NHIF wanataka kutuua na dawa za bei chee

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
1,094
1,691
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Tanzania hivi karibuni umefanya marekebisho katika kifurushi chake kinachohusisha pia dawa, yakiwemo madawa ya antibiotic, ambapo imepunguza sana bei. Anaye command soko la dawa Tanzania ni NHIF. Na sasa hii ni RASMI kwamba soko la dawa litatawaliwa na makampuni ya dawa ya India, na hakika wameweza kutuletea dawa tunazozitaka. Ikumbukwe huko India kwa muda mrefu madaktari wao wanagoma kutoa dawa ze bei chee.

Kutegemea dawa za bei chee kutoka India, ambako kuna malalamiko mengi juu ya utengenezaji duni, kunakuja kuleta usugu wa antibiotics. Hebu fikiria NHIF wanataka walipe Antibiotic ya Ceftriaxone ya gramu moja kwa Tsh 1,300/=, wakati ukitaka Ceftriaxone ambayo inaweza kuwa bora, kwa bei ndogo, yamkini utapata ya Egypt, ambayo bei yake ya jumla haitopungua 9,000/=. Egypt ni kati ya nchi ambazo zina sheria kali za kuzalisha antibiotics. Wanataka kutuua hawa wandugu. Lakini nani alisema unapofanya costing uchukue the lowest?

Fikiria unanunua gari. Wakati unachagua gari ulikuwa ukitazama bei ndogo pekee bila kuzingatia historia ya gari husika, usalama, au jinsi linavyoaminika, unaweza kujikuta gari uliyonunua unatumia muda mwingi kwenye garage, au mbaya zaidi, inaweza kuharibika kipindi unaihitaji sana. Mfano huu unaweza kutumika kwa Tanzania ya sasa ya kutaka kupata dawa za bei chee, hasa antibiotics, ili kupunguza gharama za huduma ya afya.

Kwa kununua dawa kwa bei chee hasa antibiotics kutoka vyanzo vya uzalishaji visivyokuwa makini, kama baadhi ya wauzaji nchini India, Tanzania inachagua gari la bei ndogo bila kujali vitu vingine. Chaguo hili linaweza kuokoa pesa sasa, lakini linakuja na gharama zilizofichika ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa zaidi siku za usoni:

1. Ongezeko la Usugu wa Antibiotics: Kama vile gari la bei ndogo linavyoweza kushindwa kuwaka, antibiotics za bei chee zinaweza kushindwa kupambana na maambukizi. Bacteria wanaweza kuwa sugu kwa dawa hizi, ikimaanisha maambukizi ya kawaida ya bacteria yanaweza sababisha kifo kwa sababu antibiotics hazifanyi kazi.

2. Ubora wa Huduma ya Afya Hatarini: Kwa kuruhusu dawa duni kuingia sokoni, tunahatarisha afya na imani kwa mfumo wetu wa huduma ya afya. Ni kama kuwa na barabara zilizojaa na magari mabovu; hatimaye, usalama wa kila mtu unahatarishwa.

3. Gharama za Muda Mrefu: Kama vile gari la bei ndogo linavyokuwa ghali kutokana na matengenezo ya mara kwa mara, antibiotics duni zinaweza kusababisha magonjwa ya muda mrefu, matatizo makubwa zaidi ya afya, na gharama kubwa zaidi za huduma ya afya baadaye kwa sababu ya matibabu yasiyo na ufanisi na kuenea kwa bacteria sugu.

Kwa kifupi, ingawa ni muhimu kufanya huduma ya afya kuwa nafuu, ni muhimu pia kuhakikisha kwamba dawa tunazotumia ni salama, za ufanisi, na za ubora wa juu. Kuokoa pesa leo haipaswi kuja kutugharimu kesho. Kama ilivyo kwa magari, wakati mwingine bei chee huwa ghali zaidi baadaye.

Jana Mtoto wa rafiki yangu alienda hospital ya Private hapa Mwanza alipimwa Damu na choo lakini Mkojo walikataa na fun enough alikutwa na Malaria na minyoo lakini wakasema akanunue dawa maana dawa zilizopo hazilipiwi na NHIF Huyu Ummy Mwalimu anafanya nini mpaka leo ofisini na Mama Samia ameamumua kunymazia ? Hajui tunaingia kwenye uchaguzi atawaambia nini wananchi ambao mbali na haya wengi pia wameathirika na kufutwa kwa kifurushi cha toto Card kwa watoto ?
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Tanzania hivi karibuni umefanya marekebisho katika kifurushi chake kinachohusisha pia dawa, yakiwemo madawa ya antibiotic, ambapo imepunguza sana bei. Anaye command soko la dawa Tanzania ni NHIF. Na sasa hii ni RASMI kwamba soko la dawa litatawaliwa na makampuni ya dawa ya India, na hakika wameweza kutuletea dawa tunazozitaka. Ikumbukwe huko India kwa muda mrefu madaktari wao wanagoma kutoa dawa ze bei chee.

Kutegemea dawa za bei chee kutoka India, ambako kuna malalamiko mengi juu ya utengenezaji duni, kunakuja kuleta usugu wa antibiotics. Hebu fikiria NHIF wanataka walipe Antibiotic ya Ceftriaxone ya gramu moja kwa Tsh 1,300/=, wakati ukitaka Ceftriaxone ambayo inaweza kuwa bora, kwa bei ndogo, yamkini utapata ya Egypt, ambayo bei yake ya jumla haitopungua 9,000/=. Egypt ni kati ya nchi ambazo zina sheria kali za kuzalisha antibiotics. Wanataka kutuua hawa wandugu. Lakini nani alisema unapofanya costing uchukue the lowest?

Fikiria unanunua gari. Wakati unachagua gari ulikuwa ukitazama bei ndogo pekee bila kuzingatia historia ya gari husika, usalama, au jinsi linavyoaminika, unaweza kujikuta gari uliyonunua unatumia muda mwingi kwenye garage, au mbaya zaidi, inaweza kuharibika kipindi unaihitaji sana. Mfano huu unaweza kutumika kwa Tanzania ya sasa ya kutaka kupata dawa za bei chee, hasa antibiotics, ili kupunguza gharama za huduma ya afya.

Kwa kununua dawa kwa bei chee hasa antibiotics kutoka vyanzo vya uzalishaji visivyokuwa makini, kama baadhi ya wauzaji nchini India, Tanzania inachagua gari la bei ndogo bila kujali vitu vingine. Chaguo hili linaweza kuokoa pesa sasa, lakini linakuja na gharama zilizofichika ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa zaidi siku za usoni:

1. Ongezeko la Usugu wa Antibiotics: Kama vile gari la bei ndogo linavyoweza kushindwa kuwaka, antibiotics za bei chee zinaweza kushindwa kupambana na maambukizi. Bacteria wanaweza kuwa sugu kwa dawa hizi, ikimaanisha maambukizi ya kawaida ya bacteria yanaweza sababisha kifo kwa sababu antibiotics hazifanyi kazi.

2. Ubora wa Huduma ya Afya Hatarini: Kwa kuruhusu dawa duni kuingia sokoni, tunahatarisha afya na imani kwa mfumo wetu wa huduma ya afya. Ni kama kuwa na barabara zilizojaa na magari mabovu; hatimaye, usalama wa kila mtu unahatarishwa.

3. Gharama za Muda Mrefu: Kama vile gari la bei ndogo linavyokuwa ghali kutokana na matengenezo ya mara kwa mara, antibiotics duni zinaweza kusababisha magonjwa ya muda mrefu, matatizo makubwa zaidi ya afya, na gharama kubwa zaidi za huduma ya afya baadaye kwa sababu ya matibabu yasiyo na ufanisi na kuenea kwa bacteria sugu.

Kwa kifupi, ingawa ni muhimu kufanya huduma ya afya kuwa nafuu, ni muhimu pia kuhakikisha kwamba dawa tunazotumia ni salama, za ufanisi, na za ubora wa juu. Kuokoa pesa leo haipaswi kuja kutugharimu kesho. Kama ilivyo kwa magari, wakati mwingine bei chee huwa ghali zaidi baadaye.

ONGEZEKO LA USUGU WA VIMELEA badala ya dawa kuwa sugu( ongezeko la usugu wa Antibiotics).
 
Wao na majitu ya ccm wanapewa dawa zenye ubora na kwenda kutibiwa india ila sisi tusio wanaccm ndo tunaletewa madawa kanjanja.
 
Wanachama wa NHIF mmekwisha...tafuteni hela otherwise mkiugua Matanga.
Hiyo ndio CCM a.k.a chama dume..
 
Ukisikia shukrani zinazotolewa na watoto wa viongozi baada ya wazazi wao kufa utasikia wazazi wao walikuwa India, Germany, Uingereza nk kwa ajili ya matibabu ikiwa ni kwa gharama za serikali na 'huruma' ya Samia.
Tanzania huwa wanarudi kusubiri mauti tu na hapo mgonjwa ana kila facility ya hali ya juu ikiwemo na madaktari wazuri wakati anasubiri kufa pale Mzena.

Ikiwa wao wenyewe na ndugu zao wanaenda kutibiwa nje, unadhani watajali walala hoi wakipewa dawa generic zisizotibu?

Kikubwa ni kutafuta pesa uweze kujitibu mwenyewe, ukitegemea kina Samia utakufa huku unajiona. Samia anapeleka India viongozi na wazazi wao tu. Wewe na wazazi wako utajijua mwenyewe.

Sisi tulioajiriwa tuendelee kuchangia NHIF ili wao wachote hela kwenda kutibiana ulaya.
 
Hapo dawa za Egypt nimekuelewa, kuna kipindi mwanangu aliumwa, hangaika sana, baadae nikaenda private moja hivi, nikapewa anti biotic ya Misri....ilikuwa broad spectrum.... Alhamdulillah mtoto alikaa Sawa.
 
Ukisikia shukrani zinazotolewa na watoto wa viongozi baada ya wazazi wao kufa utasikia wazazi wao walikuwa India, Germany, Uingereza nk kwa ajili ya matibabu ikiwa ni kwa gharama za serikali na 'huruma' ya Samia.
Tanzania huwa wanarudi kusubiri mauti tu na hapo mgonjwa ana kila facility ya hali ya juu ikiwemo na madaktari wazuri wakati anasubiri kufa pale Mzena.

Ikiwa wao wenyewe na ndugu zao wanaenda kutibiwa nje, unadhani watajali walala hoi wakipewa dawa generic zisizotibu?

Kikubwa ni kutafuta pesa uweze kujitibu mwenyewe, ukitegemea kina Samia utakufa huku unajiona. Samia anapeleka India viongozi na wazazi wao tu. Wewe na wazazi wako utajijua mwenyewe.

Sisi tulioajiriwa tuendelee kuchangia NHIF ili wao wachote hela kwenda kutibiana ulaya.
Watanzania tulivyo mazuzu tumewaachia huu mjadala wamiliki wa vituo binafsi, tumenyamaza Kama vile haituhusu wakati ni afya zetu zinachezewa.
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Tanzania hivi karibuni umefanya marekebisho katika kifurushi chake kinachohusisha pia dawa, yakiwemo madawa ya antibiotic, ambapo imepunguza sana bei. Anaye command soko la dawa Tanzania ni NHIF. Na sasa hii ni RASMI kwamba soko la dawa litatawaliwa na makampuni ya dawa ya India, na hakika wameweza kutuletea dawa tunazozitaka. Ikumbukwe huko India kwa muda mrefu madaktari wao wanagoma kutoa dawa ze bei chee.

Kutegemea dawa za bei chee kutoka India, ambako kuna malalamiko mengi juu ya utengenezaji duni, kunakuja kuleta usugu wa antibiotics. Hebu fikiria NHIF wanataka walipe Antibiotic ya Ceftriaxone ya gramu moja kwa Tsh 1,300/=, wakati ukitaka Ceftriaxone ambayo inaweza kuwa bora, kwa bei ndogo, yamkini utapata ya Egypt, ambayo bei yake ya jumla haitopungua 9,000/=. Egypt ni kati ya nchi ambazo zina sheria kali za kuzalisha antibiotics. Wanataka kutuua hawa wandugu. Lakini nani alisema unapofanya costing uchukue the lowest?

Fikiria unanunua gari. Wakati unachagua gari ulikuwa ukitazama bei ndogo pekee bila kuzingatia historia ya gari husika, usalama, au jinsi linavyoaminika, unaweza kujikuta gari uliyonunua unatumia muda mwingi kwenye garage, au mbaya zaidi, inaweza kuharibika kipindi unaihitaji sana. Mfano huu unaweza kutumika kwa Tanzania ya sasa ya kutaka kupata dawa za bei chee, hasa antibiotics, ili kupunguza gharama za huduma ya afya.

Kwa kununua dawa kwa bei chee hasa antibiotics kutoka vyanzo vya uzalishaji visivyokuwa makini, kama baadhi ya wauzaji nchini India, Tanzania inachagua gari la bei ndogo bila kujali vitu vingine. Chaguo hili linaweza kuokoa pesa sasa, lakini linakuja na gharama zilizofichika ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa zaidi siku za usoni:

1. Ongezeko la Usugu wa Antibiotics: Kama vile gari la bei ndogo linavyoweza kushindwa kuwaka, antibiotics za bei chee zinaweza kushindwa kupambana na maambukizi. Bacteria wanaweza kuwa sugu kwa dawa hizi, ikimaanisha maambukizi ya kawaida ya bacteria yanaweza sababisha kifo kwa sababu antibiotics hazifanyi kazi.

2. Ubora wa Huduma ya Afya Hatarini: Kwa kuruhusu dawa duni kuingia sokoni, tunahatarisha afya na imani kwa mfumo wetu wa huduma ya afya. Ni kama kuwa na barabara zilizojaa na magari mabovu; hatimaye, usalama wa kila mtu unahatarishwa.

3. Gharama za Muda Mrefu: Kama vile gari la bei ndogo linavyokuwa ghali kutokana na matengenezo ya mara kwa mara, antibiotics duni zinaweza kusababisha magonjwa ya muda mrefu, matatizo makubwa zaidi ya afya, na gharama kubwa zaidi za huduma ya afya baadaye kwa sababu ya matibabu yasiyo na ufanisi na kuenea kwa bacteria sugu.

Kwa kifupi, ingawa ni muhimu kufanya huduma ya afya kuwa nafuu, ni muhimu pia kuhakikisha kwamba dawa tunazotumia ni salama, za ufanisi, na za ubora wa juu. Kuokoa pesa leo haipaswi kuja kutugharimu kesho. Kama ilivyo kwa magari, wakati mwingine bei chee huwa ghali zaidi baadaye.

Duuuhhh.

Kumbe hiyo ceftriaxone 1g Injection wameishusha hivyo...(yaani kutoka 2500 hadi 1300).

Wenye nchi tuendelee kudharaulika kwa sababu tushakubali kudharaulika
 
Jana Mtoto wa rafiki yangu alienda hospital ya Private hapa Mwanza alipimwa Damu na choo lakini Mkojo walikataa na fun enough alikutwa na Malaria na minyoo lakini wakasema akanunue dawa maana dawa zilizopo hazilipiwi na NHIF Huyu Ummy Mwalimu anafanya nini mpaka leo ofisini na Mama Samia ameamumua kunymazia ? Hajui tunaingia kwenye uchaguzi atawaambia nini wananchi ambao wengi wameathirika na kufutwa kwa kifurushi cha toto Card kwa watoto ?
Kwenye Maandamani ya MWanza mww yenye mtoo ali andamana? kumbuka yalikuwa ya amani.

Sikiliza hizi kulalamika hazisaidii kitu, Watawala wanajua fika wanatawala aina gani ya Raia, watawala sio wajinga.
 
Watanzania tulivyo mazuzu tumewaachia huu mjadala wamiliki wa vituo binafsi, tumenyamaza Kama vile haituhusu wakati ni afya zetu zinachezewa.
With due respect nchi ya Tanzania ina watu wajinga wa kutosha.
Kitu wasichofahamu hao wanachama wa NHIF ambao wanakatwa hizo hela ndio ViCTIMS wala sio wanasiasa wao uchwara na wapigaji na pia wala sio wamiliki wa hizo private hospitals maana wao wana hela hivyo wana options achilia mbali hayo makundi mawili asilimia kubwa wana bima binafsi.
Watu wanakopeshana hela za wanachama kununua Ma VX?
Halafu eti wanataka"BIMA KWA WOTE".....nchi ya vichaa hahahaha
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Tanzania hivi karibuni umefanya marekebisho katika kifurushi chake kinachohusisha pia dawa, yakiwemo madawa ya antibiotic, ambapo imepunguza sana bei. Anaye command soko la dawa Tanzania ni NHIF. Na sasa hii ni RASMI kwamba soko la dawa litatawaliwa na makampuni ya dawa ya India, na hakika wameweza kutuletea dawa tunazozitaka. Ikumbukwe huko India kwa muda mrefu madaktari wao wanagoma kutoa dawa ze bei chee.

Kutegemea dawa za bei chee kutoka India, ambako kuna malalamiko mengi juu ya utengenezaji duni, kunakuja kuleta usugu wa antibiotics. Hebu fikiria NHIF wanataka walipe Antibiotic ya Ceftriaxone ya gramu moja kwa Tsh 1,300/=, wakati ukitaka Ceftriaxone ambayo inaweza kuwa bora, kwa bei ndogo, yamkini utapata ya Egypt, ambayo bei yake ya jumla haitopungua 9,000/=. Egypt ni kati ya nchi ambazo zina sheria kali za kuzalisha antibiotics. Wanataka kutuua hawa wandugu. Lakini nani alisema unapofanya costing uchukue the lowest?

Fikiria unanunua gari. Wakati unachagua gari ulikuwa ukitazama bei ndogo pekee bila kuzingatia historia ya gari husika, usalama, au jinsi linavyoaminika, unaweza kujikuta gari uliyonunua unatumia muda mwingi kwenye garage, au mbaya zaidi, inaweza kuharibika kipindi unaihitaji sana. Mfano huu unaweza kutumika kwa Tanzania ya sasa ya kutaka kupata dawa za bei chee, hasa antibiotics, ili kupunguza gharama za huduma ya afya.

Kwa kununua dawa kwa bei chee hasa antibiotics kutoka vyanzo vya uzalishaji visivyokuwa makini, kama baadhi ya wauzaji nchini India, Tanzania inachagua gari la bei ndogo bila kujali vitu vingine. Chaguo hili linaweza kuokoa pesa sasa, lakini linakuja na gharama zilizofichika ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa zaidi siku za usoni:

1. Ongezeko la Usugu wa Antibiotics: Kama vile gari la bei ndogo linavyoweza kushindwa kuwaka, antibiotics za bei chee zinaweza kushindwa kupambana na maambukizi. Bacteria wanaweza kuwa sugu kwa dawa hizi, ikimaanisha maambukizi ya kawaida ya bacteria yanaweza sababisha kifo kwa sababu antibiotics hazifanyi kazi.

2. Ubora wa Huduma ya Afya Hatarini: Kwa kuruhusu dawa duni kuingia sokoni, tunahatarisha afya na imani kwa mfumo wetu wa huduma ya afya. Ni kama kuwa na barabara zilizojaa na magari mabovu; hatimaye, usalama wa kila mtu unahatarishwa.

3. Gharama za Muda Mrefu: Kama vile gari la bei ndogo linavyokuwa ghali kutokana na matengenezo ya mara kwa mara, antibiotics duni zinaweza kusababisha magonjwa ya muda mrefu, matatizo makubwa zaidi ya afya, na gharama kubwa zaidi za huduma ya afya baadaye kwa sababu ya matibabu yasiyo na ufanisi na kuenea kwa bacteria sugu.

Kwa kifupi, ingawa ni muhimu kufanya huduma ya afya kuwa nafuu, ni muhimu pia kuhakikisha kwamba dawa tunazotumia ni salama, za ufanisi, na za ubora wa juu. Kuokoa pesa leo haipaswi kuja kutugharimu kesho. Kama ilivyo kwa magari, wakati mwingine bei chee huwa ghali zaidi baadaye.

Subiri mtaona matokeo.😂😂
 
Unachosema kina matter, ila angalia upande wa pili pia,
Tukisema tutoe dawa quality ya Egypt, eg ceftriaxone tuuze 15k, watu wetu wataweza mudu ? Kisha panaldo tuuze za 3000, tutaweza ?
Mana kama tukitaka dawa hizo ujue bei ya bima itakuja kuwa mtu mmoja 1M, ukienda hospital ukapewa dawa mbili jua bill ni laki na, je tutaweza ?

Usiseme tu kina Ummy wanaleta cheap drugs,
Wote tunataka kutibia Aga khan ila bill tunaweza ? Mana dispensary hizo ceftriaxone zinachomwa kwa 5k, ila bado 80% ya watu hawamudu kulipa full dose at once, sasa zikija hizo za 15k?

Anyway, tuendelee kwa sasa kutumia dawa za India na China, huku tukijenga uchumi imara ili tuweze tumia za Egypt
 
Watanzania tulivyo mazuzu tumewaachia huu mjadala wamiliki wa vituo binafsi, tumenyamaza Kama vile haituhusu wakati ni afya zetu zinachezewa.
Watanzania tuna upumbavu mmoja wa kila mtu kujiwazia mwenyewe kibinafsi. Huwa hatuna upeo wa kujua kuwa jambo linalomuathiri mmoja likiachiwa litakuja kuathiri wote.

Ikiwa mimi nina uwezo wa kununua dawa original ambayo sio generic basi siwazi kuwa haishii kwenye dawa tu, ni huduma nzima ya afya; ambapo kesho nikikosa uwezo wa kulipia huduma bora ndio nakuja kupiga kelele.

Hazina kubwa ya Watawala wa Tanzania ni upumbavu wetu sisi wananchi. Tunachukulia poa kila kitu.
 
Back
Top Bottom