Dr.dennice
JF-Expert Member
- Jan 4, 2016
- 216
- 48
Alichokiondoa yeye ni utaratibu wa kuchagua masomo form three nadhani ana dhamira nzuri tu tusipende kutafuta baya katika kila zuri
Rebecca unataka kusema hao watoto wamewashinda wahitimu wetu wa Sayansi??hivi hujawahi kuona watoto wakijenga toroli la mbao?hehe
tatizo la wabongo ni kulalamika tu...nani kakwambia ukisoma sayansi hutasoma sheria..hata hivyo si wamesema anetaka kuchagua art anaruhusiwa akifika fm4....jaribuni kutafiti hata kidogo wanafunzi wanaofaulu asilimia 90 niwale wanaosoma masomo 9..wale wanaokimbilia arts huishia kufeli tu.....kwa mfano ktk shuleyetu tulifaulu watu 7 lakini wote tulikuwa tunasoma masomo ya sayansi na arts..wale wa arts tuwapoteza woteViongozi wa kisiasa ndio wanao haribu elimu ya nchi hii.
Kila waziri anaekuja anakija na style yake. Iliradi akitoka kesha chafua mtaala anapita hivi....
Wanadhani kila mtu akisoma sayansi hizo fani nyingine ni nani atafanua?
Wana maana jakuna tena wakusoma sjeria, utawala, ualimu, mambo dini nk!! Yaani Tanzamia ya viwanda....
Maigizo tuu hapa.
Wengi mmeona habari ya leo kuwa sasa ni lazima wanafunzi wote wasome Sayansi kabla ya hiii zimekuwepo habari nyingi za kushangaza za wizara hii ya elimu. Siku Magufuli aliposema anashangaa fimbo kupigwa marufuku mashuleni, kesho yake tu Wizara hii ikatangaza 'fimbo kurudishwa mashuleni'
yaani halikuwa na mjadala wala kutolewa maelezo labda why fimbo zilizuiwa mwanzo au kuna watalaam gani walihusika kufikia maamuzi.
Halafu yakaja maamuzi ya kuongeza ufaulu ili kujiunga na vyuo, hili nalo limechukuliwa kama Tanzania ni kisiwa vile mpaka sasa wala hakuna maelezo iwapo mwanafunzi wa kitanzania akipata nafasi kusoma nje ya nchi kwa ufaulu ambao hapa nchini haumruhusu, vyeti vyake vitakuwa na 'status' gani hapa nchini mradi maamuzi ya wizara hii sasa ni kama vile Tanzania ndo 'The world'
na kila atakachoamua yeye ndo 'final'
Huyu mama na Mabosi zake wanasahau kuwa tuko katika 'global village' Maamuzi ya ajabu ajabu sanasana yatawaathiri watoto wa masikini tu
wengine wenye options za kusoma nchi jirani na nchi za mbali hayatawagusa na mwishowe watakao 'umizwa na maamuzi' haya ni watoto wa masikini.Sasa hili la lu kulazimisha Sayansi nalo unajiuliza nchi ngapi duniani linatumika?
Je mtoto wa kitanzania akisoma Kenya au Uganda au kwingineko
ambako hakuna 'maamuzi ya aina hii' huyu mama atafanyaje? Hivi why 'tuna invest kwenye kuongeza kero na vizingiti' vya kila aina kwa watanzania? Kwani Tanzania ni kisiwa? Si masuala ya elimu yanapaswa kuwa 'Universally acceptable'? Sasa huyu mama ndo mifano wa maprofessa wetu?
Huwa mara kwa mara nawaambia watu kuwa tangu tujitawale hii serikali ndiyo itakayoingia kwenye vitabu vya historia kama serikali mbovu na ya hovyo kuliko zote. Hii ni kwa sababu haina mkakati katika jambo lolote, ni sawa na kusema inaendeshwa toka kijiweni tu.
Elimu yetu ni ya ubaoni na chaki tu badala ya kuwa ya mfumo wa kuibua na kukuza vipaji na mielekeo ya wanafunzi tangu utotoni kama nchi zingine zinavyofanya.
Hatuwezi kuwa na elimu ya maana mpaka pale tutakapoioanisha na maisha halisi, mazingira ya kibinadamu na mahitaji yake.
Ndiyo maana pamoja na JPM kuwa "doctor" na kulundika madaktari wenzie, maprofoo, na mainjinia bado kuna uhaba wa fikra.