Unstoppable
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,046
- 387
Wanabodi
Na pengine ningewaomba sana badala ya maandamano mwendeni Washington na agenda ya kumwambia JK achukue jukumu alokabidhiwa na wananchi kuwafikisha mahakamani waharifu wote laa sivyo wananchi watachukua jukumu hilo. hakuna sababu ya kumwadhili, kumkashifu hali yeye ndiye baba wa taifa iwe sifa kwetu...Itisheni mkutano na mumkalie kooni inatosha zaidi ya fikra za kuadhiliana hali sisi wenyewe ndio tulipandisha bar na hatujawahi kuweka cap ktk matatizo yetu..Mwisho wa uwezo wetu ktk kukabili matatizo haujulikani maanake tunapandisha tu bar.
Mkuu hapo penye red hicho kitu kilishafanyika term ya kwanza ya utawala wake. Nilikuwa washington Dc wakati huo and it was wastage of time kwasababu zifuatazo: Wauliza maswali walichaguliwa kabla ya muda hivyo wengine hatukupata nafasi yakuuliza maswali. 2. Maswali yaliyoulizwa hayakulenga moja kwa moja kwa mafisadi , ingawa yalilenga kero za wananchi, raisi hakujibu kitu kinachoeleweka zaidi yakucheka cheka tu. 3. Mahali mkutano ulipofanyika watu walikunywa pombe kabla mkutano haujaanza (nahisi nimapandikizi walifanya hivyo purposely) kwahiyo mkutano ukaonekana vurugu tupu. Why do you believe raisi wa nchi asiyesikiliza watu wake nyumbani even wabunge atawasikiliza watu walioko nje ya nchi? Kwanini raisi wa nchi anatakiwa "akaliwe kooni" kufanya kazi alizochaguliwa purposely kuzifanya? It is his responsibility to do so, miaka karibia sita hii hajifunzi, huo uvumilivu wa Watanzania sasa umepitiliza. Zaidi ya yote amekua anatoa majibu yakebehi yasioonesha kwamba even anajaribu au anajua anafanya nini. Kweli mtu huyu unamvumilia mpaka lini? When is it enough? It is up to DC people to decide, lakini kwahili wazo lako sikubaliani nalo. Najaribu kupima kipi kizito a) raisi kuabikia au b) ndugu zangu wanaokufa kila siku kwa uzembe wake na watendaji wake. Naona kama kuaibika aiibike tu. Kama kukosa wafadhili then let it be afterall hizo pesa za wafadhili hazimsaidii mwananchi wakawaida. Tukumbuke mficha maradhi humuumbua yeye mwenyewe. Tumekuwa tunaficha matatizo yetu lakini yanaendelea kutuumiza. Ni lazima raisi a-act now, hatumuombi, ni wajibu wake kufanya hivyo. Ni lazima tumueleze what we want na tuna mpa muda maalum wakuyatekeleza sio porojo za kuvua gamba nakuongezeana muda. Tumechoshwa na kamati zisizokuwa na tija, kila kitu kinaundiwa kamati watu wanakula tu pesa. Ni lazima tuelewe undani wa tatizo la umeme na nini kinafanyika nasio kusubiri mvua.