Magazeti yaipa kisogo ndege ya Rais Magufuli

Magazeti yaipa kisogo ndege ya Rais Magufuli

Hapa nina magazeti saba, Matano yameandika kuhusu ujio wa ndege. Tanzania Daima na Raia Mwema hayajaandika. Mtoa mada unaposema magazeti ya yameipa kisogo habari ya ndege wewe unaonesha kuwa jinga kabisa. Gazeti la Chama mfu CHADEMA tokea lini kikaandika kuhusu maendeleo ya Tanzania? Ni sawa na kuandika uhawara wa Mbowe na Mukya.
Yaani wewe badala uwepo kwenu karagwe usaidie kutindua vifusi eti unajitapa kuwepo dsm!
 
Hapa nina magazeti saba, Matano yameandika kuhusu ujio wa ndege. Tanzania Daima na Raia Mwema hayajaandika. Mtoa mada unaposema magazeti ya yameipa kisogo habari ya ndege wewe unaonesha kuwa jinga kabisa. Gazeti la Chama mfu CHADEMA tokea lini kikaandika kuhusu maendeleo ya Tanzania? Ni sawa na kuandika uhawara wa Mbowe na Mukya.
Chama mfu ni ccm
1474475423752.jpg
 
WaTz wenzangu ni watu wa ajabu sana.... Kipindi kile ndege hakuna kelele zilikuwa nyingi leo zimekuja majungu kibao
Lini kulikuwa na shida ya usafiri wa ndege kwa wananchi wake?
 
WaTz wenzangu ni watu wa ajabu sana.... Kipindi kile ndege hakuna kelele zilikuwa nyingi leo zimekuja majungu kibao
Mnashindwa kujenga na kuimarisha reli ya kati mnatuletea ndege,ni Watanzania wangapi wana uwezo wa kupanda ndege?
 
Mi mpaka sasa sijapata sababu za kibiashara kununua ndege na kuikabidhi kwa ATCL iliyoshindwa biashara na inayodaiwa. Kwa nini isifilisiwe kwanza halafu tukaanza upya? Hii biashara inalenga kuchangia pato la Taifa au kupunguza deni la Taifa au kuongeza deni la Taifa? wajuzi tueleweshane.
 
Tatizo lenu n wivu na roho mbaya na kutotaka mwenzenu afanikiwe mkijifariji kuwa akifeli mtashika nchi... si kwa upinzani huu uchwara unaoshnda unabwabwaja na kutoa matamko yasiyotekelezeka, wanafiki, waongo na vgeugeu leo wanasema hivi kesho vile... walipoti wasiripoti sisi tumemkubal huyu mheshiwa maana anatembea kwny maneno yake... na tutamchagua tena 2020
MHESHIWA ndio lugha ya wapi rwanda au?
 
Ndege zimeletwa kwa ajili ya sisi wasomi ambao hatukalii majungu JF tunajituma kwa kutumia akili , maarifa na uwezo tuliopewa na serikali yetu pamoja na kudra za Mwenyezi Mungu. Na kumbuka kwamba kila nchi Matabaka lazima na hatuwezi wote kuwa sawa kiuchumi. Maskini lazima muwepo ili mje kutupigia kelele za njaa zenu.

Serikali ina jali wananchi wake kwa kila Tabaka la uchumi Ndege zilizokuja ni kwa sisi wababe wa kifedha huwezi kupanda nenda kapande mabasi huwezi kuafford mabasi mmewekewa Bajaji na Bodaboda kwaajili yenu.

Elimu Elimu Elimu siku mkielimika na kuacha kutumiwa mtajisikia aibu sana kwa uppuzi mnaouleta humu.
Kwa wenye akili tumesha kupata
 
...i sweat to God tuna matatizo..kwani Ndege kununuliwa tatizo liko wapi. What do we want? Juzi tulikua tunataka ndege, leo haifai tena tunataka treni, treni ikija tutataka mabasi. Ee Mwenyenzi MUNGU usituhesabie dhambi sie watanzAnia. Tuna tatizo la kisaikolojia.
Hatujakataa kununuliwa ndege bali tumesema kuifanya story ya taifa
 
ATC ilianzishwa miaka 39 iliyopita ikiwa na ndege zake kumi mpya na mbili za kukodi. Sasa badala ya Watanzania kutafuta majibu ya nini kilichoifikisha ATC hapa ilipo (ambapo haina hata ndege moja) na kudai kupewa uthibitisho kwamba hii hali haitajirudia tena, wanatukuza na kushangilia pesa yao ya kodi kuunguzwa kwenye mradi ambao kiuhalisia hautakuwa na tija. Na kwa nini serikali ijiingize kwenye kufanya biashara moja kwa moja, tena ya rejareja, ilhali jukumu la serikali ni kukusanya kodi, kuratibu na kuweka mazingira mazuri ya shughuli za kiuchumi nchini?
Hilo nalo ni neno lenye maana kabisa,kama ndege 10 zilishindwa itakuwaje hizi 2?
 
Lakini nadhani Tanzania Daima linajiendesha na hatujasikia kama wafanyakazi wake wanakosa hata mishahara. Kama gazeti linajiendesha ina maana limekubalika na wateja. Gazeti la Uhuru na Mzalendo siyo chanzo cha habari, wananchi wameyakataa. Magazeti haya yatakuwa kati ya vyanzo vya ufisadi maana yanalazimishwa kununuliwa na ofisi za serikali.

Gazeti la Uhuru na Mzalendo, hayawezi kuwepo kama yakiachiwa hata kwa miezi 6 tu yajiendeshe yenyewe bila kuitumia serikali.
Sasa hivi yanasomwa lumumba tu hakuna wa kuyanunua kabisa
 
Ndege hiyo nilipoiona nikakumbuka enzi za mabasi ya Leyland - Sauti ya Mama!. Duh! Tanzania ndiyo tumerudi nyuma kweli kiasi hicho na kuwehuka nchi nzima eti tunashangilia ununuzi wa Leyland la angani!!! - Ndege ya pangaboi! tehe tehe tehe, nimechoka.
Umesahau na jina ALBION
 
Back
Top Bottom