Maaskovu Vs. Makamba na mgongano wa Arusha

This is getting interesting. Luteni Makamba strike back on Maaskofu.

NA JANE MIHANJI
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yussuf Makamba amesema kauli aliyoitoa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Arusha Thomas Laizer kumshutumu, inaashiria kuwa ni shabiki wa CHADEMA. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Makamba alielezea kusikitishwa kwake na habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi katika toleo la jana ikimnukuu askofu huyo akisema kuwa Makamba ana uelewa finyu wa Biblia. "Nilikuwa nazungumzia maandamano na ghasia zilizofanywa na CHADEMA kwa kunukuu Biblia, sasa hakunieleza au kunielimisha wapi niliikosea biblia," alisema Makamba. Aliongeza: "Nilihojiwa na TBC One na nikanukuu Warumi 13: 1-7, nilizungumzia CHADEMA, sikuwa nazungumza na askofu... sasa naona anayejibu hili ni shabiki wa CHADEMA," alisema. Katibu Mkuu huyo alisema anaendelea kuamini kwamba viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakutii mamlaka halali ambayo ni serikali. Alisema kwa kunukuu kwake mistari ya biblia hakuwa amekosea kama Askofu Laizer anavyodhani. "Kwa kweli nisingependa kulumbana na wakubwa, lakini wanapaswa kuelekeza pale wanapoona mtu amekosea, siyo kumlaumu," alisema.
"Ni kweli nina uelewa mdogo wa Biblia, kwa sababu mimi si askofu, ni muumini wa dini tena Mwislamu. Mazungumzo yangu na waandishi wa TBC One nilinukuu Biblia, Warumi sura ya 13, mstari wa 1-7," alisema Makamba.
Alibainisha kuwa inawezekana uelewa wake katika kifungu hicho ni mdogo, hivyo hapaswi kulaumiwa, bali kuelimishwa kwamba mamlaka iliyotajwa katika mistari hiyo ni ipi?
Makamba alirudia kusoma mistari hiyo isemayo: "Kila mtu na atii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo imeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu, nao washindanao watajipatia hukumu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake, kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema.
Lakini ufanyapo mabaya, ogopa kwa maana hauchukui upanga bure, kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu. Amlipizae kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu kwa hiyo ni lazima utii si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila kwa sababu ya dhamiri.
Kwa sababu hiyo na walipa kodi kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyo hiyo. Wapeni wote haki zao, mtu wa kodi, kodi, mtu wa ushuru, ushuru, astahiliye hofu, hofu, astahiliye heshima heshima."
Makamba alisema ni vyema akaelezwa uelewa wake finyu katika mistari hiyo, kuliko askofu kutaka kumnyamazisha na kuingia katika ushabiki wa kisiasa.

Source: UHURU
 
wholly Crap

If you can't read any newspaper (Uhuru/TZDaima) and make up your own independent conclusion, then you are intellectually challenged. Which sadly represent the majority of Jamii Forumers. Mnaendeshwa endeshwa tu na kina Saeed Kubenea.
 
your moral integrity is disqualified by your shallow judgment ..... stop pretending.... i will never pay my dam cash to a hate preaching daily tabloid... Uhuru
 
1.Nikisikia Jina la huyu babu jinga huwa mood yote inaharibika
2.Huwa anakera sana anapojaribu kuwapotosha watanzania na vifungu viwili vitatu anavyovijua kutoka kwenye biblia kwa kuchanganya na siasa zao chafu na za kidhalimu, huku wakisema watu wasichanganye siasa na dini
3.Askofu kusema Makamba ana uelewa finyu wa biblia je kunamfanya askofu huyo kuwa shabiki wa Chadema, wakati ni obvious makamba haijui biblia hata kidogo
4,Nashauri umoja wa makanisa Tanzania utoe kauli ya kumpinga Makamba kutumia kitabu kitakatifu asichokielewa hata chembe kueneza propanga za chama kilichoshindwa kumtoa mtanzania kwenye dimbwi la umaskini.
 
Mimi nimesoma nikidhani imeandikwa na gazeti la maana kumbe Uhuru na mletaji mwenyewe akili mzunguko.
 
We bluetooth ni wale wale,nashangaa sana jina lako,anyway ngoja nimsaidie huyu mzee ni hivi makamba,mamlaka tunayopaswa kutii ni ile tu itokanayo na Mungu,je mamlaka ya polisi kupiga marufuku maandamano ya amani kwa maelekezo yako wewe ni mamlaka halali?hapa ndipo maaskofu wanaposema uelewa wako juu ya biblia ni finyu,,kwa mujibu wa katiba ya Tanzania mamlaka zote zinatokana na wananchi,maana yake ni moja tu wananchi wana mamlaka na haki kikatiba kuandamana na kutoa hisia na mawazo yao,je polisi ina mamlaka gani kikatiba au kimungu kuzuia sauti ya wengi ambayo ni sauti ya Mungu?
 
This is getting interesting. Luteni Makamba strike back on Maaskofu.

NA JANE MIHANJI
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yussuf Makamba amesema kauli aliyoitoa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Arusha Thomas Laizer kumshutumu, inaashiria kuwa ni shabiki wa CHADEMA. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Makamba alielezea kusikitishwa kwake na habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi katika toleo la jana ikimnukuu askofu huyo akisema kuwa Makamba ana uelewa finyu wa Biblia. "Nilikuwa nazungumzia maandamano na ghasia zilizofanywa na CHADEMA kwa kunukuu Biblia, sasa hakunieleza au kunielimisha wapi niliikosea biblia," alisema Makamba. Aliongeza: "Nilihojiwa na TBC One na nikanukuu Warumi 13: 1-7, nilizungumzia CHADEMA, sikuwa nazungumza na askofu... sasa naona anayejibu hili ni shabiki wa CHADEMA," alisema. Katibu Mkuu huyo alisema anaendelea kuamini kwamba viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakutii mamlaka halali ambayo ni serikali. Alisema kwa kunukuu kwake mistari ya biblia hakuwa amekosea kama Askofu Laizer anavyodhani. "Kwa kweli nisingependa kulumbana na wakubwa, lakini wanapaswa kuelekeza pale wanapoona mtu amekosea, siyo kumlaumu," alisema.
"Ni kweli nina uelewa mdogo wa Biblia, kwa sababu mimi si askofu, ni muumini wa dini tena Mwislamu. Mazungumzo yangu na waandishi wa TBC One nilinukuu Biblia, Warumi sura ya 13, mstari wa 1-7," alisema Makamba.
Alibainisha kuwa inawezekana uelewa wake katika kifungu hicho ni mdogo, hivyo hapaswi kulaumiwa, bali kuelimishwa kwamba mamlaka iliyotajwa katika mistari hiyo ni ipi?
Makamba alirudia kusoma mistari hiyo isemayo: "Kila mtu na atii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo imeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu, nao washindanao watajipatia hukumu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake, kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema.
Lakini ufanyapo mabaya, ogopa kwa maana hauchukui upanga bure, kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu. Amlipizae kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu kwa hiyo ni lazima utii si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila kwa sababu ya dhamiri.
Kwa sababu hiyo na walipa kodi kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyo hiyo. Wapeni wote haki zao, mtu wa kodi, kodi, mtu wa ushuru, ushuru, astahiliye hofu, hofu, astahiliye heshima heshima."
Makamba alisema ni vyema akaelezwa uelewa wake finyu katika mistari hiyo, kuliko askofu kutaka kumnyamazisha na kuingia katika ushabiki wa kisiasa.

Source: UHURU

kumbe yupo!!!!!,hana tofauti na zimwi!!!
 
Asijifanye kuwa mpole wa kutaka kujifunza kutoka kwa maaskofu leo hii, baada ya kukaliwa kooni ndani ya ccm na kutishiwa kung'olewa...Sifa kuu ya Mikamba ni uchochezi, uropokaji, na ujuaji,..Mtu gan usiyeshaurika na weng? ..au tafsiri ya ukatibu wa chama ni kukosa busara na usikivu?..Na jee angekaa kimya kungeharibika nini?...AIBU!
 
Jamani Uhuru ni gazeti gani??? kumbe bado lipo?

Makamba asibwatuke hovyo sio Watanzania wote wasiosoma, Kuna watu na elimu zao> anajidhalilisha. Bora afunge mdomo kuliko kujibu hoja za watu wa Mungu.Tena asiwatishe awaache wafanye kazi zao kwa uhuru.
 
haya kazi hiyo pevu kabisa, kila nayejua kusoma na kuandika anweza kufafanua biblia! tutafika tu lakini, Mungu yupo
 
Uelewa mdogo wa makamba haupo kwenye mistari ya Biblia, bali upo kwenye matumizi ya biblia coz anataka kutumia mistari ya Biblia kuhalarisha vitendo vya kishetani vinavyofanywa na baba yake, JK.
 
Kweli sasa CCM imeparaganyika, where is the leadership??????
 
This is getting interesting. Luteni Makamba strike back on Maaskofu.

NA JANE MIHANJI
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yussuf Makamba amesema kauli aliyoitoa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Arusha Thomas Laizer kumshutumu, inaashiria kuwa ni shabiki wa CHADEMA. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Makamba alielezea kusikitishwa kwake na habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi katika toleo la jana ikimnukuu askofu huyo akisema kuwa Makamba ana uelewa finyu wa Biblia. "Nilikuwa nazungumzia maandamano na ghasia zilizofanywa na CHADEMA kwa kunukuu Biblia, sasa hakunieleza au kunielimisha wapi niliikosea biblia," alisema Makamba. Aliongeza: "Nilihojiwa na TBC One na nikanukuu Warumi 13: 1-7, nilizungumzia CHADEMA, sikuwa nazungumza na askofu... sasa naona anayejibu hili ni shabiki wa CHADEMA," alisema. Katibu Mkuu huyo alisema anaendelea kuamini kwamba viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakutii mamlaka halali ambayo ni serikali. Alisema kwa kunukuu kwake mistari ya biblia hakuwa amekosea kama Askofu Laizer anavyodhani. "Kwa kweli nisingependa kulumbana na wakubwa, lakini wanapaswa kuelekeza pale wanapoona mtu amekosea, siyo kumlaumu," alisema.
"Ni kweli nina uelewa mdogo wa Biblia, kwa sababu mimi si askofu, ni muumini wa dini tena Mwislamu. Mazungumzo yangu na waandishi wa TBC One nilinukuu Biblia, Warumi sura ya 13, mstari wa 1-7," alisema Makamba.
Alibainisha kuwa inawezekana uelewa wake katika kifungu hicho ni mdogo, hivyo hapaswi kulaumiwa, bali kuelimishwa kwamba mamlaka iliyotajwa katika mistari hiyo ni ipi?
Makamba alirudia kusoma mistari hiyo isemayo: "Kila mtu na atii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo imeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu, nao washindanao watajipatia hukumu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake, kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema.
Lakini ufanyapo mabaya, ogopa kwa maana hauchukui upanga bure, kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu. Amlipizae kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu kwa hiyo ni lazima utii si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila kwa sababu ya dhamiri.
Kwa sababu hiyo na walipa kodi kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyo hiyo. Wapeni wote haki zao, mtu wa kodi, kodi, mtu wa ushuru, ushuru, astahiliye hofu, hofu, astahiliye heshima heshima."
Makamba alisema ni vyema akaelezwa uelewa wake finyu katika mistari hiyo, kuliko askofu kutaka kumnyamazisha na kuingia katika ushabiki wa kisiasa.

Source: UHURU

Safi sana makamba huyu Askofu Laizer ametumwa mfikishie ujumbe huko kwa wana Chadema wenzie na wapambe wa Lowassa.
 
Mi naomba aanze kutumia quran si kitabu kitakatifu, Biblia. Yeye anafikiri ananukuu vifungu vya katiba. Bible is a revelation, so somebody to understand this holy book, need to be full of Holy spirit. Makamba knows nothing about it. Let us pray for him.
 
Makamba hajui kwamba mamlaka inayoongelewa katika Biblia ni hile ambayo imeingie kwa uhalali na kuchaguliwa na watu kwa haki. Mamlaka tuliyonayo Tanzania haikuwekwa kwa haki. Ni mamlaka ya kuchakachua kura, kwa hiyo ni dhambi kubwa kwa wananchi na maaskofu kama viongozi wa dini kutii mamlaka ambayo haipo kihalali.
 
Makamba kwanini unanukuu Biblia? Nchi inaendeshwa kwa Biblia? Waachie maaskofu na
biblia yao. kama wewe ni Mwislamu tumia Qurani lakini katika mazingira yanayoruhusu kujadili imani yako siyo yahusuyo siasa. Chonde chonde Makamba achana na Biblia.

Hata kama umedoeadoea kwenye shule za misioni lakini si suala mufaka kwako kutumia Biblia kujadili hoja za kisiasa kwani utaamsha hasira za wenye imani katika vitabu hivyo. Kwa wale wanaofahamu vizuri Biblia kunukuu mstari mmoja tu bila kusoma pamoja na mistari mingine na wala kupata ufafanuzi kama exegesis haina maana yoyote.

Hivyo Makamba usihangaike kutaka ufafanuzi juu ya vifungo ulivyonukuu. Wala siyo muafaka kubishana na Makamba kuhusu vifungo alivyovisema bali turejee katiba, sheria na kanuni kuhusu suala husika. Ninasema hivyo kwa sababu siku moja mtu mwingine atatuletea kifungo cha Biblia ambacho kitaudhi viongozi wa serikali na hatimaye tutaanza kulaumiana kwamba watu wanaleta udini. kama sasa tunacheka kwa sabau maneno aliyoyatamka yanatupendeza tusije kulaumiana siku nyingine tukianza kusikia yasiyotupendeza. Kumbuka baadhi ya viongozi wa dini waliwahi kutamka kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu na wala hakuna aliyemlaumu kwasababu imempendeza JK. Siku nyingine mwingine akisema Jk siye chaguo la Mungu atalaumiwa. Mwingine tena akasema anamwongezea rais ulinzi na serikali ikasema ni maoni binafsi ya mtu. kutoka upande wa serikali hakuna aliyesema kwamba matamshi hayo yana walakini. Je huyo nani kampa kazi hiyo ya ulinzi? siku akisema nitaondoa ulinzi nani atamlaumu na atakuwa amemtendea haki?
 
Kulingana na mstari huo aliousoma , kwa maoni yangu ni kwamba Makamba anatumia biblia kuidhinisha mauaji ya raia, kwamba watii Nguvu kuu japokuwa wanaishi kama watumwa ndani ya nchi yao, hili ni jambo la kukemewa na Makamba inatakiwa aadabishwe.
 
Back
Top Bottom