Madaktari waipiga changa la macho serikali

Ukiangalia kwa mtizamo dhaifu,unaweza kudhani uamuzi wa serikali kupitia tamko la bwana Masaju litamaliza tatizo na hakutakuwepo mgomo.Lakini nataka tutafakari yafuatayo:
1.Tumekuwa tukisema kazi ya udaktari ni ya wito,na huwezi kutofautisha wito na utashi wa mtu kwa maneno mengine niseme nyenzo inayosukuma wito ndani ya mtu ni utashi.Je kwa serikali kwenda mahakamani itawafanya madaktari wafanye kazi kwa wito?
2.Kugoma ni Kutowepo kwenye eneo la kazi au kutofanya kazi husika,lakini mtu akiwepo kazini na kufanya kazi lakini siyo kwa weredi huwezi kusema kagoma lakini madhara yatakuwepo kwa wanaohudumiwa.Mfano mwenye mamlaka ya kusema mtu huyu anaumwa au haumwi ni daktari(MD) na si mtu mwingine.Itakuwaje daktari akikwambia huumwi au akakupa dawa dhaifu ukilinganisha na ugonjwa unaoumwa?Ni rahisi kusema atachukuliwa hatua,ni sawa lakini kama ugonjwa huo ni kipindupindu,hatua itachukuliwa wakati mgonjwa ameishakufa.
Hivyo naiomba serikali asifanye siasa ktk suala hili,Maisha ya watz yanawasubiri ninyi kufanya uamzi sahihi.
 
Mataktari wataenda kazini wagonjwa wakifika watawashiwa tv wakichoka wataondoka sijui ndo serikali itakuwa imefanya nini
 
Kumbuka madaktari wanatumia maisha yako au ya ndg yako kuhakikisha wao wanaishi maisha mazuri. Madai yao yanaweza kuwa genuine lakini njia ya kuuwa ndg zetu ili wapate wanachohitaji hapo lipo tatizo. Je walimu nao wafanyeje? Je kwa njia hii nchi itatawalika kweli? Kumbuka viongozi wa serikali hawaathiriki na huu mgomo kwani wanazo pesa za kutibiwa popote duniani. Anaye unga mkono haya madai hajawaatendea haki the so called watanzania wa kawaida
 
Tuache kusapoti u jinga na u huni unaofanywa na hawa jamaa....Hiyo kamati imesajiliwa wapi?? Kwahili sijawahi kuunga na wala sitoliunga mkono....Ninyi shabikieni lakini athari zitakazowapata mama ana baba zenu wakiwamo bibi na babu zenu ambao hamuishi nao ndo mtajua.....hata kama tunadhani tunaikomoa CCM na serekali..nadhani strategy hii ni mbovu na haifai na wala haitatufikisha popote....Nakaribisha matusi na kejeli kama ilivyo kawaida ya baadhi ya wana JF ambao hatutaki kusikia second opinion....

wewe unachoshabikia ni mawaziri wanaofumaniwa na wake za watu, kuliko madokta wanaookoa vifo? hospitalini kuna gest ya kulala na malaya? angalia sana
 
Mkuu mbona unakimbilia kujihami hivyo?
Hivi unafikiri wagonjwa sasa hivi mahospitalini hawapati madhara hata kama hakuna mgomo? Ulipata soma au kusikia madai ya madaktari? Utaona wanachodai siyo maslahi yao tu.
Tutake tusitake hii serikali yetu ni ya kisanii sana. Hivi kama kungekuwa na mgomo.
Tatizo lipo kwa serikali yenye mawazo yale yale ya kutatua matatizo. Hivi mahakama ikizuia, inaweza kuwalazimisha madoctor kufanya upasuaji?
Serikali na mahakama zake vichwa maji tu.
kWELI HUU WOTE NI UHUNI TU.
 
Kumbuka madaktari wanatumia maisha yako au ya ndg yako kuhakikisha wao wanaishi maisha mazuri. Madai yao yanaweza kuwa genuine lakini njia ya kuuwa ndg zetu ili wapate wanachohitaji hapo lipo tatizo. Je walimu nao wafanyeje? Je kwa njia hii nchi itatawalika kweli? Kumbuka viongozi wa serikali hawaathiriki na huu mgomo kwani wanazo pesa za kutibiwa popote duniani. Anaye unga mkono haya madai hajawaatendea haki the so called watanzania wa kawaida

wabongo mnataka maisha bora bila damu kumwagika, wale waliokufa juzi ulienda msibani? acheni maneno yenu, na kwa nini vifo vya wagonjwa lawama iende kwa dalktar pekee, wenye matatizo ni wananchi nagundua sasa!
 
wewe unachoshabikia ni mawaziri wanaofumaniwa na wake za watu, kuliko madokta wanaookoa vifo? hospitalini kuna gest ya kulala na malaya? angalia sana

JF imeingiliwa....ati huyu naye anajiita GT....okay probably that's the end of your thinking capacity.....come on....
 
napenda nishauri tembelea hospitalini wakati hakuna mgomo uone, tena uwe na mgonjwa, hata kama una bima

hospitali ni kwa hovyo binafsi nawaunga mkono ili wakipata mahitaji yao! tuanze nao.
mnaonaje
 
mkirua weka hoja! acha inferiorism, kwa nini wagome na kwa nini wasidai wakiona viongozi wao hawajui hata shida za watu. bajeti ikipangwa inaishia dsm na dodoma. huo wewe ndio mwisho wako wa kufikiri? naona jf inahitaji mtaalamu wa IQ atakusaidia kujua uwezo wako kufikiri, ama net ina IQ test fanya ujue uwezo wako kama ni wa kuku au panzi.
 
Sasa kama serikali inashindwa hata kununua exray za mashine za hospitali za rufaa,tutaisaidiaje?Kama mamamjamzito anatakiwa kutibiwa bure lakini anaambiwa aende na mipira ya mkoja ya kutandika wakati anajifungua.gloves pair sita na pamba,sasa dakatari akigoma hana gloves utamlaumu?Viongozi wetu wawe wa kweli kuliko kutoa propoganda zisizojenga huu ni wakati wa utandawazi hata mtoto mdogo anajua haki zake za msingi. Watuambie mishahara ya waheshimiwa sana imepanda kwa asilimia ngapi? Mengine yafuate...........
 
Mshahara wa daktari ukiongezwa mpaka mil 3.5 kwa mwenye bachelor anayeanza kazi nawaapia jamani tutegemee reaction kubwa sana kutoka kwenye kada nyingine za wafanyakazi wa umma!Ni kweli kuwa madaktari ni wa muhimu sana lakini kwa uchumi wa Tz huo mshahara hautekelezeki,pia kila mfanyakazi wa umma ana umuhimu kwa jamii husika,hili suala la kujiona bora kuliko wengine kwakweli mimi siliafiki kabisa!
Madaktari sawa tunakubali kuna changamoto katika sekta yenu na zinahitaji kutatuliwa lakini kuingia kwenye mgomo binafsi siwaungi mkono hata kidogo.
Mkuu umewahi kulinganisha mishahara ya wafanyakazi wa BENKI KUU,TRA,EWURA,Tanesco na ile ya waalimu,wafanya kazi wa halmashauri n.k? mbona hakuna migomo wala maandamano kwa wale walioko kwenye taasisi zinazolipa kidogo? Nini sababu ya idara nyingine za serikali kulipa mishahara kidogo na nyingine kulipwa mishahara mikubwa wakati serikali ni hiyo hiyo? mimi naweza kusema mambo kama haya ndo yanasababisha na wataalam wengine muhimu wanaolipwa kidogo kugoma au kudai nyongeza SABABU wanaona wao wanadharauliwa.Huwezi kuniambia kwamba kila afisa kwenye taasisi za serikali zinazolipa vizuri ni msomi mkubwa hakuna mfano wake kwenye taasisi za serikali zinazolipa mishahara midogo.
TUKUMBUKE WALICHOKISEMA MADAKTARI NI KWAMBA SERIKALI IMESHINDWA KUTIMIZA MAKUBALIANO WALIYOKUBALIANA.Kwa nini serikali ilikubaliana nao hayo wanayoshindwa kuyatekeleza kama walijua wakiyatekeleza yataleta shida?
 
Mimi siyo daktari ila mke wangu ni daktari, MD! Hali iliyoko kwenye hospitali zetu ni afadhali mgomo kuliko hiyo hali. Nasema hivyo kwa sababu madaktari wapo, lakini vitendea kazi hakuna. Unategemea kila mgonjwa atatibiwaje kama hata sindano tu, visu vya kufanyia operation, pamba za kusafishia, mipira midogo ya kusaidia mtu kupumua wakati anapokuwa hajiwezi pamoja na mazingira magumu ya kufanyia kazi.
Pamoja na hilo la kudai nyongeza ya mishahara, lakini kuna madai ambayo ni msingi na ni ya faida kwa mtanzania si kwa madaktari tu. Bazi serikali kupitia kwa viongozi wahusika waseme ukweli waache siasa kwenye inshu sensitive kama za afya nini wanakifanya kuboresha hospitali hata kwa kuweka gharama fulani kwa ajili kutibu watu. Wakati nchi zingine zikiamini kila mtu anayo haki ya kuishi, kifo ni bahati mbaya tena kwa ajali au uzee, sisi watu tena nguvu kazi inapoteza maisha kizembe kabisa kwa daktari kukosa vitendea kazi kwa ajili ya kumsaidia mgonjwa.
Fikiria, mgonjwa anapoteza maisha mbele yako kwa kukosa kisindano! pengine huyu daktari kawasaidia watu zaidi ya kumi (mfano mke wangu) kwa kuwanunulia sindano sasa kaishiwa pesa, anamuona mgonjwa yule anahitaji kitu kidogo tu lakini hana jinsi inabidi akubali mtu yule apoteze maisha. Sasa, hapo unafikiria akili ya huyo daktari itakuwaje? kumbuka daktari naye ni binadamu.
Its too sad, wakati mtu mwenye kufanya maamuzi ya nini kifanyika kusaidia wananchi anapiga siasa pamoja na vitisho huku wengine wakiendekeza uzinzi. Ningekupa mifano ya jinsi wagonjwa wanavyopoteza maisha kizembe si kwakuwa daktari hawezi kumtibu lakini kwa kukosa vifaa vya kumsaidia yule binadamu mwenzako.

Nilishasema huko nyuma adui wa madaktari ni UTUMISHI (MAGWINI) hii ni story ndefu na hipo kwenye viapo vyao. Watangoka Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Waganga Wakuu wa Wizara ya Afya lakini hakuna kitu kitakachofanyika katika kuboresha maslahi ya Madaktari mpaka pale Wizara ya Afya itakapokuwa na nguvu kisera ya kupanga na kuamua mambo yake kama ilivyo Ofisi ya Bunge, TRA n. k.. Narudia tena Madaktari wabaya wenu ni UTUMISHI. Source, ile barua kutoka kwa Yambesi akimwandikia Katibu Mkuu Wizara ya Afya kuongeza posho kutoka 10,000 hadi 20,000 na 25,000. Hivyo basi, Wizara ya Afya ni Wizara isiyokuwa na meno kwenye masuala ya maslahi ya madaktari. Madaktari geuzeni vita yenu kuelekea UTUMISHI.
 
Serikali dhaifu ni tatizo kubwa sana.
Inabidi maamuzi magumu yafanyike huyu jamaa "DHAIFU" aondoke awapishe wenye nguvu ya maamuzi na matendo waongoze. And this is the only wayforward
 
tuache kusapoti u jinga na u huni unaofanywa na hawa jamaa....hiyo kamati imesajiliwa wapi?? Kwahili sijawahi kuunga na wala sitoliunga mkono....ninyi shabikieni lakini athari zitakazowapata mama ana baba zenu wakiwamo bibi na babu zenu ambao hamuishi nao ndo mtajua.....hata kama tunadhani tunaikomoa ccm na serekali..nadhani strategy hii ni mbovu na haifai na wala haitatufikisha popote....nakaribisha matusi na kejeli kama ilivyo kawaida ya baadhi ya wana jf ambao hatutaki kusikia second opinion....

to be honest sasa hivi ndo mama zetu na wazee wetu ndo wanateseka kwa kuwa hakuna dawa wala mazingira bora kuwawezesha mmadactari kutoa huduma bora kwao..mfano cku mbili tumeambiwa dawa ya kulazia wagonjwa ili upasuaji ufanyyike ktk hospitali ya meta mbeya ilikuwa imekwisha na watu wakabaki kutseka wodin wakat bilion tatu zinatumikaa kwa safari za nje za mtu mmoja..tatizo lako hujapita hospital ukaona hali halis unawackiliza wanacasa tu bungenii....mtu mzima anapofanya kitu kabla hujampinga fanya utafit...sawa kijana.
 
Okay GT.....Hapo kwenye RED sikujua kuwa ndio sababu ya mgomo....Aksante kwa kunielimisha....nilitegemea basi hapo mbeya wawe wakwanza kugoma...
 
Mshahara wa daktari ukiongezwa mpaka mil 3.5 kwa mwenye bachelor anayeanza kazi nawaapia jamani tutegemee reaction kubwa sana kutoka kwenye kada nyingine za wafanyakazi wa umma!Ni kweli kuwa madaktari ni wa muhimu sana lakini kwa uchumi wa Tz huo mshahara hautekelezeki,pia kila mfanyakazi wa umma ana umuhimu kwa jamii husika,hili suala la kujiona bora kuliko wengine kwakweli mimi siliafiki kabisa!
Madaktari sawa tunakubali kuna changamoto katika sekta yenu na zinahitaji kutatuliwa lakini kuingia kwenye mgomo binafsi siwaungi mkono hata kidogo.

Hivi unaweza kukisia idadi ya madaktari Tanzania, hebu nikujuze hapa jiji la Mwanza lenye hospitali moja, health centre 4 na zahanati kama 9 hivi kuna daktari (MD) 1 tu! Wengine unaowaona wamevaa koti ndefu nyeupe ni kada zingine mf. Wafamasia, Radiolojia n.k MD wetu wengi wapo Botswana, Sudani, nk.
 
Nilishasema huko nyuma adui wa madaktari ni UTUMISHI (MAGWINI) hii ni story ndefu na hipo kwenye viapo vyao. Watangoka Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Waganga Wakuu wa Wizara ya Afya lakini hakuna kitu kitakachofanyika katika kuboresha maslahi ya Madaktari mpaka pale Wizara ya Afya itakapokuwa na nguvu kisera ya kupanga na kuamua mambo yake kama ilivyo Ofisi ya Bunge, TRA n. k.. Narudia tena Madaktari wabaya wenu ni UTUMISHI. Source, ile barua kutoka kwa Yambesi akimwandikia Katibu Mkuu Wizara ya Afya kuongeza posho kutoka 10,000 hadi 20,000 na 25,000. Hivyo basi, Wizara ya Afya ni Wizara isiyokuwa na meno kwenye masuala ya maslahi ya madaktari. Madaktari geuzeni vita yenu kuelekea UTUMISHI.

Asante mkuu! Nimependa mapendekezo yako.
 
Back
Top Bottom