Maaskofu Katoliki walivyolaani mauaji Pemba 2001 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu Katoliki walivyolaani mauaji Pemba 2001

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miruko, Jan 19, 2011.

 1. M

  Miruko Senior Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu tamko la maaskofu kuhusu mauaji ya Arusha, huku wengine wakisema hakukuwa na taarifa kama hiyo kwa mauaji ya pemba mwaka 2001. Kwenye attachment ipo story ya gazeti la Majira Februari 25, 2001 (iko kama picha JPG) , likionesha jinsi Maaskofu Katoliki walivyolaani pamoja na mapendekezo yao, tusome kwa ajili ya kumbukumbu.


  Nyongeza

  Nomepata story ya Tamko la Viongozi wa Dini (kwa ujumla) la Februari 8, 2001 kuhusu mauaji ya Pemba. Source: Majira

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Watakuja tena walete longolongo lingine?? Wepesi wa kusahau!!!
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hapa mkuu umezidi kuwakandamiza Maaskofu Wakatoliki.

  Hakuna walipokemea serikali na ukisoma unaona wametoa lawama kwa vyama vya siasa na ukosefu wa elimu ya uraia
   
 4. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo utajiuliza sana busara ya viongozi wa kiislam wanaoongea mambo bila kuwa na kumbukumbu. Sijui kama huwa wanamaanisha wanachoongea au basi tu wanakuwa wanataka kuwafurahisha wafuasi wao. Hii ni aibu sana kwao na wafuasi wao! Asante sana kwa kutuwekea huu ushahidi hapa
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Isome tena Gaijin. Hasa paragraph ya 9.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  "watu wote waliohusika katika vurugu watafute suluhu kwa njia ya mazungumzo"

  "tukio hilo lilisababishwa na mambo mbalimbali baadhi ikiwa ni
  hisia za kihistoria, kukosekana kwa wale wote wanaohusika,kutoaminiana na kutokubali kuwa wote ni watu wa nchi moja, kughilibiwa kwa urahisi kutokana na watu kutojua mambo yanavyokwenda na umaskini"

  "tunataka ukweli utafutwe, na uwekwe bayana. Wale wote au yoyote yule anaetaka kusababisha machafuko, kutoelewana, awajibishwe kwa sheria za nchi"


  Kama hii makala ilikuja kuwatetea Maaskofu naona haiwezi kufanya kazi hiyo. Ni dhahiri kuwa maaskofu walikuwa upande wa serikali.
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Huwezi kusoma paragraph moja tu mkuu. The whole makala inaonyesha kuwa Tamko lilikuwa linaamini kuwa chama cha siasa kimesababisha vurugu na imewezekana hivyo kwa sababu 'vijana hawana kazi, umaskini, rahisi kughurubiwa, kukosa elimu ya uraia".

  Hakuna walipokemea serikali. Na huwezi kulinganisha na tamko lililotolewa sasa. Hili lilikuwa tamko la kupinga vyama vya siasa.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,389
  Likes Received: 19,678
  Trophy Points: 280
  mijitu ilikuwa inalaumu tu bila details sijui watakujaje tena

   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Umeshafanya uamuzi. Siwezi kukushawishi vinginevyo. Hata tamko la Maaskofu Katoliki kupitia Rais wa TEC lilikuwa laini kabisa kama hili. Nilimsikia akihojiwa BBC. Usisahau pia kuwa mmoja wa waliouwawa Arusha ni Mwislamu.
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mimi sijazungumzia uislam. Ninachozungumzia ni kuwa kwa wakati huo wa mwaka 2001, Tamko liliegemea moja kwa moja upande wa serikali na kuwa jukumu la kuleta amani waliwaachia vyama vya siasa.

  Tamko la mwaka huu limeegemea kwenye upande wa vyama/chama cha siasa na kuipinga serikali.
   
 11. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tupe maoni yako basi ni kwa nini tamko la safari hii linaipinga serikari na la zamani lilikuwa linaitetea serikali? Na kwa nini umeona hivyo?
   
 12. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Zile zama za 2001 na 2011 ni tofauti kabisa kama unafuatilia. Pia tension ya hizi sehemu mbili ni tofauti pia ijapokuwa yote ni siasa lakini kuna tofauti kubwa kati ya bara na visiwani.

  Hili suala la udini limepandikizwa na mjinga mmoja huko CCM. Kama ambavyo wengi tunavyoamini hakuwa udini what if CCM sasa ikiwa ya waislam na CDM ya wakristo? Simply NO CCM.

  Ndugu zangu waislam tusitafute majibu rahisi kwa issue ngumu kama hizi, kuirudi au kujirudi ni kwenye corner tu na heshima itakuwa wapi?
   
 13. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Gaijin hapa jf tuliaminishwa kuwa maaskofu hawakutoa tamko. Sasa kesi imebadilika ni kuwa walitoa tamko jepesi. Unaona kuna mtu anajaribu kuilisha jamii sumu ili watu waone kuwa maaskofu wanafanya kazi ya kusahihisha maovu anapokuwepo kiongozi mwislamu lakini ikiwa ni mkristo wako kimya. Je huu ni ukweli?? Inawezekana ni kama wahalifu sugu wafanyavyo anakujeruhi halafu anakuwahi polisi.
   
 14. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Someni kwa makini para 11 na 12

  " Tamko hilo pia limetaka elimu ya uraia iimarishwe na kupewa msukumo mpya, kutolewa kwa maoni watu waliopo nje ya vyombo vya habari kuhusu ushauri sahihi wa matatizo ya taifa na si kuchochea na kuvuruga wananchi"

  "Viongozi wanatakiwa kuwa karibu na wananchi wakati wa dhiki. Watu waepuke kuongozwa na jazba bali busara itumike wakati wote mambo ya kisiasa yanaposhughulikiwa na yale yanayoweza kuhatarisha amani"
   
 15. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa vizuri ukawataja hao watu ili tuwasute hapahapa na u copy link ya jukwaa waliokuwa wakisema maneno hayo. ila kikubwa zaidi mara nyingi kuna maneno ukiyazungumza utajuta mfano Cardinal Pengo aliposema hakutegemea kama Tanzania bara kungeweza kutokea mauwaji. Hii ina maana wenzetu wa upande wa visiwani wataichukulia kuwa wengi na especial Kanisa ninategemea mauwaji ya kisiasa yanaweza kutokea visiwani tu.

  My Take.

  Pengo kama kiongozi wa dini na wa wanajamii ya watanzania asitake tuamini kuwa yeye hakuwahi kujua katiba ina matatizo, na kama alijua je alishawahi kuinyooshea Serikali kidole? Kwa mauwaji yaliyotokea kiongozi gani wa dini iwe ya KKKT, Anglican, Bakwata, Baraza kuu, TAG na Full Gospel Bible Followship ambae hawajibiki na mauaji yaliyotokea Arusha?

  Kwa mtazamo wangu hakuna anaweza kujitoa kwenye ile kadhia, kuanzia viongozi wa kisiasa na wakidini.
   
 16. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa. Mijadala mara nyingi uongozwa na jazba badala ya kutulia na kuona tatizo liko wapi. Naomba msome Makala ya Msomaji Raia katika gazeti la Raia Mwema la leo Ukurasa wa 14. Makala nzurii sana kuhusu swala tunalojadili hapa leo.
   
 17. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  We should not be biased on this stuff. makosa mengine yako wazi. arusha wa2 walishatembea 4 2km then polisi ndio walipoleta gasia. now ww unaetaka kusema ghasia za mwembechai na pemba tel us the story what happened. alafu ndio 2angalie haya matamko yanatolewa katika hali gani na msingi ipi! 2jadili hilo.
   
 18. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  I wish tamko kama hili lingetolewa kwa tatizo la Arusha. Tatizo la Arusha limetengenezwa kwa makusudi maalum na hata tamko la Maaskofu lilifuata umaalum huo huo. Lau kama kusingekuwa na umaalum huo, kusingekuwa na haja kwa Maaskofu kukariri hoja ya CDM ya kutomtambua Meya na kutaka uchaguzi urudiwe kana kwamba na wao ni wapiga kura. Haya mambo ndo yanayotoa nafasi ya hisia za udini.
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kuanzia mwaka 2001 hadi sasa 2011 ni muda mrefu sana umepita na kuweza kusababisha mabadiliko makubwa ya mitazamo.

  Lakini kwa upande wangu sidhani kama tamko liliegemea serikali kwa sababu waliouliwa walikuwa 'waislam'. Inawezekana ikawa kulikuwa na woga kwa wakati ule na kushindwa kupinga serikali moja kwa moja au sababu nyengine inayoweza kufikirika ni kuwa 'Zanzibar ni mbali, sawa na nchi jirani'.
  Huwezi kutegemea tamko linalohusu mauaji mbele ya macho yako, na mauaji 'nchi jirani' kufanana.

  Na nukuu hapa maneno ya tamko
   
 20. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hitimisho;

  a) Maaskofu walitoa tamko mwaka 2001.

  b) Tamko hilo lilikemea kilichotokea.

  Hoja ilikuwa maaskofu hakukemea. Safari hii wamekemea. Sasa hoja ya nyongeza ni kwa nini hawakukemea vikali. Sidhani kama hoja ya nyongeza ina mshiko kwa sasa. Cha msingi walikemea na wakshauri. Serikali haikusikiliza ushauri wao kwa hiyo safari hii wameikemea zaidi. Hata kama walikuwa upande wa serikali then basi kwa kitendo hicho kurudiwa wana kila sababu ya kutoitetea serikali zaidi. Tusubiri kama CUF watapigwa tena tuone kama maaskofu wataitea serikali. Lakini CUF na wao wapigwe kwa kuonewa sio wafanye ukaidi ili wapigwe wategemee kutetewa na maaskofu na watu wengine! Waandamane kuhusu Dowans tujiunge nao. Wakipigwa na maaskofu wakikaa kimya ukweli utajulikana!
   
Loading...