Ummy: Msimamo wangu TMDA wasimamie Maduka ya Dawa, Baraza la Famasia libaki kwenye taaluma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema “Msimamo wangu tubadilishe Sheria ili Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) ndio isimamie maduka ya Dawa kisha Baraza la Famasi libaki kusimamia taaluma, TMDA ina nguvu na inaweza kufanya kazi."

mesema hayo Novemba 17, 2023 katika Kongamano la Tatu la Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa Mkoani Arusha ambapo amesisitiza kuwa hadi Januari 15, 2024 pendekezo hilo liwe limefika kwake ilia aliwasilishe kwenye Baraza za Mawaziri.

Kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com, Mdau alilalamika kuwa baadhi ya Maafisa wa Ofisi ya Mfamasia Mkuu wamekuwa wakiwanyanyasa Wamiliki wa Maduka ya Dawa kwa maslahi Binafsi na kushauri Wizara ya Afya kuchukua hatua dhidi ya changamoto hizo.

Pia soma = Ofisi ya Mfamasia Mkuu inawanyanyasa sana wamiliki wa Maduka ya Dawa Nchini
 
Akija mwingine naye atarudisha au kugeuza anavyojua yeye, bamba to bamba yaani ilimradi siku zisogee
 
Hii imenikumbusha pia, kuna pharmacy moja mjini Chalinze mkoani pwani wamekuwa na tabia ya kuzidishia wagonjwa dozi mpaka kupelekea hatari ya kupoteza maisha kwa wagonjwa hao. Hawa jamaa wameajiri watu kutoka form six bila kuwa na utaalamu wowote wa dawa.
 
Back
Top Bottom