Wanabodi,
Imenibidi kuchukua njia tofauti ya kuufikisha ujumbe wangu kwa wananchi. Na moja ya kazi yangu kubwa itakuwa kupambana na mawazoz ambayo kila siku yanategemea serikali yake itamfanyia nini wakati yeye mwenyewe hafikirii lolote la kuifanyia serikali yake. Haiwezekani ukapewa maisha bora on a silver plate na wala hizi habari za kulalamika tuu haziwezi kutupeleka popote pia maamuzi yoyote yasiyoweza kujenga hayawezi kupongezwa.
Kwanza nitazungumzia haya maandamano ya Washingtona DC, BBinafsi nayaona ni waste of time kwa sababu kinachofanyika ni kutoelewa mahusiano baina ya serikali ya Marekani na Tanzania na nini msimamo wa Marekani kuhusiana na Tanzania. Maandamano kama haya ni sawa na Palestine waandamane dhidi ya Israel ingawa case hazifanani.
Pili wakati mwingine tunapopanga jambo la kufanya ni vizuri pia kutazama athari zinazoweza kujitokeza. Tusiwe kama waaarabu ambao wanaona haki yao kujitoa mhanga na kujilipua mabomu nchi za watu ili kupelekea ujumbe unaohusu nchi zao. Na matokeo yake ndio wanaitwa Terrorist na hakuna tafsiri nyingine ya kuwapongeza hata kidogo.
Hivyo tupo ktk wakati wa kujaribu kujenga mahusiano baina ya Watanzania wa ndani na nje hivyo kufanya maandamano haya DC sidhani kaa yataweza kutusaidia zaidi ya kuonyesha utovu wa heshima kwa rais ambaye ni mwaka jana tu amechaguliwa na wananchi walio wengi tena basi yawezekana wote mnaoandamana hamkupiga hata kura..
Kitu kimoja tu ni kwamba wakati nchi za wenzetu hu raise bar ktk mafanikio sisi hupandisha bar ktk matatizo. Ni sawa maamuzi ya kuruka matatizo kila bar inavyopanda ndivyo tunavyipanga kuyaruka utafikiri mashindano ya kuruka juu..Sasa cha ajabu tulifika mahala ambapo ndio mwisho wa uwezo wa binadamu kuvumilia matatizo. Kama ni kuruka basi tulifikisha bar kwenye mita tatu ambapo hakuna binadamu anaweza kuruka kwa nguvu zake mwenyewe..Watanzania ndio kwanza tukatafuta njia ya kuruka juu na mti (polls)..
Ni wazuri sana wa kutafuta njia za kukabiliana na matatizo hivyo sasa hivi kila mtu anaruka na mti matatizo na kwa bahati mbaya upande wa pili hakuna confort ya kuangukia godolo.. Kila siku wanakufa, wanavunjika mbavu, miguu na kadhalika kutokana na matatizo haya ya kuruka highjump na miti bila kujua upande wapili hakuna sehemu nzuri ya kutua..isipokuwa sisi Wadanganyika tunachokiona n urefu wa bar ya matatizo na tutaweza vipi kuruka matatizo hayo kwenda upande wa pili..
This is not good, Watanzania wenzangu inabidi tufike mahala tujitazame sisi wenyewe na kujiuliza tunaifanyia nini Nchi yetu. Kama wewe ni fisadi ama jirani yako ni fisadi basi tuchukue maamuzi magumu..nakumbuka wizi wa vibaka nchini umepungua sii kutokana na ukali wa sheria ya serikali bali maamuzi ya wananchi wenyewe kuhakikisha wizi wa vibaka unakwisha. Watu walifikia kuchukua madaraka mikononi mwao wakiwashika vibaka huwachoma moto.. siombei hili na wala silipongezi isipokuwa mahala ambapo serikali ilishindwa wananchi walichukua maamuzi magumu.. Leo hii vibaka wamepungua, mtu unaweza kwenda kariakoo na pochi lako mfukoni ukakatiza mitaa ya Kongo na chain ya dhahabu..
haya yote hayakuwa maamuzi ya serikali isipokuwa wananchi wenyewe kukomesha wizi na karaha za vibaka. sasa basi imefika mahala Ufisadi umekuwa sugu na hauwezi kupatiwa dawa na serikali. wananchi wenyewe chukueni jukumu la kuwafuata Mafisadi na kuwaambia ACHA unachokifanya!.. Kama kiongozi wa serikali mwambieni ACHA UFISADI au laa wananchi tunachukua jukumu wenyewe...
Na pengine ningewaomba sana badala ya maandamano mwendeni Washington na agenda ya kumwambia JK achukue jukumu alokabidhiwa na wananchi kuwafikisha mahakamani waharifu wote laa sivyo wananchi watachukua jukumu hilo. hakuna sababu ya kumwadhili, kumkashifu hali yeye ndiye baba wa taifa iwe sifa kwetu...Itisheni mkutano na mumkalie kooni inatosha zaidi ya fikra za kuadhiliana hali sisi wenyewe ndio tulipandisha bar na hatujawahi kuweka cap ktk matatizo yetu..Mwisho wa uwezo wetu ktk kukabili matatizo haujulikani maanake tunapandisha tu bar.
Ndugu yangu Mzee Mkandara,heshma mbele.Nimeipenda post yako hii,(zingatia bold)lakini sikubaliani na mengi ulioyasema ili kujustify shinikizo ama hoja kwamba wenye mwelekeo wa maandamano waache kufanya hivyo.
Pengine kuna sababu nyingine(nadhani zipo)nzito kidogo zaidi,hata hivyo bado zinaweza kuwa disputable.Hilo la kudhalilishwa first off sikubaliani nalo.
Kama serikali ina mamlaka na mihimili kama mahakama,polisi na bunge.Basi ni lazima yawepo maswali pale inapokuja kutokuwajibika ama kutokuwajibishwa kwa wahujumu uchumi na mafisadi kwa ujumla.Wananachi walioko Tanzania wana shida nyingi sana na pia zinapelekea wao kuwa wepesi wa kusahau.
Kwa upande mwingine,wameshaona kuwa kama habari za magazeti ni soap opera.Kashfa za ufisadi zikija wanapiga tu domo na muda si mrefu werevu (mafisadi)wanaowajuwa wana tune to a diffrent music.(idara ya habari imetekwa).Unasikia story inabadilishwa na wadaganyika wanajump on to the band wagon.Humu ndani tunatakiwa tuwe tofauti.
Mtanzania ambaye amekuwa exposed ie walioko nje ni tofauti sana na wale ambao hawakufanya hivyo.(wanaorudi na kutowajali wananchi wana mioyo ya ajabu)Kwa namna dunia ilivyo kwasasa,mawasiliano yamekuwa rahisi sana,mfano ni tweeter,FB,na hata hii JF.Walioko nje hata kama hawajarudi nyumbani siku za karibuni,bado wanawasiliana na ndugu zao kwa karibu sana na wanahisi kama na wao wako huko kwasababu ni familia.Wanaelezwa shida dada zao,mama zao,shangazi zao,wajomba zao nk wanazopitia kila kukicha kuanzia umeme,mafuta usafiri nk,matatizo ni mengi,achilia mbali wasiojuwa watakula nini siku inayofuata.And so therefore they symphathise with fellow Tanzanians ie family members na hata citizens kwa ujumla.
Serikali kwa upande wake ni ya kulaumiwa badala ya kuwalaumu wananchi kwasababu ina vitendea kazi vya kulishugulikia hili suala.Laiti kama wangetumia nguvu za jeshi la polisi kuwakamata mafisadi badala ya kuuwa raia wasiokuwa na hatia na kujaribu kuwatisha wenye kuibua ufisadi.Laiti kama jeshi la wananchi/jeshi la kujenga Taifa wangekuwa wanashughulishwa na ujenzi wa Taifa kama infrastructures ie madaraja,road constructions nk,na si wenye vyeo vya juu kula mishahara baada ya kupelekwa nje vitani ama MEREMETA.Laiti kama mahakama hizo zingewahukumu mafisadi kwa haki.Laiti kama taasisi ya kuzuia rushwa ingekuwa inafanya kazi yake kiukweli badala ya usanii tunaouona.Laiti kama wabunge wa magamba wangeacha kulala bungeni na kuamka kuendelea kulipwa.Ama kutetea hoja bila kujali maslahi ya Taifa.Hayo si utumishi wa umma.Na rais yuko kimya,tunasikia yeye anasafiri tu.Laiti kama bunge hilo lingekuwa linatumika kupitisha mikataba yenye tija kwa Taifa...What is our priorities?Najiuliza kila mara,what would it take for them to listen?Hilo ndilo la kujuliza.
Unless uniwekee sababu nzito za kuwapinga wenye kutaka kuandamana.Basi ndipo nitakubalina na wewe mkuu.
Nantanguliza shukran,na pia nategemea kuendelea na mjadala huu mzito ambao unaonekana umeamsha wengi.
Pia nakubaliana na pendekezo kuwa apelekewe agenda ya kuchukua jukumu alilokabidhiwa na wananchi kuwapelekea watuhumuiwa wa ufisadi mahakamani.However hilo lingekuwa la maana kama kungeonekana dalili za yeye kuwashughulikia.
Nionavyo mimi ni michanga ya macho tu every now and then.Tulijadili sana humu kuhusu EPA nk,hadi sasa naona usanii tu na hatujui kiasi kilichorudishwa na ni wapi pesa hizo zinatumika,je ni kwa manufa ya wananchi kama alivyo ahidi?Kama ni kweli hataki kudhalilishwa(mana maisha ya watanzania wengi ni ya kiudhalilishaji)Basi kabla hajatia timu ajibu maswali akiwa huko huko,then ninaweza kuunga mkono hatua ya tofauti na agenda za tofauti,shida ninayoona mimi hapa ni kwamba wananchi hawasikilizwi.