Ofisi ya waziri mkuu yageuka kuwa mahakama kuu katika sakata la madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi ya waziri mkuu yageuka kuwa mahakama kuu katika sakata la madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by vimon, Mar 9, 2012.

 1. vimon

  vimon Senior Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  [h=6]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, leo (*Alhamisi Machi 8, 2012) *imetoa
  ... uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi
  nzima tangu jana (*Jumatano Machi 7, 2012).

  Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari
  Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia
  Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama
  walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.

  Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja
  na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine,
  kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa
  haraka.


  Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya
  kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha
  Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.

  Akitoa uamuzi huo, Jaji Rweyemamu alisema anazingatia madhara ambayo mgomo
  huo ungeleta kwa jamii kwa vile huduma za tiba ambazo madaktari walitaka
  kugoma kuzitoa ni miongoni mwa huduma muhimu zilizotajwa kwenye Sheria ya
  Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya Mwaka 2004.

  Uamuzi huo, ni kama ifuatavyo:

  Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji
  R.M. Rweyemamu
  , baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari
  Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:

  i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari
  pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi
  2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama
  kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa
  Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na
  kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9,
  Mach 2012.

  ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa
  (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa
  kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo
  huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;

  iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama
  cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za
  Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa
  haraka.
  (mwisho)
  Imetolewa na:

  Ofisi ya Waziri Mkuu,
  S.L.P. 3021
  DAR ES SALAAM.
  Alhamisi Machi 8, 2012
  [/h]Siku hizi kazi za ofisi ya PM zimekuwa za kimahakama au ndio kuzuia PM asiachie madaraka,pinda jiuzulu umeiabisha.
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mahakama inasemaje kuhusu wale mawaziri wawili?
   
 3. S

  Saas JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi siasa hizi yaani mahakama inatoa taarifa halafu chini inaandikiwa kuwa imetolewa na ofisi ya Waziri Mkuu
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  something is wrong...
   
 5. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Hii haikubaliki;Mahakama ni muhimili unaojitegemea kabisa;ningekuwa mm Dr ningeendelea kugoma kudai mafao yangu maana kinachofanyika sasa ni uhuni!

  Mkiwalazimisha ma dr ukienda unaumwa kichwa wanaweza kukuandikia sindano za kuponya kaswende,mahakama haiwezi mlazimisha dr kufanya kazi kama wanavyotaka kufanya serikali bali ni kwa majadiliano tu!
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  njia mojawapo ya kutatua migogoro ni haki ya mfanya kazi kugoma. halafu hao madaktari wataongea na nani? wakati mtu mwenyewe wa kuongea naye wapo kwenye mgogoro nae? na Pm aliwaahidi kutekeleza mambo yao ni 3/3/12 kupeana taarifa ya kilichofikiwa na kile bado lini, ikiwemo mamlaka husika kushughulikia suala la waziri na naibu waziri. yaani gharama zote hizi kwa serikali ni kwa ajili ya wanasiasa, kama ilivyo kuwa ndege ya raisi kwamba anayo haki, ya hayo matumizi hata kama sisi tutakula nyasi.
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Serikali ya wendawazimu
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wana makosa gani eti??????
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
   
 10. n

  nicksemu Senior Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hahahaaaaa siku-notice hii kitu watakuwa wameipika hii msg. Hawako makini kwakweli
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Kama mpaka Rejeo amenotice kuwa something is wrong then there must be a very serious problem there!!
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wanaweweseka hao
   
 13. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,002
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  asante kwa kuliona hilo.
   
 14. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Ikiwa tangazo hili halijaeditiwa basi madaktari wanayo haki ya kuishitaki mahakama pamoja na waziri mkuu kwa kuwahadaaa wananchi pamoja na madaktari. What a shame................. Kwanza haina hana nembo.
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kazi kweli kweli
   
 16. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Matunda ya vikao vya baraza la mawaziri na ni kati ya moja ya mbinu/mikakati yao waliyoiweka ili kuzuia mgomo. Ila naona ni mbinu dhaifu. Inabidi wajipange upya.
   
 17. a

  abdalah Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hii kali.
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Hii kaichapa Pinda mwenyewe........mbona haina reference number
   
 19. C

  Cupid 50mg Member

  #19
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes is true something wrong some where!!
   
 20. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Teh teh teh teh!Rejao for the first time uzalendo umemshinda,kaamua kusimama kwenye mstari juu ya tangazo ili
   
Loading...