Maaskovu Vs. Makamba na mgongano wa Arusha

Maaskovu Vs. Makamba na mgongano wa Arusha

Mimi nimesoma nikidhani imeandikwa na gazeti la maana kumbe Uhuru na mletaji mwenyewe akili mzunguko.

Napendekeza wanaoleta taarifa waanze na source kwanza halafu habari ndio ifuate, hii itasaidia kutokupotezeana muda, sisi wengine hatutumii computer za bure au atufanyi biashara ya internet cafe, tunanunuwa bundle ndio tunalog in, kutuletea source za gazeti la uhuru hapa ni sawa na mtu kutukosea adabu. nina hakika huyo bwana alieleta hii habari akili zake ni sawa tu na shake well before use. PERIOD.
 
We bluetooth ni wale wale,nashangaa sana jina lako,anyway ngoja nimsaidie huyu mzee ni hivi makamba,mamlaka tunayopaswa kutii ni ile tu itokanayo na Mungu,je mamlaka ya polisi kupiga marufuku maandamano ya amani kwa maelekezo yako wewe ni mamlaka halali?hapa ndipo maaskofu wanaposema uelewa wako juu ya biblia ni finyu,,kwa mujibu wa katiba ya Tanzania mamlaka zote zinatokana na wananchi,maana yake ni moja tu wananchi wana mamlaka na haki kikatiba kuandamana na kutoa hisia na mawazo yao,je polisi ina mamlaka gani kikatiba au kimungu kuzuia sauti ya wengi ambayo ni sauti ya Mungu?

mkuu... naona unachanganya mambo.. mara bluetooth .mara makamba... which is which now...reply with relevance.... au haufuatilii threads ..unakurupuka tuu
 
We bluetooth ni wale wale,nashangaa sana jina lako,anyway ngoja nimsaidie huyu mzee ni hivi makamba,mamlaka tunayopaswa kutii ni ile tu itokanayo na Mungu,je mamlaka ya polisi kupiga marufuku maandamano ya amani kwa maelekezo yako wewe ni mamlaka halali?hapa ndipo maaskofu wanaposema uelewa wako juu ya biblia ni finyu,,kwa mujibu wa katiba ya Tanzania mamlaka zote zinatokana na wananchi,maana yake ni moja tu wananchi wana mamlaka na haki kikatiba kuandamana na kutoa hisia na mawazo yao,je polisi ina mamlaka gani kikatiba au kimungu kuzuia sauti ya wengi ambayo ni sauti ya Mungu?

Sio hilo tu la polisi kuwapiga raia wema,,ila ambayo imeingia madarakani kwa kuchakachua inatoka kwa Mungu? je Mungu ana'support' uchakachuaji?...Huyu dingi ni muhuni tu..
 
Nna uhakika Makamba anaielewa Biblia kuliko huyo Askofu.
 
Safi sana makamba huyu Askofu Laizer ametumwa mfikishie ujumbe huko kwa wana Chadema wenzie na wapambe wa Lowassa.

Ww akiliza zako zikiwa ni za kushikiwa so unafikiri kila mtu yuko hivyo. Hapa hata mwanafunzi wa std one anaufahamu mzuri kuliko wako ktk ku-analyze mambo. Ww utaishia hivyo hivyo kutumwa.
 
Makamba, you have got unsound mind. Nadhani akili yake uwezi tofautisha na mtoto mdogo. Makamba wewe ndio unaevuruga nchi, mbona huoni UDOM, NA MBARALI.
 
This is getting interesting. Luteni Makamba strike back on Maaskofu.

NA JANE MIHANJI
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yussuf Makamba amesema kauli aliyoitoa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Arusha Thomas Laizer kumshutumu, inaashiria kuwa ni shabiki wa CHADEMA. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Makamba alielezea kusikitishwa kwake na habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi katika toleo la jana ikimnukuu askofu huyo akisema kuwa Makamba ana uelewa finyu wa Biblia. "Nilikuwa nazungumzia maandamano na ghasia zilizofanywa na CHADEMA kwa kunukuu Biblia, sasa hakunieleza au kunielimisha wapi niliikosea biblia," alisema Makamba. Aliongeza: "Nilihojiwa na TBC One na nikanukuu Warumi 13: 1-7, nilizungumzia CHADEMA, sikuwa nazungumza na askofu... sasa naona anayejibu hili ni shabiki wa CHADEMA," alisema. Katibu Mkuu huyo alisema anaendelea kuamini kwamba viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakutii mamlaka halali ambayo ni serikali. Alisema kwa kunukuu kwake mistari ya biblia hakuwa amekosea kama Askofu Laizer anavyodhani. "Kwa kweli nisingependa kulumbana na wakubwa, lakini wanapaswa kuelekeza pale wanapoona mtu amekosea, siyo kumlaumu," alisema.
"Ni kweli nina uelewa mdogo wa Biblia, kwa sababu mimi si askofu, ni muumini wa dini tena Mwislamu. Mazungumzo yangu na waandishi wa TBC One nilinukuu Biblia, Warumi sura ya 13, mstari wa 1-7," alisema Makamba.
Alibainisha kuwa inawezekana uelewa wake katika kifungu hicho ni mdogo, hivyo hapaswi kulaumiwa, bali kuelimishwa kwamba mamlaka iliyotajwa katika mistari hiyo ni ipi?
Makamba alirudia kusoma mistari hiyo isemayo: "Kila mtu na atii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo imeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu, nao washindanao watajipatia hukumu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake, kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema.
Lakini ufanyapo mabaya, ogopa kwa maana hauchukui upanga bure, kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu. Amlipizae kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu kwa hiyo ni lazima utii si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila kwa sababu ya dhamiri.
Kwa sababu hiyo na walipa kodi kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyo hiyo. Wapeni wote haki zao, mtu wa kodi, kodi, mtu wa ushuru, ushuru, astahiliye hofu, hofu, astahiliye heshima heshima."
Makamba alisema ni vyema akaelezwa uelewa wake finyu katika mistari hiyo, kuliko askofu kutaka kumnyamazisha na kuingia katika ushabiki wa kisiasa.

Source: UHURU

Askofu Laizer anaitwa Bibi Kiboga!
 
Sio hilo tu la polisi kuwapiga raia wema,,ila ambayo imeingia madarakani kwa kuchakachua inatoka kwa Mungu? je Mungu ana'support' uchakachuaji?...Huyu dingi ni muhuni tu..

Ndiyo! Mungu wa Biblia anasupoti uchakachuaji.
Chakachuo namba 1: YAKOBO ANAMNYANG'ANYA ESAU KWA HILA HAKI YA MZALIWA WA KWANZA. ISAKA ANAMBARIKI NA MUNGU ANAONA.
Chakachuo namba 2: MUNGU ANAPIGANA MIELEKA NA YAKOBO NA YAKOBO ANAMVUNJA PAJA MUNGU. MUNGU ANALIA NA KUOMBA YAKOBO AMUACHIA KWAMAANA KUNAPAMBAZUKA. YAKOBO ANAOMBA KUBARIKIWA NA MUNGU ANAFANYA HIVYO, YAKOBO ANAMWACHIA.

Ningeendelea lakini nachelea Shoga Laizer asinibwatukie. Hivi sio huyu aliyempokea E. Lowasa kwa heshima zote kama Mfalme?? Nimesahau mtaniswamehe!!
 
Chonde chonde wana chadema. someni alama za nyakati. Kama nilivyowahi kusema huko nyuma chadema wametengeneza uadui na mamlaka inayotawala kwa hiyo wasitarajie mteremko katika mambo yao. Inapofikia unasusa hata sherehe za UHURU wa nchi yetu basi jua matokeo ya baadaye na ujiandae vilivyo.

Msitarajie kuwa watakaokufa na kuumia kwa sababu ya propaganda zenu za kuingia IKULU kwa nguvu ni raia wasio na hatia pekee bali hata viongozi , watoto ,wake na au mahawara wao pia yatawapata madhara. Kuweni waangalifu sana na mtii amri/ushauri wa mamlaka inayotawala. Kama kuna mambo hayaendi sawa basi tumieni njia za kistaarabu pamoja na kwenda mahakamani kudai haki. Nabii SULEIMAN alisifika kwa HEKIMA na sio VISASI NA KUSUSA kike kike.

Chonde chonde, japo tunajua wazi kuwa KANISA lipo nyuma yenu lakini Watanzania wapenda AMANI hatuko tayari kuona kikundi kidogo kikiharibu usalama na amani ya nchi yetu.

Siku ikifika hayo mahekalu na madhabahu wanayojifichia yatageuka kuwa ndiyo makaburi yenu na yao pia. Rwanda sio mbali na 1994 sio mbali pia. Mtakumbuka kuwa maiti nyingi zilikutwa Makanisani. Tugeuke nyuma na tuangalie wapi tumejikwaa. Akili za kuambiwa changanya na zako!

Naandika haya nikichelea kuwa pasije kusemwa: "HAPAKUWEPO WENYE HEKIMA NDIO MAANA TUMEANGAMIA".
 
Hawa maaskofu bado wajinga wanaishi dunia gani ? Maaskofu haohao wanatumia bibilia kuruhusu ushoga! hivi wanfikiri bibilia ni mali yao ? No wonderr watalawitiana sana kwa sababu za ujinga wao
 
Maaskofu wa madhehebu ya Kikristu mkoani Arusha wamemkemea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, kwa kuitumia Biblia takatifu kuhalalisha uovu; wakamtaka aache tabia hiyo mara moja.

Maaskofu hao wakiongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer, aliyezungumza kwa niaba wenzake katika mazishi ya wahanga wa maandamano ya Arusha, alisisitiza kwamba wataendelea “kuikosoa serikali na chama chochote kile pindi kinapokosea.”

Kauli ya Makamba iliyowakera maaskofu hao, na ambayo amekuwa akiirudia mara kwa mara, ni ile aliyotumia kuwakejeli kwa kunukuu maandiko matakatifu ya Kurani na Biblia akisema “tiini mamlaka iliyo kuu.” Walisema ufahamu wa Makamba ni finyu katika kutafsiri maana halisi ya neno hilo.

“Kama serikali wameamua kutuvunjia heshima, basi wasimame kwenye majukwaaa kutetea uovu wao, na sisi tutasimama kwa ajili ya kupinga uovu wao, tuone Mungu atamsikia nani” alisema Askofu Laizer.

''Maaskofu wamesikitishwa na kauli yake na pia kauli ya Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwataka kuvua majoho na kuingia katika siasa kwani ni kuwavunjia heshima,'' alisema askofu Laizer.

Source: Tanzania Daima

Uliokuwa mgogoro kati ya SERIKALI na CHADEMA sasa umegeuka sura na kuwa Mgogoro kati ya KANISA na SERIKALI. Ni wapi wapi upepo ulibadilika, taarifa sina. Ama ni jambo lililojitokeza kwa bahati mbaya tu kama mtu kujikwaa au ndio swala lililopangwa vizuri sana bado ni kitendawili.

Moja ninalolielewa ni kwamba, katika hotuba zake mbili (kufungua Bunge na mpya) Rais Jakaya Kikwete alionya juu ya kushamili kwa udini katika kampeni na alivitaka vyama na watu binafsi kuacha mara moja tabia hiyo na kuendeleza kuwaunganisha wananchi. Ni vigumu kwa upande wangu kuunganisha moja kwa moja kati ya hotuba hiyo na sakata linaloendelea hivi sasa kati ya Askofu Laiser na serikali.

Kama serikali ndio inakiandama chama kinachojihusisha na udini na viongozi wa dini walionyuma yao, hiyo inaweza kuwa scenario No 1. Na kama hivyo ndivyo basi sioni kosa kwani madhara ya kueneza udini katiika siasa ni makubwa sana kuliko haya yanayotokea.

Scenario ya pili ni tukio la bahati mbaya, kama hili ni kweli basi watanzania tutulie na tujue kuwa tatizo halijaenea kama kansa Tanzania nzima na hivyo ni rahisi kulitatua, tena kwa muda mfupi.

Katika hali yeyote ile CHADEMA wanajibu ya maswala haya, na ni vyema watueleze ni nini muungano wa matatizo haya ya kisiasa kuingililiwa na makanisa. Hivi nchi imegawanyika?

Ni CHADEMA inafanya kazi ya kuwakomboa wananchi au kulikomboa Kanisa. CHADEMA lazima iamue moja kama inaelewa inachokitaka wananchi au dini. Sisi wazalendo bado hatuelewi kinachoendelea ndio maana tuningia ulingoni kuomba maelezo ya kina.
 
Nakupa mmoja ukamtafute yupo msikiti opposite na Chuo cha biashara (CBE) anavaa miwani mikubwa na anasalisha hapo ni imam pale ana PhD ya sharia laws ameipa Al-Azhar University. Hajiiti Dr kama Madr wenu wa Divinity na ukimwita hivyo hapendi ila watu hutoka pembe mbali mbali za dunia kumfata kwa ushauri.
kujiita Dr hata Slaa alipokuwa padre hakuwa anatumia title ya Dr hata Pope wa wakatoliki ni Professor wa Theology na haitumii hiyo title sasa sijui wapi hao wanaojitangaza na title zao though kama wana-deal na issues on their professions (e.g. academics et al) wanapaswa kutumia hizo title kiutaratibu
 
KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, amesema kuwa na uelewa finyu wa biblia si jambo la ajabu kwake kwa sababu yeye siyo askofu.

Makamba aliliambia Mwananchi jana kwa simu, kuwa licha ya uelewa finyu wa biblia, lakini amekuwa akitoa vifungu hivyo kwenye biblia.
Makamba alisema hayo kufuatia, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Thomas Laizer kusema Makamba ana uelewa finyu wa biblia.

Laizer alisema hayo juzi mjini Arusha wakati wa kuwaaga watu wawili waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi katika maandamano na Chadema yaliyofanyika Januari 5 mwaka huu.

“ Ni kweli ninauelewa finyu wa biblia kwa sababu mimi siyo askofu, hata Qurani naweza kuwa siifahamu vizuri kwa sababu mimi siyo Sheikh, ndiyo maana kila ninachozungumza kuhusu dini hizo nakariri vifungu kutoka katika vitabu hivyo,” alisema. Makamba alisema alimweleza Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutoandamana kwa sababu serikali ilipiga marufuku maandamano hayo, wao wakapuuza.

Alimtaka Laizer kutoa tafsiri ya kitabu cha Warumi 13 sehemu ya kwanza hadi ya saba, inayosema kuwa kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.
Alisema kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala anapinga chombo kilichowekwa na Mungu na watu wanaoasi hujiletea hukumu.

“ Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu, kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka basi tenda mema naye atakusifu,” alisema.

“ Laizer anieleze ufinyu wangu katika uelewa wa biblia upo wapi ikilinganisha na tukio lililotokea mkoani Arusha,” alisema.
 
Makamba amjibu Askofu Laizer Send to a friend KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, amesema kuwa na uelewa finyu wa biblia si jambo la ajabu kwake kwa sababu yeye siyo askofu.

Makamba aliliambia Mwananchi jana kwa simu, kuwa licha ya uelewa finyu wa biblia, lakini amekuwa akitoa vifungu hivyo kwenye biblia.
Makamba alisema hayo kufuatia, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Thomas Laizer kusema Makamba ana uelewa finyu wa biblia.

Laizer alisema hayo juzi mjini Arusha wakati wa kuwaaga watu wawili waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi katika maandamano na Chadema yaliyofanyika Januari 5 mwaka huu.

“ Ni kweli ninauelewa finyu wa biblia kwa sababu mimi siyo askofu, hata Qurani naweza kuwa siifahamu vizuri kwa sababu mimi siyo Sheikh, ndiyo maana kila ninachozungumza kuhusu dini hizo nakariri vifungu kutoka katika vitabu hivyo,” alisema. Makamba alisema alimweleza Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutoandamana kwa sababu serikali ilipiga marufuku maandamano hayo, wao wakapuuza.

Alimtaka Laizer kutoa tafsiri ya kitabu cha Warumi 13 sehemu ya kwanza hadi ya saba, inayosema kuwa kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.
Alisema kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala anapinga chombo kilichowekwa na Mungu na watu wanaoasi hujiletea hukumu.

“ Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu, kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka basi tenda mema naye atakusifu,” alisema.

“ Laizer anieleze ufinyu wangu katika uelewa wa biblia upo wapi ikilinganisha na tukio lililotokea mkoani Arusha
 
Makamba anadhani Biblia ni kitabu cha 'kimwili'. Akili yake ndiyo imegoti hapo. Pole sana mzee. Sikulaumu sana maana ndiyo tabia ya wadogo zetu ya kubeba vifungu vya Biblia kichwakichwa na kutamka kwenye majukwaa ili kukidhi matakwa yao.

Ninachopenda wadogo zetu wajue ni kwamba Mungu wetu ni roho na wanaomwabudu lazima wamwabudu katika roho na kweli, unaposoma neno la Mungu na akili yako ya kimwili usitarajie kupata kitu.
 
Send to a friend

Back
Top Bottom