Nchini China kuna mvinyo unaojulikana kama "SNAKE WINE" ambao huandaliwa kwa kumzamisha nyoka mzima ndani ya pombe iliyotenegenezwa kwa nafaka na huachwa kwa miezi kadhaa, Nyoka afe na kisha aoze, ili mvinyo huo uwe na ladha ya kipekee.
Lakini ipo njia nyingine ambayo mvinyo huo wa nyoka huandaliwa, muandaaji humuua nyoka na kupata damu yake na nyongo ili achanganye na pombe iliyotenegenezwa kwa nafaka na hutumiwa kwa imani kuwa unaimarisha afya na kuongeza nguvu za kiume.
Hakuna taarifa za madhara wala kifo kilichowahi kutokana na mvinyo huo, lakini pia hakuna mtu aliyewahi kujitokeza hadharani kuthibitisha kuwa amewahi kutumia mvinyo huo tata.
View attachment 2608361