Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

There your are! jamaa anachokifanya ni kukikampenia CCM kwa gharama yoyote ile ili ikishika dola apate malipo ya kazi yake, watu wakumbuke ya Makonda! kamtukana EL, kampiga Warioba then nini kimefuata si ukuu wa wilaya tena Kinondoni! Kwa maana nyingine HP kila akichekiiiii na yeye anaona akikomaa kuichafua UKAWA na EL mbona cheo kinakujaa.Vilevile NGO hazimlipi tena maana donors now wamekuwa wakali ka nini wanataka wapate thamani ya pesa yao kwa kila senti wanayotoa, so HP hana mahali pa kula ka zamani kilichobaki lazima afanye siasa maana anajua itamlipa tena fasta!

Kwani na mtatiro anatafuta cheo ?
 
danimutta

Nakubaliana na ww ktk bandiko lako kwa baadhi ya hoja lakini natofautiana na ww ktk kumkubali luwasa ktk harakati za kwenda ikulu.
Pole pole hamshambuli luwasa tu mfuatilie vizuri. Polepole amewakataa wengi SITA,MEMBE WASIRA,JANUWARI NCHEMBA nk.

Mm bado narudia kusema ukiachilia mbali hizo shutuma zinazo mkabili luwasa mm binafi naona mbaya zaidi aina mikakati mfumo anao tumia kupigania kwenda ikulu sio sahihi nahili nililikataa tokea akiwa ccm miaka 25 Lowassa anatumia njia hatarishi kwa taifa za kuelekea ikulu.

Kama tutaridhia aina ya wagombea kama luwasa basi tujiandae kuja kupata rais muuza unga silaha za magendo maharamia na makundi ya kihalifu...
 
Last edited by a moderator:
Sioni kitu cha ajabu kuhusu huyu mtu na wengi wa aina yake. Angekuwea anaishi na ku practice fani yake ktk baadhi ya maeneo duniani angefutwa kabisa. Kosa lake kubwa he is trying to play Jesus Christ kwamba anajua kila kitu na hafichi kitu. Tumemsikia akitoa mambo ya ndani kabisa baina yake na watu muhimu sana. Akibanwa mbavu anayo tabia ya kujitetea kwa kutoa siri za ndani kabisa. He is too young for that and we are living in a hostile environment. Dogo chunga sana.
 
Huwa najiuliza wapiga debe wa CCM kama akina Polepole huwa na dhamira gani mioyoni mwao, ni mapenzi ya ushabiki kama vile nipendavyo Yanga? Maana sina sababu ukiniuliza lakini naipenda na ikifungwa naumia,kwa nini chama cha siasa kinachotakiwa kuleta maendeleo wakati umewapa ridhaa ya kukusanya na kutumia rasilimali zetu kisha wanatuibia wakijinufaisha wao na jamaa zao tu.

Maana ni kashfa juu ya kashfa ya ufisadi kila uchao bado hambadiliki? Mna tofauti gani na ng'ombe? Maana atapewa majani na maji yeye anakamuliwa maziwa na mwisho wake anachinjwa ili aliwe nyama, leo hii hata ukimfungulia geti mwambie akimbie utachinjwa sikukuu inakaribia ng'ombe atarudi zizini kwa upole, basi nyie akina pole pole kama mmeamua kuwa ng'ombe nendeni kwenye zizi lenu la CCM tuacheni tulioamua kuwa ng'ombe mwitu hatufugwi tena
 
Polepole anajifanya anajua, mjuaji, wakati hajui kitu!!!!!!

Wewe unataka kusikia mazuri mabaya wala! Kila kitu kina pande mbili........pia usilazimishe watu waamini utakavyo
 
Kifaurongo

nazipangua hoja za H.polepole kama ifuatavyo

1.si kweli kwamba CCM iliwakata mafisadi , kilichotokea ni kwamba majina ya wagombea haya kufika kwenye kamati ya maadili, kwa ajili ya kuhojiwa kama kuna tuhuma . badala yake mwenyekiti alitoa majina yake 5 na kuyapeleka CC hakuna ushahidi wa vikao kwamba wagombea walikatwa kwa tuhuma za ufisadi baada ya kudhibitika hivyo.

je ni kwanini CCM katika kanuni zake kiruhusu watuhumiwa wa usisdi wachukue fomu, chama makini kingeweka utaratibu wa kuwanyima fomu watuhumiwa wote ili kurahisishia kazi kamati ya maadili

2.chama tawala ndo kinachounda mfumo uliopo, tangu uhuru, mfumo huu umeundwa na katiba, sera, sheria na kanuni ili kusimamia na kuendesha mihimili mitatu ya dola, serikali mahakama na bunge, hivyo basi ili kuubadil mfumo kidemocrasia inabidi chama kinachoongoza dola kiondoke kije chama kingine chenye kuleta katiba mpya, sera mpya, sheria mpya, kanunia mpya na falsafa mpya itakayoongoza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi

3.mabadiliko au mageuzi ni dhana tu. HP anata kusema mabadiliko (physical change) ni reversible" na mageuzi ( chemical change) ni irrevessible, hoja yake haiondoi ukeli kwanba wanaozuia mabadiliko/mageuzi ni CCM,wanatumia wingi wao bungeni, wanatumia rasilimali za nchi tulizo wakabidhi, wanatumia vyombo vyetu vya dola

4. si kweli kwamba lowasa ni taasisi mbona alipokuwa CCM hakuwa Taasisi alipoingia ukawa akawa taasisi, kama alidhibitiwa ingawa si kwa haki akiwa ccm nini kinazuia asithibitiwe akiwa ukawa?? hata huko alikoingia ni taasisi kubwa, alafu tunachokipigania ni katiba itakayo dhibiti taasisi ya uraisi, au HP bado katiba ya zamani ambayo Raisi ni mungu Mtu iendelee baadaya CCM kumpitisha Maghufuli.

madhumuini ya kuanzishwa kwa ukawa ni "Rasimu ya pili ya katiba" malengo hayo bado hayajatimia hata kama Lowasa kajiunga na UKAWA mpaka malengo ya ukawa yatimie baada ya miaka mitano ijayo,

Lowasa alipotuhumiwa na kamati ya bunge alijiuzuru hasubiri bosi wake Kikwete ajiuzuru, eti HP anadai Maghufuli alipotuhumiwa waziri mkuu ndo angejiuzuru, huu utaratibu wa wapi?? huyu HP mbona yuko biased kiasi hiki??
 
Last edited by a moderator:
... Polepole Ni Mzushi Na Mzandiki

Wabongo bwana juzi tu wakati wa katiba ulikuwa unawafukuza watoto wasiangalie katuni ili uangalie na kusikiliza hoja za polepole........leo hii mwee!
 
Picha nayopata ni mtu aliyevimbiwa sifa na kujiona mawazo yake tuu ndio mawazo sahihi. Pia CCM walivyokata wakina membe na lowasa anaona kams CCM walifuata ushauri wake basi kichwa kimekuwa kikubwa kweli!
 
channel ten ....sasa mumezidi.Tunakwenda Hot mix kule EATV.kwani pole2 amelipia hicho kipindi.
 
UKAWA ni muungano wa watu wenye fikra zisizoeleweka hata kwa wakawa wenyewe. Hadi hapo walipoita askari mamluki ili kuwapambanulia namna ya kushika madaraka ya dola ambayo wamelilia miaka yote. Nawaelewa vema akina Lipumba et.al,. Ambao kidoogo fikra zao zimejipambanua kutoka fikra butu. Sitoshangaa siku moja watakapoanza kukwaruzana. Hivi kweli walihitaji kuonyeshwa na mccm namna ya kimweka mwali ndani?
 
Picha nayopata ni mtu aliyevimbiwa sifa na kujiona mawazo yake tuu ndio mawazo sahihi. Pia CCM walivyokata wakina membe na lowasa anaona kams CCM walifuata ushauri wake basi kichwa kimekuwa kikubwa kweli!

Kuna hii kitu jombi! ""ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI "" umesahau nini?
 
kuliko aliyeuza chama?

Bora aliyeuza chama kuliko aliyeuza nchi ambaye katufanya kuwa watumwa wa ukoloni mamboleo anaetuacha tukidaiwa akiwemo na ww lak 6 kila mtz huku akisain sheria za kutupora rasilimal zetu za nishart y gesi na kuendlea kutuacha watupu kama watoto yatima. Na ipo siku mtajibu haya na team yenu yote msifikir Mungu hajaliona choz la mnyonge
 
Lowassa ndio alikua waziri mkuu sasa Nani angewajibika kama sio yeye alieshindwa kujitetea akakimbilia kuachia ngazi,mnafikiri tumesahau kilichotokea,video zipo u tube.Muulizeni lowassa kwanini hakuitumia nafasi waliyompa kina mwakyembe kujitetea?muulizeni hilo

Twende taratibu mkuu, nimekuelewa sana. Hoja ya Polepole ni kwamba mdogo anapokosa mkubwa ndiye anawajibika. Kwa mfumo huohuo Lowassa alikuwa naye katumwa na mkubwa wake na unamjua mkubwa wake Lowassa alikuwa nani. Hoja iko hapo kwa nini kwa Magufuli Polepole aseme katumwa, kwani Lowassa alijituma mwenyewe?
 
mliberali

Mimi ni mtu wa kujifunza, hoja zako nawaachia wengine wazitolee ufafanuzi na ni kwa sababu mengine uliyoyaeleza ndiyo aliyotatolea ufafanuzi Polepole kupangua hoja za Mtatiro.

Labda niulize na nijifunze toka kwako kitu kimoja tu. Iwapo Waziri Mkuu aliweza kusimamia ujenzi wa Shule za kata uliokuwa ukifanywa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi, Ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma uliokuwa ukifanywa na Wizara ya Elimu ya Juu ikishirikiana na wizara ya Ujenzi, Kwa nini hakusimamia uuzwaji wa nyumba za Umma?

Kuuzwa kwa nyumba za serikali yalikuwa ni maagizo ya nani, waziri, baraza la mawaziri au bunge? inawezekana waziri akaamka asubuhi na kuanza kufanya analolitaka bila kuulizwa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom