Tatizo la JF ni kila mchangaji kuamini kuwa anavyoona na/au kuzungumza ndivyo suala husika linavyotakiwa kuwa. Wachangiaji wengi wanatoa ushuhuda badala ya utaalam katika Nyanja husika. hapa kuna walakini.
Mwl. Ndalichako amesoma, amefundishwa na kufundisha - shule za chini hadi vyuo vikuu. Amesoma masomo ya sayansi na elimu (UDSM), kufaulu kisha kubakizwa pale asome zaidi na kuwa mhadhiri kufundisha wengine katika taaluma za elimu na hisabati (vipimo).
Mwl. Ndalichako anajua kwamba mwanafunzi hapashwi kupewa fursa ya kupenda masomo kadhaa ili achague kusoma masomo ya sanaa au sayansi. La hasha. Mwanafunzi anapotoka nyumbani anapelekwa shule kusoma masomo yote. Huko anakutana na Mwalimu, mazingira, ya kusoma na zana za kusoma, basi. Anafundishwa na kupimwa ufaulu mara kwa mara. Atashauriwa na kuelekezwa namna ya kujifunza na malengo ya taifa kwa elimu anayoipata. Ni pale tu mwanafunzi akifika elimu ya juu anapata fursa ya kuoanisha malengo yake binafsi na malengo ya taifa ya elimu anayoipata. Akifika hapo anaweza kuchagua eneo mahsusi la kujifunza umahili katika fani yoyote.
Kwa hiyo, katka madarasa ya awali, mtoto hawezi kupewa fursa ya kuchagua masomo kwa kigezo cha urahisi. Mwanafunzi anatakiwa asome masomo yote. Na hili ndio tamko la sera la Serikali. Kwamba kwa kuwa lengo la serikali ni kuzalisha wataalam watakaokuja kufanya kazi katika maeneo mbali mbali ya viwanda (kipaumbele cha sera kuu ya serikali kwa sasa), basi watoto wasome masomo yote, sayansi na sanaa, hadi kidato cha nne. Kwa namna hii watoto ambao hawataweza kuendelea na masomo ya kidato cha 5 na 6, na hata watakaoendelea hadi kidato cha 6, lakini wasiendeleaa na elimu ya juu zaidi ya hapo, basi wawe na fursa ya kufanya mafunzo katika vyuo vya elimu ya ufundi, wapate ujuzi unaotakiwa kukamilisha lengo la taifa la kujitosheleza kwa nguvukazi viwandani.
Tunatakiwa kufahamu kuwa elimu siyo mali ya mtu binafsi, ni mali ya umma/taifa (public good). Kwa hiyo elimu ni rasilimali ya taifa ambayo mtu hastahili kujiamulia kuipata na kuitumia kwa namna anavyotaka mwenyewe au familia yake. Kwa kuwa elimu ni rasilimali ya taifa, basi serikali inawajibika kuifanyia mipango, uratibu na maboresho ya mara kwa mara. Kwa hiyo, alichofanya Mwl. Ndalichako ni jukumu lake la kusimamia mipango ya serikali katika elimu - rasilimali ya taifa kwa ajili ya maendeleo ya viwanda - kipaumbele cha sera kuu ya serikali kwa sasa. Sasa akina The Boss and the like wanataka kuaminisha umma wa JF kuwa kila kaya ina fursa ya kuwa na mipango na maamuzi yake ya rasilimali-elimu nje ya mipango ya nchi/serikali, la hasha. Huo ni upotoshaji. Tangazo la serikali kupitia waziri Ndalichako ni la kisera na ni sahihi.