BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Usiku huu, Aloyce Nyanda (Mtozi) amekuwa na kipindi muhimu katika Star TV usiku huu. Agenda Kuu ilikuwa ni Maadili ya Uandishi wa Habari kufuatia Vyombo vya Habari vya mataifa mengine kuripoti taarifa kuhusu Rais Magufuli pasipo kupata uthibitisho kutoka kwa wahusika yaani Serikali ya Tanzania.
Kwanza kabisa, ninataka kutangaza maslahi kabla ya kujadili hoja hii hapa. Nimesomea 'Sociology of Mass Media' na nilitafiti kidogo kuhusu namna Vyombo vya Habari vya Nchi zinazozungumza Kiingereza vilivyoripoti taarifa za Vita vya Ghuba vilivyomwangusha Rais Saddam Hussain wa Iraq. Niliangazia zaidi Magazeti katika nchi za Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Ghana, Malawi, Zambia, Nigeria, Tanzania, Zimbabwe, Botswana, New Zealand, Australia na Uingereza yenyewe. Niliangazia pia mashirika makubwa pia ya Reuters, CNN, BBC nk.
Baadhi ya niliyogundua ni kuwa kulikuwa na taarifa ambayo ilikuwa inaripotiwa na vyombo vyote kwa mtindo uleule hii ikiwa na maana kuwa kulikuwa na chanzo kimoja Kikuu cha Habari! Hii ina maana kuwa taarifa nyingi za Kimataifa ambazo hata Vyombo vyetu vya Habari hutangaza 'humegewa' na Mashirika Makubwa ya Habari Duniani!
Ninachoweza kusema ni kuwa Mashirika Makubwa ya Habari Duniani yanakuwa na vyanzo vya Habari ndani ya nchi kadhaa ambavyo vinaaminika hata kuliko nchi husika ambamo mashirika hayo huangazia. Kuna wakati ambapo nchi husika inaweza isijue taarifa kamili hadi itakapoambiwa na mashirika hayo. Hata hivyo, kama kuna urafiki na mahusiano mazuri kati ya mashirika hayo na nchi husika, Vyombo hivyo hutafuta uthibitisho kutoka mamlaka hata kama vinakuwa na taarifa kamili. Pale ambapo taarifa au habari zinahusiana na mambo ya kijasusi au katika nchi isiyo rafiki (closed countries) katika masuala ya Habari nk basi media au mashirika ya nje yanaweza kutangaza Habari pasipo kupata uthibitisho kutoka katika mamlaka husika. Nawarejeza wasomaji wangu jinsi ambavyo BBC inavyotoa taarifa zinazohusu nchi za Urusi, Korea Kaskazini nk.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini Deodatus Balile amejitokeza na kusema kuwa wao walijatahidi kutaka kupata taarifa kutoka Serikalini lakini hawakufanikiwa. Kama watu walioko nchini wanashindwa kupata taarifa kutoka Serikalini inakuwaje kwa Vyombo vya nje? Tunachotakiwa kujua hapa ni kuwa kama baadhi ya Vyombo vya Habari vya nje vinaichukulia Tanzania kama 'closed country' kwa masuala ya Habari, basi vinaweza kutoa pasipo kusubiri uthibitisho kutoka katika mamlaka za Tanzania.
Ni vizuri tukatofautisha kati ya media ya Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa ni 'pro government' na media za nje ambazo ni huru! Media za nje nyingi huuza habari kwa hiyo utoaji wake wa Habari utakuwa tofauti sana na media zetu ambazo wasikilizaji hawana mamlaka ya kuamua nini wasikilize.
Mtazamo wangu ni kuwa Tanzania siyo kisiwa katika ulimwengu huu. Sisi tusipokuwa tayari kutoa taarifa kwa wanahabari tujue kuwa media za nje zitachokonoa tu kwa kuwa na wao wana maslahi ya kiuchumi, kiusalama na nchi yetu.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula