mjandwasafi
Member
- Jun 6, 2023
- 10
- 19
Hello habari za majukumu.
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha kikatoliki Ruaha (RUCU) kilichopo Iringa.
Kwasasa changamoto ambayo wanafunzi wengi tunaipotia ni ucheleweshwaji wa pesa za kujikimu (meals and accomodations) ambayo ni sehemu ya boom.
Kitu kinachotushangaza na kutusikitisha wanafunzi wengi ni kwamba baadhi ya wanafunzi hususan waliopo mwaka wa kwanza na baadhi ya wale waliopo mwaka wa pili tayari wamepokea pesa hizo na wengi wao wapo field (na hawa ni wale ambao husaini fedha hizo kwa kupitia HESLB app) na kundi kubwa la wale tuliobaki chuoni mwaka wa tatu na nne ( Kwa upande wa sheria) ndio tunakumbana na changamoto hii. (tunaosaini pesa hizo kwa alama za vidole)
Kwa kawaida pesa hii huingia baada ya siku 60 ambapo ni sawa na miezi 2 kwa semester na kwa mara ya mwisho pesa hii iliingia tarehe 20/12/2023 lakini cha kushangaza mpaka wakati huu naandika haya pesa hii haijaingia ikiwa ni tarehe 18/03/2024. Na hakuna taarifa yoyote ya kuridhisha kutoka kwa viongozi wanaohusika na suala hilo chuoni.
Kimsingi hali za watu ni mbaya sana, uendeshaji wa maisha umekuwa mgumu mno. Na wengi wetu ukizingatia tumetoka familia ambazo siyo imara sana upande wa uchumi kwani pesa hizo ndizo hutuwezesha kujikimu kwa muda wote tunaokuwa chuoni.
Ninaomba mamlaka husika ziingilie kati suala hili kunusuru hali za maisha yetu.
Asante.