Kila mtu atakubaliana na mimi kuwa Bunge hili la 10 litakuwa ni moto na lenye changamoto za kila aina baada ya upande wa Upinzani kuingiza Wabunge wengi zaidi kuliko wakti wowote tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. Kwa maana hiyo basi Bunge hili linahitaji Spika makini,asiye na tuhuma yoyote,msomi na anayejua sheria na taratibu zote za kusimamia na kuendesha Bunge.
Kwa vile CCM wamemng'oa Samwel Sitta ambaye ndiye angeweza kulimudu Bunge hili kwa kisingizio cha kuweka Mwanamke awe Spika kwa mara ya kwanza tangu tupate uhuru basi Upinzani utakuwa umepata nafasi nzuri ya kuchukua kiti hicho kupitia Mhe. Mabere Marando wa CHADEMA.
Nina sababu kuu 4 za kutaka Mabere Marando apewe kiti hicho:
- Kwa vile Rais Kikwete kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa alisema kwamba HAKUNA ALIYESHINDA BAALI NI WATANZANIA WOTE TUMESHINDA na akaahidi kuanza kutibu majeraha yaliyotokana na kampeni za Uchaguzi basi huu ni wakti wa kuonyesha hiyo DHAMIRA. Kuwa CHADEMA ambao wameporwa USHINDI WAO MEZANI WAPEWE KITI CHA USIPIKA ili kutibu majeraha yaliyosababishwa na harakati za Uchaguzi.
- Kwa vile Bunge la hili la 10 litakuwa la moto na Changamoto za kila aina inatakiwa Spika makini,mwenye msimamo na asiyeyumbishwa na hoja ya namna yoyote. Kwa vile CCM wameweka MWANAMKE nachelea sana kama ataweza KUKABILIANA NA MIKIKIMIKIKI ya Bunge la 10. Kweli wanawake wanaweza siyo sehemu zote na mambo yote!Niwaulize CCM mbona hawajawahi kuweka Rais Mwanamke, IGP mwanamke,Mkuu wa JWTZ mwanamke au Jaji Mkuu. Kwanini iwe kwa Spika tena kwa Bunge hili?Hapa CCM wameamua kumkomoa Sitta kiujanjaujanja. Ukweli ni kwamba Mwanamke hataliweza hili Bunge. Sana sana atakuwa anaongozwa kwa REMOTE CONTROL na MAFISADI waliosuka huu mpango wa kumng'oa Sitta. Nahofia kuwa tutashuhudia vilio vya Spika mwanamke na malalamiko ya kuburuzwa na kuonewa. Hivyo Mabere Marando anafaa.
- Kwa vile tayari ndani ya CCM kuna mgawanyiko au Makundi yaliyosabaishwa na Chenge na Sitta haitakuwa busara kuchagua Spika kutoka ndani ya CCM kwa vile kutaendeleza mgawanyiko uleule maana hata hawa wanawake wa CCM wana makundi yao. Nawaomba Wabunge wa CCM wampigie Kura mgombea wa CHADEMA Mhe. Marando kwa nafasi ya SPIKA na naibu wa Spika wampe huyo wa CCM bila kujali kama atakuwa mwanamme au mwanamke ili ku-neutralise situation.
- CCM wenyewe wanajua kabisa wakti wa Spika Sitta kulikuwa na mijadala na Miswada ambayo ilikuwa inaahirishwa kama Sitta amesafiri nje ya Bunge mpaka anaporudi mfano ni mjadala wa Richmond, Anne Makinda hakuweza kuuendesha mpaka Sitta alipokuwepo. Hii ina maana kwamba CCM wanajua mwanamke hawezi kumudu kusimamia mijadala mijadala na hoja nzito za Bunge.
Nahitimisha kwa kusema kuwa safari hii Spika atoke upinzani kwa sababu kuu nilizozitaja hapo juu. Kama CCM watalazimisha mwanamke wao apite whether atakuwa Anne Makinda,Anne Abdulla au Kate Kamba wajue kabisa ITAFIKIA SIKU WABUNGE WATAPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA SPIKA WA BUNGE KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA BUNGE KWA KUTOKUWA NA MSIMAMO.
Hii ndiyo picha ninayoiona.