Ukiwa na akili kama za madaktari, raha sana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiwa na akili kama za madaktari, raha sana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msendekwa, Jun 26, 2012.

 1. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali kupitia mahakama kuu, imeamuru MAT(chama cha madaktari tanzania) kutangaza kuwa hakuna mgomo.
  Kumbe Madaktari walishaliona hili tangu mgomo wa mwanzo, pale walipoiengua MAT isijihusishe na mgomo kwani kisheria walijua haina mamlaka ya kuitisha mgomo, kwani si trade union, badala yake wakaunda jumuia ya madaktari(ambayo MAT ni sehemu yake) na kuweka uongozi chini ya kamanda Ulimboka.
  Jumuia hiyo haijasajiliwa popote, na inajumuisha madaktari wote nchini kwa ujumla wao.
  Sawa, MAT inaweza kusema hakuna mgomo kwa amri ya mahakama, lkn haitakuwa na maana, kwani si wao walioitisha mgomo.
  Jumuia ya madaktari sidhani km inaburuzika mahakamani, na ndo imeamua kugoma!
  Hivyo amri ya mahakama dhidi ya MAT ni serikali kujipiga changa la macho tu, haitasaidia lolote kumaliza mgomo.
  Muhimu watambue tu kuwa wanadili na watu wenye akili sana, cream of the nation, great thnkers, waliopitia misukosuko mingi sana tangu sekondari, wakisoma PCB kwenye shule zisizo na walimu wa kueleweka, na bado wakafaulu sana na kwenda medical school.
  Huko nako wamepambana na ku absorb stress kibao, hd kuwa na taaluma hii adhimu.
  Serikali haina chaguo jingine, zaidi ya ku give in to doctors' demands!
  Ujanja ujanja mwingne hausaidii.
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hakuna ujanja ujanja hapa katika hili porojo za pinda na tabasamu la kikwete sio suruhisho wapeni chao madr mazungumzo gani yasoisha? mnapindisha pindisha tu taarifa zenu
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,347
  Likes Received: 22,198
  Trophy Points: 280
  Basi Kikwete na wenzake, wakiwaona hawa wanavyoteseka, wanacheka kwelikweli, wanaona raha isiyo na kifani, ndio maana hawajatatua tatizo hili la wagonjwa kurundikana na ukosefu wa vitanda na mawodi.

  [​IMG]
   
 4. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  bonge ya chenga ya mwili hiyo! Hii cream ya taifa wanayoipigisha danadana ikiamua na sasa imeamua kutumia akili na uwezo wao walionao kulishughulikia hili swala for good! sasa serikali iendelee kucheza, mwisho watajikuta wako wametupwa nje!
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hao wamama wako nchi gani wanjameni? Nimepata uchungu hadi kwenye mifupa ninapowaangalia hawa akina mama ambao kuwa kwao hapa ni ku reproduce walipa kodi ambao kodi zao zinatumika kama mitaji ya mafisadi pasipo huruma ya kurejesha angalau kitu kidogo kiwasaidie hawa akina mama ili nao wafurahie matunda ya matumbo yao.
   
 6. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda sana hii picha, coz hizi ndo situation tunazokutana nazo. Hapo wakati wa round mnapishana utafikri tupo kwenye daladala like that.
  Jk yeye hata hawazi kama kuna jambo linaendelea anasubiri muda ufike yeye aende Canada kwenye Canada day.
   
 7. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wasiache kazi kuliko kuwaia wagonjwa? Mm mwenyewe naumwa Typhod na maleria ntaenda orivate nao wakigoma Konyagi ni dawa
  Madai yao sikubaliani nao hata km walisoma PCB hawajaenda JKT wakapate Imani ya uzalendo au BCom wakajua hela yao itapatikana wapi bila ya kuwashurutisha wagonjwa walipe 100,000/ kuandika daftari la 500 na kumuona yeye Dr bado dawa au kulazwa
  Shime rudini kazini au muachie ngazi tutajua mbele kwa mbele hela hakuna 3.5m km start salary wakati Mwl 210,000 tena kijijini tofauti na hapo Muhimbili
  Mwisho msicheze na Mahakama au Serikali
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  serikali ya kishkaji ina matatizo sanaa
   
 9. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,935
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  teh teh tehh
   
 10. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  usicheke mkuu!chukua hatua!
   
 11. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali ndo inayocheza na madaktari kupitia mahakama.
  Anaeua wagonjwa ni serikali, maana ndiyo iliwaahidi afya bora kupitia ilani yake ya uchaguz, madaktari ni waajiriwa tu wa serikali, yenye dhamani ya afya.
  Na kugoma ni last resort kwa Drs, ni haki yao, baada ya mazungumzo ya miezi mi3 yaliyoishia kwa madai yote kutupwa, na serikali kuongeza posho ya postmortem ambayo haikuombwa!
  Ulitarajia wafanye nini zaidi?
  Wakae chini waanze kulia?
  Wavumilie dhuruma na kuendelea na kazi huku wakinung'unika kizazi baada ya kizazi?
  No, imetosha sasa, na uamuzi wao wa sasa ni bora kabisa, wakaze tu.
  Eti hawajapita JKT!
  Je, walioua viwanda hawakupita JKT?
  Waliofilisi parastatals hawakupita JKT?
  Waliotuingiza kwenye IPTL, richmond/dowans, Epa, hawakuwahi kuwa makuruta?
  Wale wenye 300bn uswizi hawakupita JKT?
  Kwa taarifa yako ewe ukwaju, hawa Drs waliopo hapa nyumbani na wamegoma, ni wazalendo mno, wamebaki nchini (wkt wenzao wengne wakitafuta green pastures nje)
  ili kupigania masilahi yao na ubora wa sekta ya afya kwa ujumla, kuiondoa nchi kwenye fedheha ya kutumia pesa nyingi kutibu viongozi India, kuliko ile inayotumika kuendeshea hosp za rufaa nchini.
   
 12. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MUngu wangu imefikia halii Tanganyika??? Moyo wangu umeumia sana kwa kweli kutoka moyoni aisee duh

   
 13. e

  ellyjr8 Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
  Leo ningependa turudijamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza yamada hii, nilijaribu kuainisha madaiyetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu"SIKIVU" ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kamahukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe machoKIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leonilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.
  HALI HALISI HOSPITALINI:
  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke,Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatarikwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO(KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZAUDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..
  Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishaharatu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali,tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
  1. Madai ya madaktari yalianza lini?
  2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
  3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia poshompya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
  4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwakatika bajeti?
  5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

  SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WATRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YAMSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZIKUJIONGEZEA(duringthe same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NAKULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
  Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idarawamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katikahospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu nikushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

  VYOMBO VYA HABARI:
  Katika "episode" mbili za "series" yetu hii ya Mgomo waMadaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi palewatu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!
  Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajuiau wanapuuzia?
  Halafu mnatuitamadaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzaniawanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtuhauwekwi rehani lakini hatukuingiakatika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndiomaana muda wa mazungumzo ulikuwepo nahata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikaliikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basiijipange kuhudumia wananchi.
  Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya paleStar TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali nihaya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kamatungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), nakwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?
  MKAKATI:
  Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
  1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
  2. Wanatumia pesa ya nani?
  3. Last‘episode" walileta wanajeshi,
  KAMA MADAI YAMADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKOSAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??
  KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZIMNAYYOIITA KAZI YA WITO????

  MAKOLIGI (colleague)??
  Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afyazao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakoseakidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali "sikivu", hivyo lawama, maombi, na hisia zotepelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time sikwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKEVIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
  Najua wanasema when you get in a fight you should dig, twograves but I guess you should not fightwith someone who has NOTHING to loose,..We either overestimated the power of Government's responsibility orThey(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stopus.. you cant stop what you cant catch,because the more they will push us the worse this is going to get…
  ..Solidarityforever..
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wakawachukue wale wapiga kwata Kama kawaida yao
   
 15. W

  We know next JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii haswa ni analysis ya Great Thinker! Nimependa hapo unapotuuliza Watanzania, Je tuna mikataba na madaktari kuhusu Afya zetu?? Nimeipenda sana hii. Let call spade a spade. Bravo
   
 16. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hapo Bujibuji naona hizi sura za wagonjwa zimekaa kingono.....Watz wanapenda sana huu mchezo
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,347
  Likes Received: 22,198
  Trophy Points: 280
  Boflo huna huruma hata kidogo, unatamani mbunye zenye uchungu!!!!
   
Loading...