Wakuu,
hapa lumbaneni. itaneni majina, semeni udini.
Ukweli utabaki kuwa 2001, wengi wetu tuliwaona Wazanj, wapemba kuwa ni wakorofi waliostahiki kushughulikiwa.
Tafuteni kauli, matamko, yaliyotolewa na masheikhe, misikiti au mapadri,wachungaji, makanisa.
Kwa ujumla wetu kama watz bara tuliona ni mambo yasiyotuhusu na yasiyotugusa kabisa.
La msingi sasa ni kuwa tunajua, "mwenzako akinyolewa. wewe tia maji".
kwa hiyo haki za raia mwenzetu yeyote ,akiwa mwanachama wa chama cha siasa, au hana chama, wa kikundi fulani au dini fulani au dhehebu fulani inapokanyagwa basi ni lazima tuhakikishe, tunasimama pamoja kulaani uovu huo na kutaka uwajibikaji kwa waliotenda ovu hilo au kuwajibishwa.
kuendeleza malumbano haya, yanatugawa tu badala ya kuungana..au bado hatujasoma, hatujang'amua kuwa tulitenda kosa kuona ya wazenj hayatuhusu? kuwa ni watu wakorofi waliostahiki rungu la dola?
Tusitake kumuosha mtu, kumsafisha mtu...yale ya 2001 yalipita na ni vizuri tuache kubeza maridhiano huko Zanzibar...na sasa tushughulikie haya ya leo yanayotukabili.
tusitoneshe vidonda vya 2001, hivyo vimeanza kupatiwa dawa, tutizame haya tulionayo leo, tuyakabili haya ,bila ya kunyoosheana vidole