Maaskofu Katoliki walivyolaani mauaji Pemba 2001

Sidhani kama bandiko hilo linawakaanga maskofu hata kidogo, hata kama hawakutumia lugha kali kama ambavyo tungependa iwe hivyo...hivi kweli mngetegemea hao maaskofu watamke kuwa hawamtambui Komandoo Salmin Amour ndio turidhike kuwa wametoa tamko kali???

Ukilinganisha na kichwa cha thread hii, bandiko haliendani na kichwa hicho. Kuna tofauti kati ya neno "Kulaani" na "Kusikitika" au "Kuonyesha masikitiko". Kwa hali ya kawaida mtu yoyote yule husikitika pale tukio baya kama ghasia na vifo vinapotokea na kusikitika huku kutokana na kuguswa na madhara ya tukio kama hilo. Kulaani ni kupinga kwa nguvu zote na katika tukio kama hilo mtu wa kawaida hulaani yule aliyesababisha masahibu hayo iadha kwa kutoa amri ya kudhuru au kudhuru.

Either way, it will be interesting to revisit what was said on Feb the 8th, 2001. Unajua tatizo la imani linaamsha hisia sana kwa baadhi yetu na ni lazima tukubali kwamba kuna baadhi bado wanafeel aggrieved kutokana na kuona kwamba wenzao hawakuwasupport vya kutosha pindi walipowahitaji.

Mkuu umeibua a very interesting point, je siku ikitokea viongozi fulani wa dini fulani wakasema hawamtambui rais na wenzao wa dini nyingine wakawapinga itakuwaje especially in light ya haya matatizo ya Arusha?

Tisa kumi, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hata katika kudai haki au kupinga perceived injustice. Hivi hawa viongozi wa dini za Abrahamu walishindwa kuwasiliana, kuketi na kutoa tamko la pamoja kuhusiana na kule Arusha au Zanzibar kabla ya hapo? Siku hizi kuna njia nyingi tu za mawasiliano na isitoshe Arusha mjini ni eneo dogo. Wangeweza kuepusha malumbano yote haya ya sasa hivi kwa kufanya hivi.

Ndiyo maana narejea ujumbe wangu wa awali, viongozi wa dini za Abrahamu warudi kwenye nyumba zao za ibada waziombee amani nafsi zao,zetu na taifa kwa ujumla. Na pia wasisahau kuomba tuepushwe na dhambi ya ubaguzi ambayo inawezekana pasi kukusudia wamezileta.
 
Hakuna atakayetumbembeleza mkuu, sisi tutaendelea tu kupambana iwe mnafurahi au mnachuki ndiyo maana inaitwa dunia uwanja wa mapambano ahera mapumziko ok...

Maaskofu unafiki wao umeshikwa umejulikana wanatapatapa
Unapambana na nani.
 
hitimisho;

a) Maaskofu walitoa tamko mwaka 2001.

b) Tamko hilo lilikemea kilichotokea.

Hoja ilikuwa maaskofu hakukemea. Safari hii wamekemea. Sasa hoja ya nyongeza ni kwa nini hawakukemea vikali. Sidhani kama hoja ya nyongeza ina mshiko kwa sasa. Cha msingi walikemea na wakshauri. Serikali haikusikiliza ushauri wao kwa hiyo safari hii wameikemea zaidi. Hata kama walikuwa upande wa serikali then basi kwa kitendo hicho kurudiwa wana kila sababu ya kutoitetea serikali zaidi. Tusubiri kama CUF watapigwa tena tuone kama maaskofu wataitea serikali. Lakini CUF na wao wapigwe kwa kuonewa sio wafanye ukaidi ili wapigwe wategemee kutetewa na maaskofu na watu wengine! Waandamane kuhusu Dowans tujiunge nao. Wakipigwa na maaskofu wakikaa kimya ukweli utajulikana!
Tusitake kuzunguka vichakani, Maaskofu waliotoa tamko ni wa Arusha, wao ndio wanaoijua Arusha, suala la mwaka 2001 lilitokea Pemba, sina hakika kama Pemba kuna maaskofu wa kuweza kupaza sauti zikasikika. Cha zaidi ni kwamba mwaka 2001 maaskofu hawakupingana na Mashehe, cha ajabu mwaka huu waislam wamewapinga maaskofu waziwazi, simply because Rais ni mwislam, mimi nikiwa muislam, rais mwislam ana msaada gani kama hali ya uchumi ni mbovu? Tuache kufikiria kwa makalio!
 
Poa sana mkuu tatizo la arusha lilikuwa la kisiasa ambapo kila mtu wakiwemo maaskofu kama raia wa tz wanahaki ya kutoa maoni yao, tatizo ni kuwa jamaa wamelitoa katika siasa na kuingia katika dini. Ni ufinyu na uzembe wa kufikiri na kuyatanguliza maslahi ya tz mbele!
 
Hapa napata picha nyingine, waislam wanataka kuwa remote controller wa maaskofu na wakristu. Hayo mnayotaka yatamkwe kwa ajili ya pemba arusha ama popote pale waambieni hao mashehe wafungue vinywa vyao watamke wenyewe, kwa nini kushiunikiza maaskofu kutamka ebo!
Au mnaogopa mtamwaga sumu,au sheikh makamba na yahya wameshasema? ACHENI KUDANDIA DANDIA KILA KITU MPAKA MATAMKO YA WENGINE.
 
Ukilinganisha na kichwa cha thread hii, bandiko haliendani na kichwa hicho. Kuna tofauti kati ya neno "Kulaani" na "Kusikitika" au "Kuonyesha masikitiko". Kwa hali ya kawaida mtu yoyote yule husikitika pale tukio baya kama ghasia na vifo vinapotokea na kusikitika huku kutokana na kuguswa na madhara ya tukio kama hilo. Kulaani ni kupinga kwa nguvu zote na katika tukio kama hilo mtu wa kawaida hulaani yule aliyesababisha masahibu hayo iadha kwa kutoa amri ya kudhuru au kudhuru.

Either way, it will be interesting to revisit what was said on Feb the 8th, 2001. Unajua tatizo la imani linaamsha hisia sana kwa baadhi yetu na ni lazima tukubali kwamba kuna baadhi bado wanafeel aggrieved kutokana na kuona kwamba wenzao hawakuwasupport vya kutosha pindi walipowahitaji.

Mkuu umeibua a very interesting point, je siku ikitokea viongozi fulani wa dini fulani wakasema hawamtambui rais na wenzao wa dini nyingine wakawapinga itakuwaje especially in light ya haya matatizo ya Arusha?

Tisa kumi, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hata katika kudai haki au kupinga perceived injustice. Hivi hawa viongozi wa dini za Abrahamu walishindwa kuwasiliana, kuketi na kutoa tamko la pamoja kuhusiana na kule Arusha au Zanzibar kabla ya hapo? Siku hizi kuna njia nyingi tu za mawasiliano na isitoshe Arusha mjini ni eneo dogo. Wangeweza kuepusha malumbano yote haya ya sasa hivi kwa kufanya hivi.

Ndiyo maana narejea ujumbe wangu wa awali, viongozi wa dini za Abrahamu warudi kwenye nyumba zao za ibada waziombee amani nafsi zao,zetu na taifa kwa ujumla. Na pia wasisahau kuomba tuepushwe na dhambi ya ubaguzi ambayo inawezekana pasi kukusudia wamezileta.

Bandiko hili limekuja baada ya maaskofu hawa wa Arusha kushutumiwa kwamba hawakutoa tamko lolote juu ya mauaji ya 2001, hawakushutumiwa kwa kutoa tamko laini... Hebu turudi mwaka 2001 tuone ni nani na nani waliotoa matamko ya kulaani mauaji yale kabla ya kuwahukumu viongozi hawa!

Tatizo ni kwamba wanaowashutumu maaskofu wanataka kutuaminisha kwamba wamelaani mauaji ya Arusha kwa maslahi ya kidini kitu ambacho si kweli hata kidogo.
 
Nashukuru mkuu kwa hii attachment. Nimeisoma na kuilewa na nadhani muda si mrefu tutapata ripoti kamili. Inasikitisha sana kuona mtu anasema maaskofu walikaa kimya!

Sasa ni wakati wa kutumia busara zaidi maana wanasiasa wanatafuta weak point ili iweze kuwabeba na kufunika maovu yao na tusipokuwa makini watatuingizia kwenye machafuko, wao na familia zao watakimbilia majuu kama Tunisia! Tusilalame tu kwenye vyombo vya habari, tutafakari juu ya maisha yetu kama watanzania wamoja na si kama waislamu, wakristu, wapagani, wahindu n.k. Suara la imani ni la kiroho zaidi na hapa duniani tunavyopigania sasa ni vya kimwili zaidi ili roho iweze kuendelea kuuishi ulimwenguni. Na ili roho iendelee kuuishi ulimwenguni mambo ya kimwili lazima yatimwize! Ni katika hili tunajikuta tukidai maisha bora ambayo wanasiasa wetu wamejisahau na kudhani wao tu kwa kukabidhiwa dhamana ya kutuongoza ndo pekee yao wanastahili maisha bora tu wakiacha tuliowengi tukitaabika. Kwa kuwa waliowengi sasa nao wanayatamani hayo maisha bora, wanapoyadai kwa umoja wao kama watanzania, wanasiasa wanatafuta njia ya kuwagawa! Kwa sasa kinachotusumbua sisi kama watanzania ni umasikini wetu ambao wanasiasa wameutumia sasa kama mradi!. Kama watanzania hatutofautiani kiumasikini awe mwislamu, awe mkristu kwa kuwa tunaishi katika jamii moja ya watanzaia. Matatizo ya kutowajibika kwa serikali zetu yanatugusa moja kwa moja kama watanzania kwa umoja wetu na si kama mkristu au mwislamu! Katika hili naamini wapo viongozi wa kidini watakaotumiwa vibaya na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi kuwatoa watanzania wamoja katika kudai mambo ya msingi na kuwaingiza katika chokochoko za kidini.

Swali la msingi ni je kama Tanzania ikiendelea ikawa kama ulaya ambako hata asiyefanya kazi anaripwa posho, nani wa kufaida kama si sisi watanzania kwa umoja wetu? Je rasi kuwa mkristu au mwislamu inatusaidia nini sisi kama watanzania wamoja tuishio katika jamii moja bila ya kuwajibika kwetu kama raia tuliiweka madarakani?
Tulengenge kujenga Tanzania moja ya watanzania wamoja wenye lengo la kuiona Tanzania ikijitegemea kiuchumi na wananchi wake wakinufaika na uchumi wa nchi yao bila kujali itikadi za imani zetu, na tujenge tabia ya kukemea uovu kwa dhati na si kushinikizwa kwa maslahi ya wanasiasa kama ilivyo sasa.
 
Kuanzia mwaka 2001 hadi sasa 2011 ni muda mrefu sana umepita na kuweza kusababisha mabadiliko makubwa ya mitazamo.

Lakini kwa upande wangu sidhani kama tamko liliegemea serikali kwa sababu waliouliwa walikuwa 'waislam'. Inawezekana ikawa kulikuwa na woga kwa wakati ule na kushindwa kupinga serikali moja kwa moja au sababu nyengine inayoweza kufikirika ni kuwa 'Zanzibar ni mbali, sawa na nchi jirani'.
Huwezi kutegemea tamko linalohusu mauaji mbele ya macho yako, na mauaji 'nchi jirani' kufanana.

Na nukuu hapa maneno ya tamko

Haya ni matatizo ya kusoma kitu ukiwa atayari na "prejudice"...soma kilichoandikwa.Acha kuweka mitazamo yako kwenye makala ambayo hujaandika wewe.Kilichoandikwa kwenye hiyo makala hakishaabiani kwa namna yeyote na unachoandika hapa.Tuachane ushabiki!
 
kwa mtindo huu wa wenzetu kukurupuka tutafika wapi jamani??? kama wamechoka na amani iliyopo wahamie Iraq au Somalia kutawafaa sana.
 
Umeshafanya uamuzi. Siwezi kukushawishi vinginevyo. Hata tamko la Maaskofu Katoliki kupitia Rais wa TEC lilikuwa laini kabisa kama hili. Nilimsikia akihojiwa BBC. Usisahau pia kuwa mmoja wa waliouwawa Arusha ni Mwislamu.
Yeah ni kweli, inaonesha mkuu Gaijin hapa kesha-conclude na ana hofu sana ya kuamini kua yaweza kuwa tofauti na anachopenda kuamini. Para ya 12 wanavitaka vyombo vya dola kutumia njia za kisasa kupambana na vurugu na kutumia utu katika kutekeleza majukumu yao. Hii in tofauti gani na yaliyosemwa juzi? Au Mkuu alitaka litolewe kwa JAZBA kidogo ndipo lionekane ni la dhati? Kwa bahati mbya ndivyo wanavyotoa matamko yao hawa jamaa,coz hawana political authority wao,...asset yao kubwa ni Moral authority inayowaruhusu kukemea maovu na si kutoa amri kwa serikali kama ambavyo mimi ningetamani iwe.Ikumbukwe pia hili lilikua tukio la kwanza kubwa la mauaji ya kisiasa kutokea tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uanze, Linavyojirudia Arusha,mtu concerned anaanza kuhofu kuwa tunarudi tena kule tulikotoka tena na anaona haja ya msingi kutoa tamko tena..What is wrong with this jamani,dini zetu aside?
 
Hapa kuna hoja, hoja ambayo imekuwa ikibebewa bango na CCM pamoja na apologist wake. Hoja hii imeanza hasa wakati wa Kampeni. Hoja yenyewe ni kuwa Mheshimiwa Kikwete anapingwa na wakristo kwa kuwa yeye ni Mwislam; na amekuwa akiongea wazi wazi kuwa uchaguzi huu umeacha makovu makubwa ya udini. Ndo maana kila move inayofanywa na watu wenye majina ya Kikristo dhidi ya serikali imeonekana kuwa ni matatizo ya dini ya Kikristo dhidi ya Kikwete kama Mwislam, na si kama rais.

Kuna hisia ambazo mheshimiwa Kikwete amekuwa akijaribu kuzipandikiza kuwa yeye ni rais anayetetea umoja wa watanzania wakati wengine wakimuona kama anayefanya "affirmative action" ya kuwapendelea waislam. Hili limekuwa likiranda randa hapa JF na kwenye media nyingi kwa sura mbali mbali.

Yalipotokea ya Arusha Matamka ya viongozi wa Kikristo yametafsiriwa kuwa yamechagizwa na upinzani wa wakristo dhidi ya Mheshimiwa Kikwete kwa sababu ya dini yake! Hata media za serikali zikiakisi kile anachoamini kiongozi wao zimekuwa zikiifanya sana hii kazi. Wengi tunakumbuka jinsi ambavyo mgogoro wa wakatokiki (wenyewe kwa wenyewe) kule Sumbawanga umekuwa ukitumiwa sana na media za serikali kuonesha kuwa wakatoliki wale walifukuzwa kwa sababu ya kuwaunga mkono CCM na Kikwete. Jambo hili halijifichi kabisa!

Kuna wengi wamekuwa wakisema 2001 viongozi wa Kikristo hawakutoa matamko baada ya mauaji. Hata hivyo inaonekana kuwa matamko yalitolewa ingawa yanatofautiana kutokana na mazingira na wakati kutofautiana vile vile. Kuna matamko huwa yanatolewa kila wakati uchaguzi unapokaribia, na mwaka huu matamko hayo yalitolewa. Kama kawaida wako waliopinga kuwa matamko kama hayo hayakutolewa wakati wa chaguzi zilizowaingiza wakristo madarakani, ushahidi ulipoletwa bado watu walikataa kuwa matamko hayo hayakuwa makali kama ya wakati huu.

Wenye akili tunajiuliza, kwa nini mpasuko wa kidini umeonekana mwaka 2010? Kwa nini mpasuko haukuonekana mwaka 2005? Pengine mheshimiwa sana Rais Kikwete majibu anayo kwani ana vyombo vingi vya uchunguzi na uchambuzi chini yake. Haya mambo yanapokuzwa na watawala ndo inapokuwa tatizo kubwa hasa. Watawala dhaifu hutafuta mahala pa kujificha. Rejea kauli za mwalimu Nyerere kuwa Mtu akishafirisika kisiasa atatafuta namna ya kujihalalisha. Dini sasa hivi ndo kitu chepesi kutumia.

Ikumbukwe kuwa hizi kelele si kwamba huko nyuma zilikuwa hazipo! Zilikuwepo, ila serikali zote zilizotangulia, ziliyapuuza. Lakini serikali hii kupitia media zake, imejiingiza moja kwa moja na kuchukua side! hapa ndo kwenye tatizo kubwa. Serikali iliyokuwa inatakiwa kukemea haya mambo, ndo inayaendekeza. Ni jambo la aibu kabisa!
 
Yeah ni kweli, inaonesha mkuu Gaijin hapa kesha-conclude na ana hofu sana ya kuamini kua yaweza kuwa tofauti na anachopenda kuamini. Para ya 12 wanavitaka vyombo vya dola kutumia njia za kisasa kupambana na vurugu na kutumia utu katika kutekeleza majukumu yao. Hii in tofauti gani na yaliyosemwa juzi? Au Mkuu alitaka litolewe kwa JAZBA kidogo ndipo lionekane ni la dhati? Kwa bahati mbya ndivyo wanavyotoa matamko yao hawa jamaa,coz hawana political authority wao,...asset yao kubwa ni Moral authority inayowaruhusu kukemea maovu na si kutoa amri kwa serikali kama ambavyo mimi ningetamani iwe.Ikumbukwe pia hili lilikua tukio la kwanza kubwa la mauaji ya kisiasa kutokea tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uanze, Linavyojirudia Arusha,mtu concerned anaanza kuhofu kuwa tunarudi tena kule tulikotoka tena na anaona haja ya msingi kutoa tamko tena..What is wrong with this jamani,dini zetu aside?

Huwa sipendi kujirudia lakini kwa faida yako na wengine kama wewe wanaopata tabu kusoma Kiswahili wakaelewa mara moja msimamo wangu ni kuwa na ninanijinukuu

Kuanzia mwaka 2001 hadi sasa 2011 ni muda mrefu sana umepita na kuweza kusababisha mabadiliko makubwa ya mitazamo.

Lakini kwa upande wangu sidhani kama tamko liliegemea serikali kwa sababu waliouliwa walikuwa 'waislam'. Inawezekana ikawa kulikuwa na woga kwa wakati ule na kushindwa kupinga serikali moja kwa moja au sababu nyengine inayoweza kufikirika ni kuwa 'Zanzibar ni mbali, sawa na nchi jirani'.
Huwezi kutegemea tamko linalohusu mauaji mbele ya macho yako, na mauaji 'nchi jirani' kufanana.
 
Huwezi kusoma paragraph moja tu mkuu. The whole makala inaonyesha kuwa Tamko lilikuwa linaamini kuwa chama cha siasa kimesababisha vurugu na imewezekana hivyo kwa sababu 'vijana hawana kazi, umaskini, rahisi kughurubiwa, kukosa elimu ya uraia".

Hakuna walipokemea serikali. Na huwezi kulinganisha na tamko lililotolewa sasa. Hili lilikuwa tamko la kupinga vyama vya siasa.

Kuna para inasomeka hivi: "Maaskofu pia wametaka vyombo vya dola vielimishwe njia za kisasa za kukabiliana na vurugu na kuwa na utu katika kutekeleza majumu yao". Hii nayo unaionaje? Bado hujaona busara ya hawa viongozi wa dini? Come on... Isitoshe mazingira yanatofautiana sana kwa hiyo usitegemee tamko la maaskofu wakati ule baada ya mauaji ya Pemba liwe sawa na hili lililotokea sasa Arusha.
 
Kuna sehemu nilipopinga busara za hawa watu? Na kuna sehemu nimetegemea tamko la mauaji ya Pemba liwe sawa na Arusha? Kwenye post yangu nimesema wazi kuwa SITEGEMEI kuwa matamko yawe sawa kutokana na hali ya kisiasa ya wakati ule na umbali wa Pemba ukilinganisha na Arusha.

Umeninukuu kusema "hakuna WALIPOKEMEA serikali". Naendelea kusimamia hilo kuwa hawakukemea na paragraph uliyonukuu kutoka kwenye tamko, huwezi kusema WAMEKEMEA unless neno kukemea liwe linamaana nyengine sasa.
 
Back
Top Bottom