Najaribu tu mkuu kuforecast situation itakavyokuwa..haswa kwa wanyonge wa nchi hiiMkuu mbona unakimbilia kujihami hivyo?
Hivi unafikiri wagonjwa sasa hivi mahospitalini hawapati madhara hata kama hakuna mgomo? Ulipata soma au kusikia madai ya madaktari? Utaona wanachodai siyo maslahi yao tu.
Tutake tusitake hii serikali yetu ni ya kisanii sana. Hivi kama kungekuwa na mgomo.
Tatizo lipo kwa serikali yenye mawazo yale yale ya kutatua matatizo. Hivi mahakama ikizuia, inaweza kuwalazimisha madoctor kufanya upasuaji?
Serikali na mahakama zake vichwa maji tu.
npo maeneo ya muhimbili,ngoja nicheki hali halisi ikoje!
Kama unaweza kuona ushabiki unaofanywa sasa kushabikia mgomo wa madaktari, mbona hukuuona ushabiki wa unaowatetea wakati wa uchaguzi? waache walipe gharama ya maamuzi yao ya kishabiki!Watumie vizuri nafasi yao ya kupiga kura ili wachague serekali makini itakayotumia vizuri rasilimali tulizojaliwa ili wafanyakaze wote walipwe vizuri..
Ambacho sikubaliani nacho hapa ni kushabikia matendo yatakayopelekea madhara kwa wasioukuwa na hatia kwa sababu tu tunataka kuiadhibu serekali ambayo to my opinion haiathiriki katika hili...
Hivi wananchi hatuwezi kuishitaki Serikali Kama vifo vitatokea?Kwa mfano sisi wananchi tumeshatimiza jukumu letu kwa kulipa kodi ya Serikali na kila siku tunaendelea kulipa kodi ya moja kwa moja kwa ununuzi Wa mahitaji yetu ya kila siku(unga/sukari/mafuta/sababuni/mchele/n.k.),sasa vipi kwa upande wa pili wa Serikali kuwajibika kwetu sisi wananchi kwa kutupatia Huduma bora na salama?
Kama unaweza kuona ushabiki unaofanywa sasa kushabikia mgomo wa madaktari, mbona hukuuona ushabiki wa unaowatetea wakati wa uchaguzi? waache walipe gharama ya maamuzi yao ya kishabiki!
Mimi nimetembelea hospitali ya mkoa wa Dodoma. Kwa kweli hali ni mbaya sana kwasababu huduma inayoendelea ni ya usafishaji vidonda tu.
Uko sahihi kabisa.....pata picha kila kitu kitakapokuwa kimesimama.....
Pili je, tunamuadhibu nani hapo?? serekali? Kwa maana ya nani?Kikwete Pinda au hussein Mwinyi wa wategemezi wao??.....
Kama unaweza kuona ushabiki unaofanywa sasa kushabikia mgomo wa madaktari, mbona hukuuona ushabiki wa unaowatetea wakati wa uchaguzi? waache walipe gharama ya maamuzi yao ya kishabiki!
Sio tu tunaweza mkuu Ciril, pia ni haki yetu kuandamana kuzidai haki hizo zinazoambatana na huduma za afya, hatimaye kukiadhibu kwa kukifuta chama kinachowadharau wananchi [/color=red]ikibidi kuleni nyasi lakini lazima ndege ya rais inumuliwe[/color] this time wameongeza ukali wa adhabu [/color=red]kufeni, hatuongezi mishahara ya medical doctors kwani mishahara ya wabunge bado haitoshi, posho za wakurugenzi wateule wa jk ndio kipaumbele[/color]
Mi nafikiri tatizo si madaktari, tatizo ni wanasiasa, fikiria wakati wengine wanajiongezea miposho ya safari tena za nje, madaktari wanapunjwa kwa kazi ngumu wanayoifanya, Jamani hii taaluma si ya kubeza. Mi nilipenda sana kuwa daktari, lakini nilipofika muhimbili pale, wiki mbili za kwanza tu nikaona pagumu hapa, huyooo nikatimkia Mzumbe nikapiga BBA yangu.
Wakati si tunapiga shule miaka 3, hawa jamaa wanapiga 5, halafu tunawazidi na maslahi kwa kupiga kwetu domo. hii si sawa, wagome tu serikali iwe sikivu. walazimishwe kusikiliza
View attachment 57264
cheki kama hawa jamaa hapa wanasinzia tu, halafu wanakula maposho kibao ya m.a.t.a.k.o
Wacha utani! unamaana kazi ya madaktari ni ngumu kuliko ya wabunge wanaojadili bajeti na kuipitisha kwa kishindo?wafundishe watz kufanya wanachopaswa kufanya, kutimiza wajibu wao! si sahihi madaktari kulalamikia maslahi yao, sisi wananchi na hao unaowatetea tulipaswa kuilazimisha serikali iwajali madaktari wanaotutibu, kumbuka kazi yao ni ngumu, hata pale ndugu wa mgonjwa hawaruhusiwi kumgusa ndugu yao madaktari lazima wamhudumie! unayajua haya? km unaujua ukweli huu huwezi kuwalaumu madaktari kwa kile wanachofanya sasa, wamelazimika kufanya hivyo.
Wacha utani! unamaana kazi ya madaktari ni ngumu kuliko ya wabunge wanaojadili bajeti na kuipitisha kwa kishindo?
Naungana nawe kwa hili, ni mbaya wananchi kusapoti huu mgomo, ni vizuri tukajadili au kujenga mijadala itakayoleta suluhu nzuri pasipo kuleta athari mbaya jamii hasa wale ambao maskini. Mimi na hawa wengine ambao wako huku JF huenda tuna uwezo wa kwenda Hindu Mandal, Aga Khan na kwenine... lakini kuna ambao hizi hospitali za serikali ni mkombozi wao. Tunavyoshabikia huu mgomo utokee tunadhani nani ambaye ataathirika!!!! Ni watanzania hawahawa ambao hata humu JF hawapo. Yes it's true that kuna uzembe mkubwa wa serikali lakini hatuwezi kusema Doctoros wagome!Tuache kusapoti u jinga na u huni unaofanywa na hawa jamaa....Hiyo kamati imesajiliwa wapi?? Kwahili sijawahi kuunga na wala sitoliunga mkono....Ninyi shabikieni lakini athari zitakazowapata mama ana baba zenu wakiwamo bibi na babu zenu ambao hamuishi nao ndo mtajua.....hata kama tunadhani tunaikomoa CCM na serekali..nadhani strategy hii ni mbovu na haifai na wala haitatufikisha popote....Nakaribisha matusi na kejeli kama ilivyo kawaida ya baadhi ya wana JF ambao hatutaki kusikia second opinion....