Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Kamabado muda itakubidi usubiri kupata jibu.
Huwezi juwa hata mm mwenyewe naweza nikapendekezwa au nikaobwa kugombea hiyo nafasi na chama changu kwa sababu sifa ninazo.
Nikulize ww sasa hili swali uliloniuliza mm?
 
Kwa ujumla HP anajichanganya sana. Ni mtu ambaye anapigia chapuo Magufuli kwa hoja za kitoto nad double standards iliyopitiliza. Ni aibu kwa mtu anayejifanya msomi wa kiwango hicho kushindwa kujenga hoja zenye mantiki na badala yake analeta dhana na kuzitafsiri apendavyo yeye.

HP ameshindwa hadi sasa kufafanua yafuatayo;

1. Mgombea Urais hapaswi kuwa na 'tuhuma'. Sawa. Lowassa anatuhuma ya Richmond ambayo waliowajibika ni
mawaziri Nazir Karamagi na Msabaha. Magufuli ana tuhuma ya kuuza nyumba za serikali kifisadi na tena kwa watu
wasiostahili tena wengine anadaiwa kuwa na uhusiano nao
HP angeleeweka kama angekuwa anawapinga wote Magufuli na Lowassa, lkn kutmuia kanuni hii dhidi ya Lowassa
na hapo hapo akimpigia chapuo Magufuli ni udhaifu uliopita mipaka.

2. Kuhusu ,dhana ya madiliko na mageuzi hapa HP ameonesha udhaifu na utoto uliokithiri. Anaimba ama vitu
asivyovijua au alivyokaririshwa muda mfupi kabla ya kuingia studio. Hivi Ndugu Polepole anataka kufundishwa
kuwa kutoa chama 'twawala' madarakani na kuingiza chama kingine sio mwanzo mzuri zaidi wa kuleta kile
anachokiita mageuzi badala ya kuacha chama kilekile, watu walewale, sera zilezile, katiba ileile na utendaji uleule?
Anahitaji kweli kuelimishwa kuhusu hili au ni dhihaka yake tu kwa wasikilizaji wake? Hivi mjumbe huyu wa Bunge
lile la katiba ameshasahahu kwamba uandikwaji wa katiba mpya pekee una mchango mkubwa ktk kubadilisha
mfumo wa utawala, uongozi na uendeshaji wa mambo?

Mwisho, niseme tu tukimchagua Magufuli tuatakuwa tumebadilisha sura ya Rais pekee lakini kupitia Lowassa tutakuwa tumebadilisha chama, watu, sera, katiba, ukubwa wa serikali na staili ya uendeshaji wa mambo
 
PRINCE CROWN

Namshukuru sana Polepole kwakuwa jana alinielimisha tofauti ya MABADILIKO NA MAGEUZI na pia kunifumbua macho kuwa EL ni yeye kama yeye ni MFUMO. Funzo lingine alilonifundisha kwa maana ya kunikumbusha ukweli kwamba kubadili mfumo siyo kubadili chama. Pole pole alikuwa sahihi kwa 95% kwa mujibu wa tathmini yangu.
 
Last edited by a moderator:
tatizo ni watu kutotaka kusia wasiyoyapenda.POLEPOLE YUKO SAHIHI
Hahaaaa ni mwamuzi wa mpira kati ya man u na chelsea lakini ametangaza kuwa ni mpenzi na mwanachama wa MAN U teh,teh,teh upo hapo???
 
Mpaka sasa kwa hawa aliozungumza nao wamemshindwa. Si kwamba ana hoja nzito sana bali anachotetea kipo sahihi zaidi. Ni sawa na Sheikh au mchungaji kumtetea mzinifu. Ni lazima ashindwe hata kwa mfuasi wake kwa kuwa anatetea uovu.
 
Amepewa pesa za media kuing'arisha ccm wakati juzi alipokataliwa na ccm hiyo hiyo kuhusu na katiba leo amekaa bila haya kuinanga UKAWA kweli njaa haina Bouncer!
 
polepole nchi hii hakuna msafi maana yake hata wewe ni mchafu sna
 
PRINCE CROWN,

Nikuulize swali! Hivi mnaituhumu ccm kwa lipi hasa. Ukijibu hili nitaendelea kukuuliza mengine
 
Last edited by a moderator:
Humphrey Polepole kama Samuel Sitta!! wameshindwa kupambana na mfumo dola wa CCM, wameamua kujiunga nao! Pole Humphrey Polepole!
 
Mpaka sasa kwa hawa aliozungumza nao wamemshindwa. Si kwamba ana hoja nzito sana bali anachotetea kipo sahihi zaidi. Ni sawa na Sheikh au mchungaji kumtetea mzinifu. Ni lazima ashindwe hata kwa mfuasi wake kwa kuwa anatetea uovu.
Mimi nimetoa majibu ya James Msonge kwa Polepole,,
 
Kama walizalisha watashindwa nini kuitokomeza? aliyekuzaa si ndo anakufahamu vizuri? na mwiba si unatokea ulikoingilia? kama walileta wao basi ni wao wanaoweza kuutokomeza kwani siri ya mtungi aijuaye ni kata
 
mwendomdundo,

Hakuna kampeni yoyote duniani inayo fanyika bila pesa. January Makamba ametumia billion 4.7 kutangaza nia, Magufuli ametengewa almost 1 trillion kwa ajili ya uchaguzi, utaona utaniambia...

Tusipoteze viongozi bora kwa tuhuma cha kipuuzi-- Benjamin William Mkapa
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa napenda kuwa shukuru wote ambao wamekuwa wakifuatilia mijadala mbambali kuhusu uchaguzi mkuu.Na hasa wale ambao wamekuwa wakifuatilia mijadala mbalimbali ambayo amekuwa akiifanya Mh.Polepole.lengo langu ni kutaka kumuuliza huyu Mh.POLEPOLE, maana amekuwa akimsakama sana Lowasa popote pale anapokuwa akichambua siasa,huku akisimamia ajenda yake ya maadili kwa waagombea,hasa ule alioufanya chanel 10, akiwa pekeyake na alipokuwa na MH.msigwa na Mh.Mtatiro.

Naomba kukuuliza kati ya Magufuli na Jaji Agustino ni nani mwenye maadili zaidi?kwasababu unajinasibu kwamba mliwaomba kamati kuu kuwakata watu wasio na maadili na unasema wamekatwa kweli. kwani naamini katika wagombea wale wote sidhani kwamba wanamzidi huyu Jaji kwa maadili. kama ni kweli magufuli anamaadili kuliko Jaji basi mimi nitahisi kwamba unaajenda ya siri ya kumchafua Mh.Edward Lowasa.

Pili, kipindi cha Jana ukiwa na Mh.Mtatiro ulikuwa ukisisitiza kwamba taasisi ya uraisi ni kama kuchagua Padri au Askofu,Jamani ni kweli tumefika huko kwenye masuala ya siasa au viongozi kuweka sifa kanakwamba tunachagua viongozi wa kidini?na kama hivyo basi hata huyo magufuli unaemsema hatufai katika nchi hii,na hakuna kiongozi mwenye sifa hizo na kama tunataka iwe hivyo basi tubadili nchi hii iwe na utawala wa imani fulani hapo ndo tutaweza kupata kiongozi kama unavyotaja hizo sifa zako.

Mimi nikuombe tu achana na Mh.Edward Lowasa. humutedai haki Mzee wa watu,kwani ndani ya chama chako mmepitisha watu waliofanya ufisadi na unadhihirika wazi na hainahaja ya kuwataja na wamehojiwa na tume ya maadili,mwache nae lowasa aombe ridhaa ya kuongoza Tanzania,kiujumla humtedei haki,pia wewe sio msemaji wa watanzania,jinsi unavyoseme kwamba utazunguka nchi nzima,kusema movu ya lowasa,mbona husemi maovu ya raisi au JK ambayo anayo lukuki? asante. taaluma yangu mwalimu
 
Kama walizalisha watashindwa nini kuitokomeza? aliyekuzaa si ndo anakufahamu vizuri? na mwiba si unatokea ulikoingilia? kama walileta wao basi ni wao wanaoweza kuutokomeza kwani siri ya mtungi aijuaye ni kata

Hahaha kunawatoto wengine hawashikiki,,,,mbaya zaidi hadi walezi Wa chama nao mafisadi watajitokomeza??
 
Back
Top Bottom