Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

FAHAMU NI KWA NAMNA GANI VIONGOZI WA DINI WAMERAHISISHIWA KAZI ZAO NA UTAWALA WA RAISI DR. JOHN MAGUFULI.

Viongozi wa dini zote wanalojukumu kubwa la kujenga mioyo ya wanachi kwa kutekeleza yale Mungu anayoyataka na kuya acha yale Mungu anayokataza.

Hili linathibitika katika dini ya Kiislamu tunapo ambiwa katika Quar-an takatifu kuwa litoke kundi miongoni mwenu litakalowaamrisha watu mema na kuwakataza mambo mabaya (3:104).Vivyo hivo kwenye Bibilia …” tumepokea neema na agizo la kuwaongoza watu wa mataifa yote wasiomjua Mungu, wapate kumwamini na kumtii (Warumi 1:1-9:26).Hivyo utiii juu ya Mungu kwa kufanya mema na kuacha maovu ndio msingi mkubwa wa imani zote duniani.

Maovu duniani yanaongezeka na yamekuwa yakishangiliwa na kupewa chepuo kuliko mambo mema katika jamii.Mfano kijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kuoa limekua jambo la kawaida,ulevi,wizi,uzinzi,mavazi yasiyo na stara nakadhalika.Wimbi hili kubwa la kuongezeka maovu limeiweka dunia katika majanga mbalimbali yakiwemo maradhi,umaskini,ufisadi pamoja na kuondoka kwa amani katika jamii.

Mambo mengi ambayo Mungu anakataza yanahasara kubwa kuliko faida inayopatikana.Mfano uzinzi,dini zote zinakemea uzinzi kutokana na hasara zinazopatikana kwenye tendo hilo ambazo ni pamoja na magonjwa,ustawi wa jamii,kuzorota kwa uchumi nakadhalika.

Viongozi wa dini katika karne hii popote duniani wamekua na changamoto kubwa katika kuwaondoa waumini wao kutoka katika wimbi la maovu na kuwapeleka katika kumtii Mungu.

Katika awamu ya tano ya Raisi John Pombe Magufuli serikali yake imeweza kuwarahisishia Mapadri,Wachungaji,Mashekhe,Maimamu pamoja na viongozi wengine wa dini kazi zao za kuwaita waumini kumwabudu Mungu pamoja na kuondoa maovu katika jamii ya Watanzania.Uawala wa awamu tano umepambana vikali na kutoa matokeo ambayo hayajawahi kupatikana katika historia ya Tanzania tangu na kabla ya kupata uhuru.Hii imepelekea viongozi wa dini zote kumuunga mkono kwa dhati Raisi John Pombe Magufuli kwa kutamka hadharani na katika madhabahu na mimbari zao.

Dua kutoka kwa Mashekhe na Maimamu zimekua zikifanyika mara kwa mara katika miskiti kumwombea Raisi John Pombe Magufuli afya nje ili aweze kutekeleza majukumu yake.Mashekhe wakubwa kama Shekh Mkuu Mufti Zubeir pamoja na Mashekhe wengine kama shekh Kishki wamekua wakimuombea kutokana na kazi yake kubwa ya kuondoa maovu ndani ya jamii ya Watanzania kwa kutekeleza kwa uadilifu kazi yake ya uongozi wa nchi.

Viongozi wa Makanisa na Mapadri nao wamekua msatari wa mbele katika kuhakikisha wanafanya maombi kwa Raisi ili aweze kuyatekeleza majukumu yake.Mchango huu wa viongozi wa dini kwa Raisi umekua ukimfariji na kuona vita aliyonayo dhidi ya machafu yaliyoidumbukiza nchi katika wimbi la umaskini inaungwa mkono na waumini wengi.

Ni ndani ya mwaka huu katika mashindano makubwa ya Kimataifa yaliyohusiha washiriki wan chi zote Africa ya Qur-an Mashekhe walitumia fursa hiyo kumwombwea Raisi John Pombe Magufuli.

Kwa uchache tuyaangalie mambo makubwa amabyo yamerahisisha kazi za viongozi wa dini na kuwafanya wawe na imani na serikali ya wamu ya tano chini ya Uongozi wa Raisi John Magufuli kama yafuatayo:-

1.Madawa ya Kulevya.
Janga la madawa ya kulevya kwa nchi ya Tanzania hasa maeneo ya mijini lilikua kubwa na la kuogopesha,madawa ya kulevya yaliuzwa wazi mchana kweupe na wale waliokuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu walijulikana na vyombo vya usalama.Watoto wengi wa Kitanzania waliangamia katika janga hili la madawa ya kulevya.

Baada ya Raisi Magufuli kuingia madarakani,vita ya kweli dhidi ya mtandao wa madawa ya kulevya ilipiganwa kwa dhati ambapo iliwagusa wafanyabiashara wakubwa na wakati.Hivi sasa biashara hiyo imekaribia kuisha kabisa na vijana wengi walioathirika wanapata matibabu.

2.Mapenzi ya jinsia moja
Dini zote zinakataza mapenzi ya jinsia moja,licha baadhi ya wanasiasa kuhamasisha utamaduni huu kwa manufaa yao binafsi,utawala wa Raisi John Pombe Magufuli umeweka wazi kuwa Tanzania ni nchi Takatifu kwa maana ushenzi huo haukubaliki na hatua za kisheria zitachukuliwa wale wote wanaofanya biashara hizo.

3.Ufisadi
Ufisadi ni chukizo mbele ya Mungu kwani unaleta maangamizi kwa jamii kwa kuikosesha mahitaji yake pamoja na kuangamiza makundi ya watu wengi.Ufisadi umepigwa vita katika awamu zote za uongozi,lakini awamu ya tano imeupiga vita na kutoa matokeo makubwa ambayo hayakuwahi kupatikana tangia kupatikana kwa Uhuru.

4.Rushwa
Rushwa huhubiriwa katika makanisa na misikitini ili waumini waondokane na hili janga ambalo linawakosesha wenye haki kupata haki zao.Awamu ya tano ya uongozi wa Raisi John Pombe Magufuli imepambana na Rushwa kiasi cha kushtusha jamii za kimataifa.Wanchi wanapata haki zao na hakuna dhulma inayofanyika kwa misingi ya rushwa.Wapo wanachi wachache ambao bado wanaendelea na uovu huu kwa njia ya siri kubwa.

Raisi Magufuli amaweka msisitizo kwenye masuala ambayo Mungu anayataka,mfano wa mambo ambayo ni kipaumbele cha Raisi Magufuli nikama yafuatayo:-

1.Elimu
Elimu ndani ya dini ya Kiislamu imepewa kipaumbele kikubwa kwa kufanywa aya ya kwanza kumshukia Mtume Mohamad.Mtume Muhamad aliambiwa soma kwa jina la Mola wako.

Raisi Magufuli amefanikisha kufanya elimu ya awali,elimu ya msingi mpaka sekondari kuwa bure kwa wanchi wote wa Tanzania.Raisi ameimarisha miundombinu ya masomo mashuleni kwa kuongeza madarasa,walimu pamoja na mahitaji mengine muhmu ya utoaji wa elimu.

2.Uwajibikaji
Watumishi wa umma wanawajibika kwa kutoa huduma kwa wananchi jambo ambalo ni la msingi kwa serikali yoyote ya wanachi.Urasimu serikalini umepungua kwa kiwango kikubwa na huduma kwa wanchi zinafika kwa wakati.

3.Miradi ya maendeleo
Serikali ya awamu ya Tano imekua ikitatua changamoto za kimaendeleo kwa wanchi kwa kuanzisha miradi ya kimaendeleo.Miradi mingi ya kimaendeleo imeanzishwa na wanachi wamekua wakiridhishwa na miradi hii.

Nimtakie Raisi wetu Afya Njema ili aweze kuendelea kuwatumikia wananchi
 
Wasalamu ndugu zangu,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosomeka, mimi kwangu napenda kumleta kwenu His Ex. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa jamhuri ya Muungano Tanzania kama nominee katika ushujaa wa upambanaji wa rushwa hapa afrika.

Tumpe sapoti mkuu wetu wa nchi azidi kuyatenda yale yaliyomema kwetu.

Kataa rushwa.. usitoe,usishawishi wala kupokea.
 
One in four people in Africa pay bribes to access services, survey says

Global Corruption Barometer – Africa, released on African Anti-Corruption Day by Transparency International in partnership with Afrobarometer, reveals that more than half of all citizens surveyed in 35 African countries think corruption is getting worse in their country. Fifty-nine per cent of people think their government is doing badly at tackling corruption.

Hii vita ni kubwa, Rais ameonyesha njia. Asibaki mtu nyuma tusonge nae katika kuikabili.
 
Anti Corruption hero? Which corruption are you talking about? 😳




Wasalamu ndugu zangu,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosomeka, mimi kwangu napenda kumleta kwenu His Ex. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa jamhuri ya Muungano Tanzania kama nominee katika ushujaa wa upambanaji wa rushwa hapa afrika.

Tumpe sapoti mkuu wetu wa nchi azidi kuyatenda yale yaliyomema kwetu.

Kataa rushwa.. usitoe,usishawishi wala kupokea.
 
Mnasifia ujinga sana nyie wapuuzi.
1. Mnyeti kununua madiwani.
2. Makonda kuingiza makontena ya samani za ofisi za mabilioni.
3. Kumzuia CAG kufanya kazi yake kwa kumtumia spika.
4. Upotevu wa tril 2.5 usio na majibu.
5. Ujenzi wa kifisadi usiofuata sheria za nchi,Chato airport,Ukuta Mererani n.k
6. Ununuzi wa wabunge wa upinzani na madiwan.
7.Rushwa ya Kangi Lugora na kuzawadiwa uwaziri.
8. Kumteua ndugu yake hazina.

Magufuli atavunja rekodi ya ufisadi toka kuumbwa kwa Tanzania.
 
Natengeneza Fraud-fighting System/Application inaitwa "JPM Fraud Fighter"...kwa kuanzia,pamoja na mambo mengine hii tool itakuwa na uwezo wa kuzuia au kugundua ghost employees na ghost students.
 
Wasalamu ndugu zangu,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosomeka, mimi kwangu napenda kumleta kwenu His Ex. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa jamhuri ya Muungano Tanzania kama nominee katika ushujaa wa upambanaji wa rushwa hapa afrika.

Tumpe sapoti mkuu wetu wa nchi azidi kuyatenda yale yaliyomema kwetu.

Kataa rushwa.. usitoe,usishawishi wala kupokea.
huyu anayenunua wabunge na madiwani na wengine kuwahonga vyeo kama Mtatiro na Dr Slaa ?
 
Heroes and Heroine of corruption in Tanzania.

MEMBERS OF THE WARIOBA ANTI~CORRUPTION COMMISSION.

[Ndio kulikuwa na mwanamama mmoja kwenye ile tume ingawa hatajwi sana]
 
Back
Top Bottom