Mkirua unaudhi ile mbaya,nadhani unaongea kishabiki wewe,na sio hao unawasema wanashabikia,wewe ndo unashabikia kishabiki na ushabiki huu ni ule wa Nyinyiemu-CCM.for sure wewe umetumwa na Nape,unaangalia matokeo badala ya kuangalia chanzo cha tatizo.hivi reflect hili suala la madaktari ambalo ni lao wao,naaminisha maslahi yao kama wao,Je ungelikuwa wewe unaefanyiwa hayo ungeliona ni sawa tu?hivi ni kweli serikali haina pesa ya kuwaongezea mishahara na posho zingine wanazoziomba,je matumizi ya anasa ya hizo pesa zinazo fujwa na viongozi mafisadi chini ya CCM zinatoka wapi?wewe uko tayari kulipwa ujira kidogo wakati unafanya kazi kubwa?
Kingine sidhani kama huwa unaenda hospitali zetu sisi walala hoi,madktari wanadai mazingira ya kufanyiia kazi yaboreshwe,kinachomaanishwa hapa wanataka vifaa tiba vya kutosha na vya kisasa,wanataka majengo ya kutosha wanataka vitanda vya kutosha mahospitalini na vitu vingine ambavyo ni essential katika utendaji wao wa kazi.sasa haya yote unaona ni upuuzi au,haya yote unaona tunashabikia sio,hujawahi kuuguliwa au kuugua kiasi kwamba ikabidi ulazwe ndio maana unaropoka.ujinga huu unaofanywa na chama chako hauwezi kuisha bila watu ku-sacrifice.najua tutakufa,na huenda ikawa ni mimi lakini ni vema saratani hii iitwayo CCM iondoke.maana haya yote ni sababu ya udhaifu wa chama cha magamba.wacha tushabikie lakini one day yes ukombozi utapatikana.
chonde chonde madaktari msi-beep tafadhalini pigeni