwa kama ilivyopangwa.

Msigwa amesema rais Samia ameidhinisha billioni 371 kwenda kuanza ujenzi wa SGR mkoani Mwanza kuelekea Isaka mkoani Shinyanga.

My take:
Hao walioapa kuuwa legacya ya Magufuli wameshindwa? Inakuwaje miradi yote bado inaendelea kujengwa tena kwa kasi zaidi?
View attachment 1810421
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,344
2,000
Hakuna aliyeapa kuua legacy ya JPM, acha siasa za kijinga bosi liko wazi. Yale mema yataendelezwa kwa namna nzuri tu na yale maovu yataachwa na hatua kuchukuliwa kwa wote waliyoyatenda.

SGR ilishaanza kujengwa na hela imeshalala pale tayari japo wazo lilikuwa zuri ila utekelezaji wake ulikuwa mbaya, ni hasara juu ya hasara kuucha ule mradi na hakuna namna zaidi ya kuumalizia maana ulishaanza na hela nyingi ilishatumika japo unalikamua Taifa.

Binafsu sikuunga mkono ujenzi wa SGR wakati hata ile meter gauge ilitushinda kuiendesha kwa ukosefu wa maarifa na akili na matokeo yake tukaiua, tungepump hela kidogo kuiimarisha ili meter gauge ya mkoloni na kuiongezea ufanisi walau ifike hata 80% then yenyewe ingetusaidia kuijenga SGR kidogokidogo kwa miaka kadhaa, badala ya kuwakamua wanyonge na kupump trilioni za hela huko kwa ahadi ya wanyonge kufaidika siku za usoni.
 

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,099
2,000
Hakuna aliyeapa kuua legacy ya JPM, acha siasa za kijinga bosi....liko wazi, yale mema yataendelezwa kwa namna nzuri tu na yale maovu yataachwa na hatua kuchukuliwa kwa wote waliyoyatenda...

SGR ilishaanza kujengwa na hela imeshalala pale tayari japo wazo lilikuwa zuri ila utekelezaji wake ulikuwa mbaya, ni hasara juu ya hasara kuucha ule mradi na hakuna namna zaidi ya kuumalizia maana ulishaanza na hela nyingi ilishatumika japo unalikamua Taifa...

Binafsu sikuunga mkono ujenzi wa SGR wakati hata ile meter gauge ilitushinda kuiendesha kwa ukosefu wa maarifa na akili na matokeo yake tukaiua...tungepump hela kidogo kuiimarisha ili meter gauge ya mkoloni na kuiongezea ufanisi walau ifike hata 80% then yenyewe ingetusaidia kuijenga SGR kidogokidogo kwa miaka kadhaa....baadala ya kuwakamua wanyonge na kupump trilioni za hela huko kwa ahadi ya wanyonge kufaidika siku za usoni..
Tayari rais Samia ameanza ujenzi wa SGR mkoani Mwanza kwa wasukuma gang.
Je una lipi la kumwambia?
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,744
2,000
Acha ushamba wa kumtetea mwendazake.

kila kona katumaliza sasa subiri wakina SABAYA waanze kuropoka mauaji ya watetea haki km Ben Saanane, Aghondi, Mcomoro, kutekana nyara na kuumiza kina Lissu, Nape Nnauye kutishiwa bastola.

Nchi haikuwa huru kabisa, km hiyo SGR Mwanza Isaka jengeni tu hayo mabehewa muyavushe hewanimpaka Isaka. mnaacha kumalizia Makutupora Kigoma mnataka kwenu tu.

jaribu kuficha ujinga wako maana imebaki Historia ambayo hatutaiingiza vitabuni Dikteta wa Tanzania.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,890
2,000
Msutaji jifunge vitenge basi kwani anayeendeza kazi hataki uonevu bali maendeleo kwa wote
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,744
2,000
Tulia dawa ikuingie kenge wewe
Miaka 6 ya utawala wa Mwendazake ilikua ya Machozi, Jasho na Damu kwa Watanzania. Haya ni baadhi ya matukio niliyoyakumbuka kwa haraka, baadhi yalitokea nikiwa huko nyumbani na mengine yametokea nikiwa nimeshaondoka.

1. Alizika uhuru wa vyombo vya habari na kutia saini sheria kandamizi kwa vyombo vya habari. Vyomno vyote vililazimishwa kumuandika kwa kumsifu na kumpamba, kilichothubutu kumkosoa kilifungiwa.

2. Alitumia nguvu nyingi kupambana na upinzani na kutesa wanasiasa wa upinzani kwa kuwafungulia kesi za uongo mpaka leo bado wengi wapo jela kwa kesi za kisiasa za kubambikiziwa.

3. Aligawanya nchi kwa misingi ya ukabila, ukanda, uchama na udini na ubaguzi wa kijinsia. Serikali yake ilijaa watu wa kanda ya ziwa na 75% ya serikali yake ilijaa wasukuma watupu

4. Alikua na ubaguzi wa kijinsia na aliendekeza mfumo dume. Wanawake walikua 17% tu ya mawaziri katika serikali yake.

5. Alihakikisha wakuu wa vyombo vya ulinzi wanatoka kanda ya ziwa ili kumlinda likitokea lolote, CDF - Mara, IGP - Mara na CGP - Geita na CGF - Mwanza. Madikteta wote hufanya hivi maana wanajua watu wa kwao hawawezi kuwageuka.

6. Hakupandisha mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa miaka yote 6 ya utawala wake.

7. Hakutangaza ajira mpya katika kipindi chote cha utawala wake. Waalimu waliomaliza vyuo mwaka 2015 hadi leo wapo mtaaji jobless.

8. Aliua sekta binafsi kwa kutoza kodi kubwa, na kuharibu mazingira ya biashara. Hoteli nyingi za kitalii zimekufa kama vile Ngurdoto, Impala, Naura Spring na nyingine zimegeuka hostel za wanafunzi kama Landmark ya Ubungo.

9. Alipunguza mzunguko wa pesa mtaani na kuhakikisha matajiri wanaishi kama mashetani.

10. Katika utawala wake waliibuka watu wasiojulikana ambao waliteka, kujeruhi na kuua watu wasio na hatia. Watu hao walimpiga risasi Tundu Lissu mchana kweupe na mpaka leo hawajakamatwa.

11. Aliwapa nguvu baadhi ya viongozi kama vile Makonda na Sabaya kutesa na kuumiza wananchi kadri walivyojisikia. Makonda alishambulia kituo cha CMG kwa mitutu ya bunduki lakini hakuchukuliwa hatua yoyote. DC Sabaya majuzi kampiga diwani wa Sombetini nusura kifo.

12. Alifuta fao la kujitoa na kusababisha watumishi wengi wenye mikataba ya muda mfupi kuishi maisha magumu baada ya ajira zao kukoma.

13. Katika serikali yake Wapinzani walionekana maadui na sio watu wenye mawazo mbadala. Waliteswa na kufunguliwa kesi za uchochezi. Wengine walipotezwa na hata kuuawa. Alitamani upinzani ufe.

15. Katika utawala wake maiti 17 ziliokotwa ufukwe wa Coco na nyingine 6 ziliokotwa mto Ruvu kwa pamoja zikiwa zimefungwa kwenye sandarusi, na baadhi zikivuja damu.

16. Aliharibu mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengi ukimwenguni. Serikali yake ilichoma vifaranga vya kuku kutoka Kenya na kutaifisha ng'ombe waliovuka mpaka kuja Tanzania.

17. Alisababisha wanasiasa wa Tanzania wakimbie nchi na kuishi uhamisho kama wakimbizi wa kisiasa wakiwemo Ansbert Ngurumo, Tundu Lissu na Godbless Lema.

18. Alitumia mabavu kulazimisha ushindi kwenye uchaguzi wa 2020 na kuhakikisha CCM inashinda majimbo yote. Alipora ushindi wa upinzani kwenye majimbo mengi kwa mtutu wa bunduki.

19. Alitumia sheria ya uhujumu uchumi kutesa wapinzani wake kisiasa na wafanyabiashara aliokua na kisasi kwa mfano Rugemala na Lema wa Elerai Construction.

20. Alipenda kuabudiwa, kutukuzwa na kuogopwa. Wote waliomnyenyekea aliwapa vyeo.

21. Aliamini mawazo yake ndio sahihi na hakutaka kushauriwa kwenye jambo lolote. Aliwahi kusema yeye hapangiwi cha kufanya.

22. Alipenda kuonekana mcha Mungu japo kiuhalisia ni dikteta katili aliyetisha. Alimpoteza Ben Saanane baada ya kuhoji kuhusu PHD yake.

23. Alitangaza kuwa Tanzania haina corona na akataka watu wasivae barakoa wala wasikubali chanjo kutoka nje ya nchi.

24. Alipeleka miradi mingi ya maendeleo kijijini kwake Chato kama uwanja wa ndege, hospitali ya rufaa, benkiz barabara za lami na mbuga ya wanyama ambayo haikua na wanyama ikabidi kuhamisha kutoka mbuza zingine.

25. Aliingilia mihimili yote ya dola ikiwemo mahakama na bunge. Aliwazawadia vyeo vya ujaji mahakimu waliowafunga wapinzani jela.

26. Aliigeuza Tanzania kama mali yake binafsi na katika kila mradi alipenda atajwe yeye. Aliamini akiondoka hakuna atakayeweza kuendeleza yale aliyofanya. Bunge liliwahi kupendekeza kumuongezea muda wa kutawala atakapomaliza mihula yake miwili, kumbe Mungu ana mipango yake hata hiyo miezi 4 hakumaliza ya kura alizoiba


1.Chato International Airport
2.Chato National Park
3.Trafic light Chato
4.3 star hotel Chato (TANAPA)
5.Bohari ya kanda madawa Chato
6.Hospital ya rufaa Chato
7.Stadium (proposa)
8.CRDB Chato

Jana usiku nilienda kumtembelea mzee mmoja ambaye ni mtu wangu wa karibu anae jihusisha na biashara ya madini,akinipa story fupi tu ya rafiki yake ambayo ilinihuzunisha sana.

Jamaa yake alikua na zaidi ya bilioni 7 kwenye account yake bank mwaka jana mwanzoni,alipigiwa simu na branch manager aende urgently na alipofika pale mida ya mchana akajulishwa kwamba account yake imepigwa spana na tra (task force). Ikabidi aende tra mkoa ili kufuatilia hiyo ishu.

Tra mkoani wakamwambia inabidi awasiliane na TRA makao makuu,ikapigwa sim akapewa appointment saa tatu asubuhi next day. Akapanda ndege jioni hiyo kuelekea huko, asubuhi kafika mapema kasechewa kweli kweli then akaingia ofisini kuzungumza na team roho mbaya.

Wewe ndio fulani? Ndio, inaonekana una pesa nyingi sana kwa account ila hulipi kodi. Jamaa akasema akasema kodi nalipa na ninapata tax clearance kila mwaka mbona sielewi? Wakamwambia ana option 2 TRA wachukue 5B wamuachie 2 au akalete vielelezo huku wakiendelea kuzuia hela zote. Vielelezo visipo jitosheleza watachukua hela zote pamoja na kesi ya uhujumu uchumi.

Pale ulikua huruhusiwi kwenda na mwanasheria wala accountant,jamaa akatoka nje kufikiria kwa muda akaona isiwe nongwa akawaachia 5B lakini pia akaambiwa arudi CCM kwa kujitangaza kwenye media kwa sababu alikua supporter mkubwa wa lowasa uchaguzi wa 2015.

Matajiri wengi wa mawe wameumizwa sana huko kanda ya kaskazini ila wamekaa kimya tu,bora huyu jamaa amekufa maana alikua anatupeleka shimoni/motoni kiuchumi na kijamii.

Akasema nyumba za kimara zibomolewe lakini za mwanza zisibomolewe maana ni wapiga kura wake....Maiti zilikua zinaokotwa baharini enz za mwendazakeNitamkumbua Magufuli kwa ukatili wake wa kutisha

1. Kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara - Mbezi bila chembe ya huruma ila wale wa mwanza aliwaachia

2.Kupora Korosho za wananchi wa mikoa ya kusini kwa mtutu wa bunduki, hii hali iiwatia wananchi umasikini

3. Bila kujali kuwa watu wameshahudumu serikalini kwa muda mrefu na wanategemea kustaafu, akapitisha hoja ya uhakiki na kuwafukuza maelfu ya watu hao Huku akiwaacha bila kuwagusa wanasiasa na wateule wake katika hilo zoezi

4. Kubabikizia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatesa kupitia mfumo wa mashitaka na kuzisababishia familia zao maumivu makubwa na hali ngumu

5. Kuendelea kuwashikilia mamia ya masheikh walioko jela huku akisamehe wabakaji akina Babu Seya

6. Kukataa kuwapa watumishi wa serikai stahiki zao kwa wakati, ikiwemo kupandishwa madaraja na nyongeza za ishahara

7. Kuharibu chaguzi zote zilizofanyika chini ya serikali yake, kuanzia zile za marudio, serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Alidhuluu haki ya wananchi kuchagua viongozi wao

8. Magufuli alitunga sheria kandamizi, na kuvuruga misingi ya katiba. Kafanya kia jitihada kulifanya bunge liwe butu, kuiweka mahakama mfukoni etc

9. Magufuli alikuwa na kauli mbaya zisizo na staha mfano "sisomeshi wazazi, serikali siyo iliyoleta tetemeko, baki na mavi yako nyumbani, nitapiga mashangazi.. etc"

10. Alikuwa na miradi kadhaa au mpango wa miradi kadhaa ambayo ni white elephant mfano, uwanja wa ndege Chato, Midege,Mpango wa Uwanja wa mpira Chato

11..Magufuli alikuwa mkabila, huhitaji kuwa mwanasayansi wa elimu ya jamii kuona kuwa teuzi zake ziliaia sana watu wa kanda na kabila lake.

12. Magufuli alikuwa haheshimu katiba waa sheria pale zinapokinzana na anachokitaka yeye, mfano haki ya kufanya siasa kwa vyama vya siasa iliyokuwepo kikatiba hakuiheshimu

13. Magufulu hakuthubutu na wala hakujali kufanya uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na waliompiga risasi Lissu

Kwa hiyo mimi nakichukulia kifo cha Magufuli kama nafasi muhimu ili Taifa letu lipone.

Na sisi kama Taifa, tumeona kwa macho yetu namna katiba ya sasa ilivyokuwa hatari kama tunampata mtu mmoja asiyejali, ambaye ana element za udikteta, basi tuitumie nafasi hii kuliponya Taifa

Tangulia Magufuli, uwongo mbaya sitokumiss na sijawahi kukupenda kwa style ya uongozi wako, ninatamani Taifa lisipate Kiongozi mwenye mapungufu ya aina yako, ni mapungufu hatari kabisa
thanx kimsboy
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom