Machinga waanza kumlilia Hayati Magufuli

Hawa wa Mwanza nawafahamu vizuri sana. Nilikuwa mmoja wa watu waliowashauri waipigie kura CCM 2020 kwa Rais na Mbunge Mabula (tena huyu labda aanze kuaga kabisa kama suala la machinga litaendeshwa hivi). Hivyo, kwenye kampeni za 2025 usishangae wanatelekeza mikutano ya kampeni kama walivyotelekeza meza zao leo. Na sijui kama Mh. Mabula atakuwa na ubavj wa kuwashawishi tena nikifikiria kazi kubwa tuliyoifanya ya kumrudisha 2020.
Kwamba Mabula hajawatetea kwa wanavyoondolewa?
 
Hatimaye kilio cha machinga kumlilia JPM, chaanza kusikika, baada ya gari la matangazo kupita mitaa ya tandika na kuwaambia kuwa mwisho wa kupanga bidhaa zao, pembeni mwa barabara, mbele ya maduka, na kwenye hifadhi za barabara mwisho ni 18.10.2021.Hivyo wanatakiwa kuondoka mapema na kwenda sehemu walizopangiwa, baada ya muda huo, wasije kuilaumu serikali!!Ndipo wakaanza kuimba "tunakukumbuka jpm mtetezi wa wanyonge sasa haupo tumeanza kunyanyaswa" Sasa naona serikali imeamua kweli, ni jambo zuri sana kwani ilikuwa ni kero tupu.

Waende wakamfufue bac. Waache kulialia
 
Hawa wa Mwanza nawafahamu vizuri sana. Nilikuwa mmoja wa watu waliowashauri waipigie kura CCM 2020 kwa Rais na Mbunge Mabula (tena huyu labda aanze kuaga kabisa kama suala la machinga litaendeshwa hivi). Hivyo, kwenye kampeni za 2025 usishangae wanatelekeza mikutano ya kampeni kama walivyotelekeza meza zao leo. Na sijui kama Mh. Mabula atakuwa na ubavj wa kuwashawishi tena nikifikiria kazi kubwa tuliyoifanya ya kumrudisha 2020.
Kichaa mwingine huyu hapa, eti "kazi ngumu ya kumrudisha tena 2020". Hivi 2020 kulikuwa na uchaguzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimaye kilio cha machinga kumlilia JPM, chaanza kusikika, baada ya gari la matangazo kupita mitaa ya tandika na kuwaambia kuwa mwisho wa kupanga bidhaa zao, pembeni mwa barabara, mbele ya maduka, na kwenye hifadhi za barabara mwisho ni 18.10.2021.Hivyo wanatakiwa kuondoka mapema na kwenda sehemu walizopangiwa, baada ya muda huo, wasije kuilaumu serikali!!Ndipo wakaanza kuimba "tunakukumbuka jpm mtetezi wa wanyonge sasa haupo tumeanza kunyanyaswa" Sasa naona serikali imeamua kweli, ni jambo zuri sana kwani ilikuwa ni kero tupu.
wamachinga ni mpango wa CCM, hawana +ve impact kwenye uchumi wa nchi. wanatumiwa na waagizaji bidhaa kukwepa kodi, nguvu zao hazitumiki kuzalisha ili kuongeza uchumi ktk nchi. pia ni maficho ya vibaka.
 
Back
Top Bottom