Consultant
JF-Expert Member
- Jun 15, 2008
- 11,620
- 21,161
Kuna watu tunachangia tu na kurusha makombora probably bila kuwa na uhakika sana na alichokisema Prof. Ndalichako
Mzaha UPI?? Ww toa point zako zieleweke maana imeshakuwa ni mjadala wa kitaifa hata kama unamuunga mkono tupo ambao hatuungi mkono hasa kuweka limit yalazima form6...Wakuu acheni mzaha kwenye elimu.
Leo nakuunga mkono mkuu..huyu mama atupelekako sasa ni kule tulikotoka...hadi aliyepata kadigrii kake bils form 6 ajiangalie wakti kuna watu wanesota hadi kufikia hpo na wengine ni maprofesa wamejiendeleza ns kufika huko. Kwa hali hii mtoto wa maskinj kujiendeleza ndo itakuwa basi tena
Naunga mkono hoja, amekurupukaWaziri wa elimu Ndalichako kwa kuendelea kutoa matamko yako ya utatanishi juu ya elimu ya Tanzania ikiwepo la kuwazuia watu kujiendeleza kielimu ni kujivunjia heshima
Diploma za technician zinakubalika.Umesoma hilo tamko au umehadithiwa.Mzaha UPI?? Ww toa point zako zieleweke maana imeshakuwa ni mjadala wa kitaifa hata kama unamuunga mkono tupo ambao hatuungi mkono hasa kuweka limit yalazima form6...
Kama anataka diploma zifutwe ..
Hiyo ni danganya Toto huu ni mwanzo wa kuchinjiwa baharini watu wa diploma..Diploma za technician zinakubalika.Umesoma hilo tamko au umehadithiwa.
Very true mkuu,kuna watu wengi wamekuwa maprofesa na madaktari bila kupita form 6 huyu mama hajielewi
Ni ukweli kabisaa mpka nkauliza ukiwa t.o toka uanze mpka kumaliza ina maana una maamuzi sahihi kwenye kila kituMH.NDALICHAKO HII SIYO NECTA
Kwa kipindi cha miaka tisa alifanyakazi ya katibu baraza la mitihani japo marachache nyuma alioneka akifanya masuala ya utafiti na shirika la elimu la aghakhan.Siukatai uwezo wake mkubwa kipindi hicho cha nyuma ingawa amepata bahati baada ya kutoka masomoni anakutana na fursa ya uwaziri......
Siku zote unapoipata fursa ni lazima umuonyeshe aliyekupa kuwa hajapoteza...kwa kipindi kirefu umekuwa ukijishughulisha na matukio badala ya matatizo yanayoikabili sekta ya elimu...
Najaribu kutafuta nini umefanya ili baada ya miaka miwili mitatu tukukumbuke kwa kusema hiki ni cha fulani au unataka tuseme baadae matatizo haya kayaleta ndalichako.......
UTATA WA MH.NDALICHAKO
Kuna vitu Mh waziri amevifanya mpaka unajiuliza huyu ni waziri au nani kasema? Baadhi ni:-
1: Masomo ya sayansi lazima
Hivi waziri ulishindwa kutengeneza miundo mbinu bora kuboresha maslahi ya walimu wa sayansi na kuandaa walimu wakutosha motisha n.k wala ilikuwahaina haja kulazimisha wenyewe wangeenda....
Mfano mzuri jiulize kwanini raisi magufuli ni mwalimu mzuri wa sayansi mzuri aliacha kazi ya ualimu akaenda kiwandani baadae kwenye siasa...sababu zilizomtoa yeye na wengine zinawatoa pia......
2: Ubora wa baadhi ya vyuo vya elimu ya juu....
Kimsingi huwezi ukatibu tatizo hili kwa kusema wachuo fulani wakienda chuo fulani warudie mwaka mmoja nyuma kwa kuwa ubora tofauti ilihali hawa maprofesa ndiyo hao hao kilachuo......
Lakini nikukumbushe kitu ulikuwa huna haja kuwaambia warudie mwaka kwani kila chuo kikuu upo utaratibu wa KUSAP na KUDISCO sasa hivyo ndiyo vilikuwa vipimo kuwa wana ubora au la kuliko kusema asiyetaka arudi kwao(huu ni ubabe).....
Ulichotakiwa kufanya nikuuangalia upya mfumo mzima wa elimu ya juu ikiwezekanafumua wote......
3: Utoaji adhabu kwa wanafunzi
Hili jambo naona mara ya tatu unalirudia kana kwamba waalimu awajitambui vile..kifupi kwa sheria ya adhabu mashuleni hakuna mwalimu mwenye muda mchafu wa kuweza kuitekeleza kila mwalimu anamambo yake ya kufanya......
MWISHO
Kama utaendelea kuwa waziri wa kuzindua na matamko ukifikiri bado upo NECTA na kusahau kuwafikiria walimu tutegemee kushuhudia waziri mbovu ndani ya wizara ya elimu baada ya Magreth Sitta na Mungai kutokea
Sayansi inatakiwa iwe option sio lazima kama namuandaa mwanangu aje arithi biashara zangu au ofisi yangu ya sheria sayansi itamsaidia nn,kujenga tz ya viwanda kinachotakiwa ni kufufua vyuo vya maendeleo ya jamii,kufungua vyuo vingi vya ufundi kila kona na kuviboresha,Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?