Mfumo wa Taarifa za kiutumishi wa walimu katika Tume ya Utumishi "TCSMIS" na Shahada za uzamiri

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,659
3,575
Napenda kuipongeza tume kwa kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha walimu wanapatiwa huduma kuendana na mahitaji ya kiteknolojia ya sasa. Jambo hili kwa kweli linatia moyo na limeisogeza huduma mikononi mwa walaji.

Masikitiko yangu makubwa ni kuona mfumo huu muhimu wa Taarifa za walimu ukiacha ombwe la utambuzi wa elimu, licha ya uwepo wa hamasa ya kujiendeleza kielimu. Mfumo huu hauna uchaguzi wa kujaza taarifa kama Mwalimu amejiendeleza na kuwa na elimu katika ngazi ya uzamili.

Huwa najiuiliza ni kigezo kipi kinachotumiwa kuhalalisha kuwa ualimu mwisho ni shahada ya kwanza au postgraduate diploma?. Ualimu ndiyo fani inayojihusisha na elimu kwa upana na undani wake hivyo kitendo cha kuweka ukomo fulani ni fedheha.

Ipo wapi haja ya elimu ya watu wazima "lifelong education" ikiwa mifumo yetu inabagaza ngazi za elimu na kuzifanya kama kwamba hazipo?. Elimu katika ngazi yoyote ni uwekezaji wenye mrejesho jamii na binafsi, kupo wapi hata kutambua tu ngazi hizo za elimu katika kada ya ualimu wa shule zinazotoa elimu ya msingi?.
 
Napenda kuipongeza tume kwa kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha walimu wanapatiwa huduma kuendana na mahitaji ya kiteknolojia ya sasa. Jambo hili kwa kweli linatia moyo na limeisogeza huduma mikononi mwa walaji.

Masikitiko yangu makubwa ni kuona mfumo huu muhimu wa Taarifa za walimu ukiacha ombwe la utambuzi wa elimu, licha ya uwepo wa hamasa ya kujiendeleza kielimu. Mfumo huu hauna uchaguzi wa kujaza taarifa kama Mwalimu amejiendeleza na kuwa na elimu katika ngazi ya uzamiri.

Masters ya nn kama unaenda kufundisha primary na sekondari ambapo certificate na diploma respectively wanatosha kufundisha? Masters na PhD wanahitajika kufundisha vyuoni. Hatuwezi kukutambua wewe na masters ukiwa unafundisha primary cos utatudai mshahara wa mwalimu wa chuo. Fanya mpango utoke huko ukafundishe chuo tukakutambulie huko. Alafu mangiiii, huwa hatusemi Uzamiri, ni uzamili
 
Aisee...
 
Napenda kuipongeza tume kwa kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha walimu wanapatiwa huduma kuendana na mahitaji ya kiteknolojia ya sasa. Jambo hili kwa kweli linatia moyo na limeisogeza huduma mikononi mwa walaji.

Masikitiko yangu makubwa ni kuona mfumo huu muhimu wa Taarifa za walimu ukiacha ombwe la utambuzi wa elimu, licha ya uwepo wa hamasa ya kujiendeleza kielimu. Mfumo huu hauna uchaguzi wa kujaza taarifa kama Mwalimu amejiendeleza na kuwa na elimu katika ngazi ya uzamiri.

Huwa najiuiliza ni kigezo kipi kinachotumiwa kuhalalisha kuwa ualimu mwisho ni shahada ya kwanza au postgraduate diploma?. Ualimu ndiyo fani inayojihusisha na elimu kwa upana na undani wake hivyo kitendo cha kuweka ukomo fulani ni fedheha.

Ipo wapi haja ya elimu ya watu wazima "lifelong education" ikiwa mifumo yetu inabagaza ngazi za elimu na kuzifanya kama kwamba hazipo?. Elimu katika ngazi yoyote ni uwekezaji wenye mrejesho jamii na binafsi, kupo wapi hata kutambua tu ngazi hizo za elimu katika kada ya ualimu wa shule zinazotoa elimu ya msingi?.
Kiuhalisia kazi yenyewe haihitaji Masters

Mfano unaenda kuspecialize kitu fulani halafu ukirudi shule haiendi kukifundisha hicho kitu

Unaenda kuspecialize kwenye environmental biology huku ukirudi shule unatakiwa kufundisha mada zote na hakuna utofauti na yule mwalimu wa diploma
 
Hivi kufundisha "hii ndio a a a a a a a a a a" unataka mpaka uwe na masters ya Linguistics mzee baba!!!!???
 
Taja majina wewe boya. Kama ndio hilo Victor Mlaki weka hapa
Ila kuna mijitu mingine sijui inatokea wapi, kama thread hujaipenda achana nayo unanifuatilia unanifahamu wewe? Halafu unaniita boya!... Naitwa Victor Mlaki ndiyo nifuatilie tukutane, ila ngoja nikupuuzie tu Kwa sababu unaonekana huna adabu hata kidogo.
 
Kiuhalisia kazi yenyewe haihitaji Masters

Mfano unaenda kuspecialize kitu fulani halafu ukirudi shule haiendi kukifundisha hicho kitu

Unaenda kuspecialize kwenye environmental biology huku ukirudi shule unatakiwa kufundisha mada zote na hakuna utofauti na yule mwalimu wa diploma
Karne hii haipo kazi isiyohitaji maarifa mapana. Fanya tafiti utagundua
 
Kufundusha vishazi huru unahiji masters?

Mashariki ya chekacheka na ngoswe diploma inazitosha kabisa.
 
Kielezo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) ni takwimu inayotumiwa kupima maendeleo ya binadamu katika nchi mbalimbali. Hujumuisha mambo kama vile matarajio ya kuishi, elimu, na kipato cha wastani kwa kila mtu. Kwa mara ya mwisho nilipouzingatia mwezi Januari 2022, takwimu za HDI kwa Tanzania zilikuwa za mwaka 2020, ambapo ilikuwa 0.529, ikiiweka Tanzania katika kundi la maendeleo ya binadamu kwa kiwango cha wastani.

Kama walimu wenyewe tunabeza elimu, ni dhahiri Taifa letu Lina safari ndefu sana kuliko hata matamanio yake.
 
Back
Top Bottom