Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,143
Kwa siku za karibuni hapa JF kuna mjadala mkali sana unaendelea kuhusu taaluma ya ufamasia na maduka ya dawa hapa Tanzania. Kupitia mijadala hiyo, nimejifunza mambo kadhaa ambayo hapo kabla sikuyajua kwa kina. Nimegundua mambo haya:
1. Mtu ili kuanzisha na kuendesha biashara ya duka la dawa, huihitaji uwe ni mfamasia kitaaluma bali unahitaji kukodisha cheti cha mfamasia yoyote na kukitundika kwenye duka lako la dawa, na kuanzia hapo utauza dawa yoyote hata kama elimu yako ni darasa la saba! Hii ni sawa na rubani mwenye leseni ya kurusha ndege za abiria kuikodisha leseni yake kwa kampuni ya ndege ili itundikwe ndani ya ndege, halafu mtu yoyote anaweza kushika usukani wa ndege na kuamua kuirusha ndege!
2. Kumbe wafamasia kitaaluma hawajui (hawakufunzwa) na hawapaswi kumpima mgonjwa (examination), kugundua ugonjwa (diagnosis), kuidhinisha dawa za kutumia (Prescription) au kumtibu mgonjwa kwa dawa (drug administration). Mfamasia anapaswa tu kumgawia mgonjwa dawa (drug dispensing) kwa mujibu wa kibali cha Daktari. Ajabu ni kuwa huku mitaani maduka ya dawa ndio hospitali zisizo rasmi, tukiumwa tunaenda na pesa kwenye duka la dawa na kutibiwa faster!
3. Kiujumla karibu dawa zote hazipaswi kuuzwa na duka lolote la dawa mpaka kibali rasmi cha dawa kutoka kwa Daktari (Prescription). Ajabu ni kuwa huku mtaani dawa yoyote unaweza ukauziwa na duka lolote la dawa ukienda na pesa tu!
Baada ya kupitia hayo yote nimegundua wazi kubwa, kiujumla maduka ya dawa hapa Tanzania huenda kwa sehemu kubwa yanatuibia, kutuumiza, kuharibu afya zetu na kutuua!