Maandamano ya amani kwa wanafunzi wote wa vyuo nchini

kuna mambo mawili ya kuzingatia
moja kigezo cha malipo ni idadi ya siku au mhula?(mkataba umesema fixed amount au kuna bases za kupata iyo amount per day?
pili kigezo cha ada ni idadi ya siku kufundishwa au material na gharama za kuendesha chuo kwa siku husika?
ukishapata majibu mnaweza endelea na hatua inayofuata.....ila tusisahau anko sio mjomba
Hadi njiuliza hivi Elimu zinafaida gani kama mtu anadai kulipwa hela ya siku ambazo hayumo chuoni.
Mkataba umeandika mtu alipwa Per Day ila kwa vile kazoeshwa lipwa 510,000 kila Phase ndo anaikazania.

Hivi hawaezi kuhoji kwanini wanaosoma MD wana boom kubwa kuliko Wengine?(Kinachoangaliwa ni idadi za siku za masomo chuoni,sio semistar na ndo inayopelekea wanaosoma MD japo huita semistar kubwa na boom maana hukaa chuoni siku nyingi.)
 
Hamjambo wanabodi
Moja kwa moja niende kwenye mada husika, kutakuwa na maadamano ya amani dhidi ya bodi ya mkopo nchini (HESLB), maandamano haya yataanza siku ya jumatatu tarehe 27/07/2020 na kuendelea mpaka pale HESLB itakapo rejea masharti ya mkataba na kutenda haki kwenye utoaji wa pesa ya kujikimu(boom).
.
Maandamano haya yatafanyika kwa kufuata hatua zifuatazo:-
.kutoingia darasani kuanzia jumatatu na kuendelea mpaka pale pesa itakapo kuja yote kutoka HESLB
..
Kwanini maandamano?
Kwasababu mkataba ulipo kati ya mnufaikaji wa pesa ya kujikimu ni sh 2, 040, 000/=kwa mwaka ambapo hulipwa sh 510, 000/= kwa kila phase. Mwaka wa masomo huwa una phase 4 za ulipaji. Kilichotokea baadhi ya vyuo wanaambiwa wakasaini boom la sh 306, 000 /=kwa UDSM na sh 206, 3000/= kwa UDOM, vipo vyuo hadi laki moja.
Ukirejea mkataba haujawahi kusema kwamba ikitokea siku zimepungua na pesa itapungua.
.
Kama ndio hivyo basi nasi mtupunguzie ADA maana muhula umekuwa mfupi na siku zimepungua sana.
.
Vijana wa kiume na kike naomba tuungane kwa pamoja kufanikisha wazo hili najua nalo litapita lakini tunaihitaji kuwakumbusha bodi ya mikopo kwamba hatujalala na tupo hapa kupigania haki zetu kwa pamoja tunaweza.
.
Vijana ndio taifa la kesho, amka pambana dai haki yako na tekeleza wajibu wako.
......kwa UDSM tukutane 'Revolution Square' jumatatu SAA 2 asubuhi....
..
..
#MAANDAMANO YA AMANI
View attachment 1515754
Funny.

Mungu awatangulie mimi simo.
 
Hizo laki mbili zitawatokea puani!

Be humble. Ni ushauri tu lakini.

Unaweza kuwa upande wa haki na ukaumia vile vile!

La kuambiwa........
Haki ni haki tu! Acheni kuwalisha upuuzi vijana! Kama wewe ni zuzu hujui kudai haki yako kwa ujinga wako tulia
 
Madogo mtavunjwa miguu....hawana na hela uchaguzi ndiyo huu.....mtu mzima akiguna basi ondoka kalale ukikomaa unalitaka balaa...yaani mwana kuli faindi.....

afu timbwili lenyewe mtakiweza nyie watoto mayai? Ule mziki ni balaa lazima mjue kuucheza

Siwatishi ila mkigawanyika tu mmekwisha...degree zenu mtazipatia home ...dutumiii....!! Mzenga, Kisaki na Kidogozero...
Acha kutisha vijana! Kwani kuandamana ni kosa? Na hukumu inatolewa na polisi?
 
Hadi njiuliza hivi Elimu zinafaida gani kama mtu anadai kulipwa hela ya siku ambazo hayumo chuoni.
Mkataba umeandika mtu alipwa Per Day ila kwa vile kazoeshwa lipwa 510,000 kila Phase ndo anaikazania.

Hivi hawaezi kuhoji kwanini wanaosoma MD wana boom kubwa kuliko Wengine?(Kinachoangaliwa ni idadi za siku za masomo chuoni,sio semistar na ndo inayopelekea wanaosoma MD japo huita semistar kubwa na boom maana hukaa chuoni siku nyingi.)
Na vipi wale wameopanga, ambao vyuo vyao havina hostel/hostel hazitoshelezi ,wenye nyumba watawapunguzia kodi kisa muda wakukaa chuoni umepunguzwa?.

Vipi ada nazo zitapungua kwa sababu muda wa masomo umepunguzwa?.

MD wanapata boom kubwa kwa sababu ya siku zakukaa chuoni ndio, kwa sababu pia hufahamika tangu mtu anapopewa mkopo kiasi cha mkopo wake kwa semister.

Kama wanaounguza kiwango cha pesa wangeshauri pia vyuo pia vipunguze viwango vya ada, maana kuna wengine wanapata pesa ya kujikum hio hio hutumia kulipia ada.
 
Fikilia kabla ya kutenda! Mhurumie mzazi ambae amekutoa nursery mpaka hapo ulipo fikia wenzangu tafadhali nawaombeni msifate mawazo hayo wahamasishaji hao wana lao jambo nyuma ya pazia Tafadhali utaipoteza nafas adhimu ya masomo wenzako hao utawaona wanasonga upande mwingine Tafadhali sana ipuuze taarifa hii
Taifa linapitia kipnd kigumu sana cha MSIBA WA RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Watanzania wenzangu vijana tuwe wazalendo wa nchi yetu mioyo yenu iyone uchungu wa kujenga nchi yako
Soma nyakati za taifa lako unataka wakufanyie nini wewe kwani budget za wazaz wetu zina fanikiwa 100%? Tujitambue vijana wenzangu sio kila kitu kinataarifa ndugu zangu!! Aaah naumia sependezwi kabisa usikubali kutumiwa, SOMA NYAKATI LA TAIFA LAKO

TAFUTA NJIA NYINGINE YA KUPATA HAKI YAKO HII NI BATILI.
Hawa wanafunzi wanaleta majaribu 😂
Kipigo watakachopata asee hawataamini.
 
Tupo kwenye wakati ambao anayedai haki yake anaonekana mkosaji, tupo kwenye kipindi ambacho kila waziri anajitutumua kwa ubabe bila kuangalia namna ya kuwasaidia anaowaongoza.
Tupo kwenye kipindi ambacho hadi akina mama kama Mh. Ndalichako wanakosa uchungu wa watoto wa mama wenzao kwa kuwafukuza vyuo kisa wameomba haki zao ili tu ionekane kwenye kipindi chao hakuna mtu aliyeandama.

Be careful guys.
tukumbuke na kurejesha na riba na bodi hawana mkataba mpaka upate kazi
 
Tangu lini wanafuata mkataba hawa? Wanajipangia tu vile wanavyojisikia. Hata hii 15% wanayotukata ni nje ya mkataba ila waliilazimisha hadi wakafanya yao.

Kila la kheri katika hayo maandamano.
Hope mmeusoma mkataba na kuuelewa maana nijuavyo mie hizo pesa hulipwa kulingana na idadi ya siku za masomo ila ada huwa si hivyo.
 
kuna mambo mawili ya kuzingatia
moja kigezo cha malipo ni idadi ya siku au mhula?(mkataba umesema fixed amount au kuna bases za kupata iyo amount per day?
pili kigezo cha ada ni idadi ya siku kufundishwa au material na gharama za kuendesha chuo kwa siku husika?
ukishapata majibu mnaweza endelea na hatua inayofuata.....ila tusisahau anko sio mjomba

Usikute zishapigwa panga juu pasu kwa pasu,Kama zilikuwa kwenye schedule kwann wasipewe
 
Back
Top Bottom