Niongezee yafuatayo kwa ushauri mzuri wa Msonge.
Watanzania lazima tuwe waangalifu/makini na kikundi cha watu wachache wanaojitahidi kutuwekea agenda zao kama vipaumbele vya taifa tukielekea uchaguzi mkuu 2015. Hawa wanapewa airtime nyingi isivyostahili kwenye TVs kurudiarudia propaganda zao mbovu ili hatimaye watu waamini ni wakweli kwa staili za akina Hitler - " Ukiurudia uongo mara kwa mara, watu wengi wataamini kuwa ni ukweli".
Kwanza ieleweke kwa mfano, kutofautiana maoni katika mijadala ya katiba ni jambo la kawaida katika mfumo wa demokrasi. La msingi ni kutoa nafasi ya wazi kwa raia kupigia kura (referendum) rasimu au hoja zinazopendekezwa ili maoni ya wengi yapite - na hapa Tanzania ukiondoa uchakachuaji wa wazi uliyofanywa na CCM na mfumo usiofaa wa bunge la katiba ingewezekana kuwaachia wananchi kuamua muundo wa serikali ya muungano (2 au 3) kama swali la msingi kama CUF na raia wengi walivyodai miaka yote.
Hivyo ni upuuzi kwa Polepole kumshkia bango Lowasa na wengine kuhusu mawazo yao juu ya jambo hili. Hata Kenya baadhi ya viongozi waliopinga katiba mpya ndiyo wamechaguliwa (Ruto n.k.) kuongoza nchi na kuitekeleza. Kuhusu sakata la Richmond watu wakweli na wenye akili wanajua kabisa watu wengi na serikali yote ilihusika katika maamuzi.
Richmond ilitokea katika mazingira ya dharura ya taifa ya umeme (national emergency). Nchi ilikuwa inaelekea kuingia gizani na kusababisha hasara ya mabilioni kila siku. Mchakato wa tenda za kununua mejenereta usingefuata taratibu za kawaida hivyo ilibidi maamuzi yafanyike haraka - na tusisahau hata hizo bodi za tenda za mashirika ya umma kama Tanesco zimekumbwa na tuhuma/kashfa nyingi za ufisadi miaka yote zikisababisha hasara na utekelezaji wa miradi.
Kilichotokea wafanyabiashara wajanja wakajitokeza kama agents na hili ni jambo la kawaida pote duniani sababu huwezi kununua mitambo hiyo moja kwa moja kiwandani katika mazingira ya dharura. Issue ni kwamba Richmond waliposhindwa kumobilise pesa na logistics ndipo utapeli wao ulipogundulika!
Ni serikali iliyogundua tatizo wala siyo kamati ya Mwakyembe. Sasa Lowasa na Waziri wa Fedha Meghji wamethibitisha kwamba mpaka hatua hii hapakuwepo malipo yoyote yaliyofanyika! Ni baada ya hapo siasa na jazba zikaingia, Lowasa akajiuzuru na kupelekea nchi kulipa faini kwa amri ya mahakama - the rest is history.
Mapendekezo mazuri ya Zitto kuepusha faini hiyo na hasara yalipuuzwa na akina Sitta na wapambe wake ili watimize lengo lao kummaliza Lowasa. Wengine wanatuletea stori za Mwl. Nyerere zilizotokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Jamani Mwalimu alikuwa na maoni mengi tofauti kwa watu wengi na mabo mengi katika kipindi cha maisha yake. Nayeye alisema alifanya makosa mengi na hakuwa malaika! Yeyote anaye jitwisha jukuma la kumsemea mzee wetu huyu (iwe walipokuwa Msasani au Butiama) ni vizuri akaacha.
Watanzania wa leo wana uwezo wa kuwatambua viongozi wanaofaa kwa kuona matendo yao. As a nation we have moved on after demise of Mwalimu. Vinginevyo hao wanaomsemea Nyerere washinikize CCM irejeshe Azimio la Arusha na miiko ya viongozi kama ilivyokuwa wakati wake. Mwisho yupo Mzee mmoja ninaye mheshimi sana ambaye kwa kushirikiana na "kitengo" ndani ya CCM amekuwa mstali wa mbele kukata wagombea akiwemo Lowasa kwa hoja ya maadili, tamaa ya madaraka n.k.
Ni ajabu, Mzee huyu aliwahi kuwa Spika wa Bunge na wakati huohuo akakubali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya VODACOM - kampuni kubwa ya mashirika binafsi! Nilimpenda mzee mwingine mkweli wa CCM aliyesema Lowasa amekatwa kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo miongoni mwa viongozi na wanachama wa CCM.
Hoja yangu hapa watanzania na hasa wana UKAWA tuungane kukabiliana na changamoto halisi na taifa ambazo ni mabadiriko ya katiba na mfumo wa utawala- ili tupate katiba itakayopunguza madaraka ya Rais, kupunguza ukubwa wa serikali, Kuimarisha taasisi huru za utawala bora (mahakama, bunge, taasisi ya kupambana na rushwa, uchaguzi) ikiwezo "vetting" ya viongozi, devolved government na uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu, uwiano sahihi katika muungano.
Magenge ya wachambuzi uchwala (Polepole, Mkinga, Mtikila, Kasoli n.k.) yasiachwe kutupangia agenda ambazo zinajikita kuwachambua watu binafsi kwa maslahi ya kulinda watawala na "status quo", badala ya issues za msingi.