Maaskofu Katoliki walivyolaani mauaji Pemba 2001

Zile zama za 2001 na 2011 ni tofauti kabisa kama unafuatilia. Pia tension ya hizi sehemu mbili ni tofauti pia ijapokuwa yote ni siasa lakini kuna tofauti kubwa kati ya bara na visiwani.

Tueleze hiyo tofauti kubwa tafadhali
 
je baada ya tamko hilo 2001 (jepesi kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini) kuna yoyote alitamka kuwa waache kujihusisha na siasa?
 
Na mbaya zaidi kuna watu wanachekelea na kushabikia udini. Na wala hawaoni kuwa hisia za udini ni janga la kitaifa.
 
Ukitazama vuziri hii story para ya 4, utaona tamko hili linaunga mkono tamko jingine lililotolewa na viongozi wa dini (Madhehebu mbalimbali) Februari 8, 2001. Bado nalifuatilia (lenyewe au story yake kwenye magazeti) ili niweke hapa tuone nalo lilikuwa linatoa kauli gani kuhusu mauaji hayo. Kumbukeni hapa tunajadili Story iliyotokana na tamko...tamko lenyewe halipo hapa, hivyo inategemea mwandishi/mhariri aliamua kutuletea taarifa kwa kiwango gani na kuacha mambo gani.
 
Na mbaya zaidi kuna watu wanachekelea na kushabikia udini. Na wala hawaoni kuwa hisia za udini ni janga la kitaifa.

Tukifanya watu wajuwe kwamba tunaangalia mazuri yao kabla ya mabaya yao watakubali kupokea nasaha. Siku zote msifie mtu kwanza halafu usimwambie mabaya yake bali mpe nasaha. Na ndio maana nasisitiza hakuna wa kuepuka lawama ya yaliyotokea Arusha na Zanzibar vyama vyote, makundi ya kutetea haki za binadamu, makundi ya kidini na waliopo madarakani kila mmoja ana nafasi yake katika hizi lawama.

Nimeona sehemu kumeandika haya maneno :-

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][FONT=arial, helvetica, sans-serif]Tanganyika Law Society, you guys make us (helpless wananchi) feel
proud that at least there are existing some remnants in the legal
fraternity who would still come to our aid at a great time of need
like this.

Ni kweli UWEZO MNAO wa kuifanya Tanzania yetu hii hii hapa kuwa mahala
pazuri sana kwa kila mmoja wetu kuishi raha mstarehe bila kilio cha
maonevu wala dhuluma. Pole pole wananchi tunaanza kuwatambueni umuhimu
wenu na huko mbeleni kidogo huenda pia tukaamua kuanza kuwathamini
kama taasisi muhimu katika ustawi mzuri wa taifa letu kwa ujumla.

Lakini hebu niambieni TLS ilikuaga wapi miaka yote hiyo tulipokua
tunanyanyaswa kushoto kulia na kusainishwa mikataba ya kitapeli kila
kukicha? Chonde msinyamazie hili swali langu kwa ni swali la wengi tu.
[/FONT][/FONT]

Hayo ni maswali baada ya tamko la TLS.
 
hitimisho;

a) Maaskofu walitoa tamko mwaka 2001.

b) Tamko hilo lilikemea kilichotokea.

Hoja ilikuwa maaskofu hakukemea. Safari hii wamekemea. Sasa hoja ya nyongeza ni kwa nini hawakukemea vikali. Sidhani kama hoja ya nyongeza ina mshiko kwa sasa. Cha msingi walikemea na wakshauri. Serikali haikusikiliza ushauri wao kwa hiyo safari hii wameikemea zaidi. Hata kama walikuwa upande wa serikali then basi kwa kitendo hicho kurudiwa wana kila sababu ya kutoitetea serikali zaidi. Tusubiri kama CUF watapigwa tena tuone kama maaskofu wataitea serikali. Lakini CUF na wao wapigwe kwa kuonewa sio wafanye ukaidi ili wapigwe wategemee kutetewa na maaskofu na watu wengine! Waandamane kuhusu Dowans tujiunge nao. Wakipigwa na maaskofu wakikaa kimya ukweli utajulikana!

Yaani unawategemea watu waridhike kuwa tamko lilitolewa japo kuwa tamko hilo lilikuwa tofauti kwa asilimia 100 na tamko lililotolewa sasa?

Ni bora ingelikuwa halikutolewa kabisa kuliko tamko lilokuwa likipendelea serikali baada ya kitendo cha kikatili cha mauaji.
 
Yaani unawategemea watu waridhike kuwa tamko lilitolewa japo kuwa tamko hilo lilikuwa tofauti kwa asilimia 100 na tamko lililotolewa sasa?

Ni bora ingelikuwa halikutolewa kabisa kuliko tamko lilokuwa likipendelea serikali baada ya kitendo cha kikatili cha mauaji.

Nadhani wakati ule ndio hao waliosema JK ni chaguo la Mungu lakini miaka mitano baadae wakabadilika rangi zao. Wahenga walinena
Kabla ya kuzungumza chaguwa neno la kusema, na uchukuwe muda wa kusema ili maneno yako yachipuwe kama linavyo chipua mmea
wakaendelea kusema
Watendee watu kama wao ni binaadamu si kwa sura zao wala pesa zao wala vyeo vyao wala dini zao
mwisho wakamalizia
Anaye ishi na sura mbili,hufa bila ya sura
Sasa kazi kwao hao waliosema JK chaguo la Mungu leo hii wanaenda mbio kupinga kauli zao.
 
Kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu tamko la maaskofu kuhusu mauaji ya Arusha, huku wengine wakisema hakukuwa na taarifa kama hiyo kwa mauaji ya pemba mwaka 2001. Kwenye attachment ipo story ya gazeti la Maira Februari 25, 2001 (iko kama picha JPG) , likionesha jinsi Maaskofu Katoliki walivyolaani pamoja na mapendekezo yao, tusome kwa ajili ya kumbukumbu.

Soma na uelewe mantiki ya taarifa nzima kabla ya kuibandika hapa JF.

Lakini wewe unaelewa maana ya neno KULAANI. Itafsiri hilo neno katika kiingereza, halafu usome tena hiyo taarifa na utueleze maneno yaliyotumika kulaani mauaji ya pemba. Tofautisha kati ya kulaumu na kulaani

Msikazane kutafuta yasiyokuwepo, ili muonekane wazuri leo. Na angalieni kauli zenu za leo zitakuja kuwasuta baada ya miaka 6 na kuendelea.
 
Kuanzia mwaka 2001 hadi sasa 2011 ni muda mrefu sana umepita na kuweza kusababisha mabadiliko makubwa ya mitazamo.

Lakini kwa upande wangu sidhani kama tamko liliegemea serikali kwa sababu waliouliwa walikuwa 'waislam'. Inawezekana ikawa kulikuwa na woga kwa wakati ule na kushindwa kupinga serikali moja kwa moja au sababu nyengine inayoweza kufikirika ni kuwa 'Zanzibar ni mbali, sawa na nchi jirani'.
Huwezi kutegemea tamko linalohusu mauaji mbele ya macho yako, na mauaji 'nchi jirani' kufanana.

Na nukuu hapa maneno ya tamko

Ok nimeshakipata ulichojisadikisha kwenye akili yako, sawa ni ngumu kumwelewesha mtu ambaye tayari ameshakiona anachokielewa ni sahihi, Kumbe waislam si watanzania? Aisee udini huu utatubagua mpaka basi!
 
Katika kipande cha hilo gazeti hakuna sehemu ambapo maaskofu walipoikemea au kukosoa serikali juu ya hayo mauaji.
 
Ok nimeshakipata ulichojisadikisha kwenye akili yako, sawa ni ngumu kumwelewesha mtu ambaye tayari ameshakiona anachokielewa ni sahihi, Kumbe waislam si watanzania? Aisee udini huu utatubagua mpaka basi!

Kaka nisome uzuri nimeandika hivi na najinukuu

SIDHANI kama tamko liliegemea serikali kwa sababu waliouliwa walikuwa 'waislam'

Unajua maana ya SIDHANI?
 
Kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu tamko la maaskofu kuhusu mauaji ya Arusha, huku wengine wakisema hakukuwa na taarifa kama hiyo kwa mauaji ya pemba mwaka 2001. Kwenye attachment ipo story ya gazeti la Maira Februari 25, 2001 (iko kama picha JPG) , likionesha jinsi Maaskofu Katoliki walivyolaani pamoja na mapendekezo yao, tusome kwa ajili ya kumbukumbu.

kumbukumbu nzuri
 
Mimi sijazungumzia uislam. Ninachozungumzia ni kuwa kwa wakati huo wa mwaka 2001, Tamko liliegemea moja kwa moja upande wa serikali na kuwa jukumu la kuleta amani waliwaachia vyama vya siasa.

Tamko la mwaka huu limeegemea kwenye upande wa vyama/chama cha siasa na kuipinga serikali.

kwani CCM ambayo ndiyo inaongoza serikali na Mkapa ndiye alikuwa mwenyekiti wake na rais wakati huo, hiyo ccm si chama? au ni mpaka msikie wametukana matusi ya nguoni ndiyo mtaamini kuwa wamelaani matukio ya ukandamizaji na unyanyasaji?
 
kwani CCM ambayo ndiyo inaongoza serikali na Mkapa ndiye alikuwa mwenyekiti wake na rais wakati huo, hiyo ccm si chama? au ni mpaka msikie wametukana matusi ya nguoni ndiyo mtaamini kuwa wamelaani matukio ya ukandamizaji na unyanyasaji?

Tamko litaegemea vipi upande wa serikali (ambayo inaongozwa na CCM na Mkapa) wakati huo huo ipinge vyama vya siasa kisha useme CCM ilipingwa pia?

Mie sioni tatizo liko wapi. Miaka 10 nyuma tamko lilikuwa upande wa serikali sasa liko upande wa vyama vya siasa.
Miaka kumi ni mingi, hakuna ubaya kwa Kanisa kubadili msimamo wake kwenye masuala ya kijamii.
Hii ya kulazimisha tamko 'lisomwe' vyenginevyo mimi siielewi.
 
Para 13: "Maaskofu pia wametaka vyombo vya dola vielimishwe njia za kisasa za kukabiliana na vurugu na kuwa na utu katika kutekeleza majukumu yao" Hapo pia bado hamridhiki?
 
Nakumbuka pia kuna Mkutano wa Anglikana ulifanyika Dodoma ambako kulikuwa na mwakilishi wa serikali ya CCM na CUF iliwakilishwa na Prof. Lipumba, Askofu Mkuu wa Anglikana, Dk. Mokiwa alitoa maneno makali juu ya danadana za serikali kuhusu mwafaka wa CCM na CUF. Alihitimisha kwa kusema "Rejeeni katika mazungumzo, lakini muache unafiki". Natafuta reference hiyo nikiipata nitaipost hapa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom