Mada maalum ya walevi na wanywa Pombe

Mada maalum ya walevi na wanywa Pombe

Duh!brother don hang out with people ambao huwajui kihivyo ......sio kila mtu unayekutana nae JF na akataka kukujua ni mtu mzuri,jua ww unatumia real ID na wengine wanatumia fake ID's.Mi nakujua vzuri and am ur friend na unanijua vzuri na tushakaa sehem mbalimbali na kusaidiana pia kwenye mambo tofauti nakupa as an advice.
Duh aisee pole sana Mkuu!

Sent from my SM-M305F using JamiiForums mobile app
 
Nilitamani kukamilisha kila kitu ndio nilete mrejesho lakini nisiwaweke sana naomba nisimulie sehemu ya kwanza!

NB: sina bifu na mhusika na kama atahisi nimemuonea nitaomba aje hapa anisute!

Huyu ndugu ni mojawapo ya wanaJF wa mwanzo kabisa kufahamiana kwa maana ya kuonana live mwaka 2014.. Na mpaka tunaonana tena juzi ilikuwa ni mara ya tatu

Siku ya Jumatatu wiki hii nilienda kikazi nje ya Dar mwendo wa kilometers 100 hivi.. Kufika eneo husika nikakuta mhusika hayupo, hivyo nikasogea bar ya jirani na hapo nikapate lunch maana ndio ilikuwa mida yake!
Naingia pale mahali nikakutana uso kwa uso na mhusika, tukasalimiana na kushangaana kule tulikokutana kama tukio la bahati kubwa
Nilikuta yeye muda huo anatoa lock..tukakaa counter ambayo ilikuwa kwenye mzunguko wa hexagon na kati yangu mimi na yeye tukatenganishwa na mdau mwingine niliyemkuta naye hapo
Alinikaribisha kinywaji kikali lakini nikamwambia lazima nile kwanza na nisingeweza kunywa muda ule wa kazi
Kibingwa akaniwekea kidogo nikanywa na baadae nikala
Nakaribia kuondoka akaniongeza .. Lakini kuna muda alichomoka mara moja na kurudi.. Kwakuwa nilikuwa busy na kupiga simu sikufuatilia kila kitu
Nikanywa kile kidogo tena alichoniwekea tena nikamaliza na kumuahidi kurudi nikimaliza ishu yangu.. Nikatembea kurudi kwenye ofisi husika na kukuta mhusika hajarudi., nikasema ngoja nikajiegeshe kidogo kwenye gari kwakuwa nilihisi uchovu wa ghafla!
Kule kujiegesha nililala masaa mawili mpaka nilipokuja kuamshwa.. Mwenyeji wangu akanitania kuwa naonekana mchovu inawezekana weekend nilipiga maji sana
Nilimaliza na mwenyeji wangu. Na kuondoka nikapita pale alipokuwa rafiki yangu wa JF.. Kuna vitu vya kushangaza vilitokea pale
1. Niliona Kama wahudumu waliokuwa wamekaa meza moja wananishangaa
2. Jamaa kama alishtuka sana na kama kutaka kukimbia
Mpaka hapo nilikuwa sijahisi kitu kibaya.. Nikamwambia nimeshamaliza nimepita kumuaga .(alikuwa amashasema tutaondoka wote kurudi dar)
Niliagiza pepsi baridi sana maana koo lilikuwa kavu kupita maelezo.. Nilihisi kitu kwa jamaa kama alikuwa na mshangao na kuchanganyikiwa kidogo ... Ikabidi nmwambie tu amalizie taratibu kinywaji chake mimi niwahi maana muda ulikuwa umeshasogea
Niliondoka na kuendesha salama mpaka dar lakini njiani nilikunywa pepsi nyingine mbili huku nikihisi uchovu wa ajabu..nilifika home salama lakini nilichoweza ni kujimwagia maji tuuu
Nilijitupa kitandani na kulala fofofo mpaka saa saba usiku.. Kustuka nikakuta tena koo limekauka mno nikanywa maji tena lita nzima.. Nikalala tena mpaka saa moja asubuhi ..(sio kawaida yangu kulala hivyo)

Asubuhi hiyo ya Jumanne ndio nikawa ninajihisi nafuu ya uchovu na kiu kali.. Nikaanza sasa kukumbuka kila kitu kila tukio.. Nikalala tena mpaka saa tatu.. Nilichelewa kwenda kazini .. Baada ya lunch nikalala tena.. Yaani ilikuwa ni mwendo wa kulala na kiu

Hii ni part one
Pole sana mkuu
 
TAARIFA MBAYA
Jana kuna mwana JF kaniwekea madawa ya kulevya kwenye kinywaji .. Nadhani nia ilikuwa kuniibia gari na pengine pesa simu nk.. Hakufanikiwa... Nitaleta taarifa kamili baada ya kukamilisha mambo kadhaa
Bro pole Sana aisee..! Hope uko safe
 
Part 2
Je nilijuaje kama ni nimewekewa madawa ya kulevya?
Mimi sio mgeni wa pombe .. Nimeanza pombe 1985.. Na katika maisha yangu nimeshakutana na pombe feki hizi kali.. Mziki wake hizi si wa kitoto zina hangover kali kiwango cha 5G na zinaumiza kichwa vibaya mno na nyingine unatapika hasa
Niliwahi kuwekewa madawa Kinondoni way back 2005 nimesimulia hapa hilo tukio..
Ukiwekewa madawa ulevi wake unakuja hapa utosini na macho yanakuwa mazito.. Unachotamani ni kufumba macho na kulala.. Waangalie mateja... Kingine ni kiu kali na kukaukiwa koo na midomo
Siku husika baada ya kuondoka ule mchana na kwenda kulala, baada ya kuamka nilikuta missed call yake.. Nilimpigia na kumuuliza kunani .. Akasema alikuwa anacheki kama nitarudi
Kuna mengine mengi sitayaweka wazi hapa mpaka nikamilishe hayo mengine..
Pole sana mkuu
 
TAARIFA MBAYA
Jana kuna mwana JF kaniwekea madawa ya kulevya kwenye kinywaji .. Nadhani nia ilikuwa kuniibia gari na pengine pesa simu nk.. Hakufanikiwa... Nitaleta taarifa kamili baada ya kukamilisha mambo kadhaa

Pole sana, hizo pombe mlikuwa mnanywea vichochoroni boss ama ilikuaje?
 
Tangu Jumatatu leo ndio nashtua mabandama
JPEG_20211028_172228_4263800451864823447.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom