Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Hii wizara ya Elimu sijui ina matatizo gani, karibu kila waziri anayeteuliwa toka kipindi cha Mkapa lazima aje avuruge mfumo wa elimu.
 
Nichangamoto kubwa...grade zmependa kwend university tena nako shidah
 
Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?
Ndalichako atatuachia majanga kama ya Mungai..huyu mama kaukamia kweli Uwaziri ngoja tuone time will tell
 
Af hao walimu wenyewe wa kufundisha masomo ya sayansi wapo wapi?

Upande wangu ningeona wa maana kama angepunguza masomo, mwanafunzi aanze ku specialize toka kidato cha pili kwa masomo matatu.
 
Yule bwana alikuwa na vituko vyenye vivuko. 1. Yule ndiye aliesema hatambui special schools. Tukakaa kimya. 2. Akachakachua shule nyingi za boys ziwe na girls, mf Azania. Tukakaa kimya. Hakukoma. 3. Akasema geography, history na nini sijui, ni somo 1 liitwalo: SOCIAL SCIENCES. Tukakaa kimya. 4. Akafuta UMISSETA! Daaah, Yule jamaaaa yule!
I miss you Mumbai, sorry, sio Mumbai.

Halafu anayeweka mambo sawa ndo tunashauti tuu bila hata kujua kwa nini isiwe hivyo. Eti mtu anapinga wanafunzi wasisome sayansi. Tunawajengea watoto wetu ulimwengu wa kufikiri kuwa sayansi haifai. Weka mfumo vizuri ili wakiingia sec wakikuta sayansi lazima watanyooka tu wenyewe. Nakumbuka enzi zetu ukienza Tech sec o level comb ni moja PCM hakuna cha arts na watu wanapiga shule vzr na kufaulu vzr.
 
kwa hali hii kiingereza chetu kinaenda kufa kabisa maana hawa wa art walitusave sana
 
WASOME MASOMO YOTE YA ARTS NA SAYANSI HADI FORM FOUR MBONA MATHS NA BIOS NI LAZIMA HADI FORM FOUR? PHYSICS NA CHEMISTRY PIA IWE NI LAZIMA TU MPAKA FORM FOUR ILA MIUNDOMBINU NA WALIMU HASA WA PHYSICS NI CHANGAMOTO KUBWA SERIKALI IJIPANGE KWELI. HUU UOGA WA KUSOMA PHYSICS NDIO ULIOPELEKEA HADI SASA TAIFA KUWA NA UHABA MKUBWA WA WATAALAM WA HILI SOMO LA PHYSICS. ACHENI KUOGOPA NA KUCHACHAMAA UTAFIKIRI MNAINGIA SHULENI TENA. HII NI KWA AJILI YA VIZAZI VIJAVYO YAANI KAMA NI PENDEKEZO NI KUANZIA FORM ONE NA FORM TWO WA MWAKA 2016.SASA NYINYI MNAOPIGA KELELE HUMU NA KUTOKWA NA MAPOVU NI FORM ONE AU TWO 2016? KUSOMA SAYANSI IWE LAZIMA HADI KIDATO CHA NNE.
 
Haya mambo mimi nayatazama kwa jicho la tatu.
Unapolazimisha watu washikilie kitu ambacho hujakiboresha kiwe cha maana kwao,mantiki yake ni nini?Hutaki watu wawe na kitu cha maana na hiyo ni janja yako kuwakosesha,sivyo?
Tunalalamika kila siku humu jinsi mfumo wetu wa elimu usivyofaa kwa elimu ya sayansi,badala ya kushughulika kuuboresha,ndio kwanza tunazidi kuufanya utuletee majanga zaidi,sasa tukisema hii ni makusudi tunakosea?Hawa wazee na usomi wao hawayaoni haya?
Mimi najiuliza sana,wanachokitaka watoto wasome sayansi au watoto wafeli?Kwanini vikwazo hivi?Watu wasome Physics,Chemistry,Bios,Maths kwa lazima ndani ya mfumo mbovu hivi halafu unawaambia wapate division one na two form six ili wasome bachelor,na wale watakaoshindwa hapo wapitie njia ya certificates,diplomas,kwa GPA ya 3.5!
Wenye akili mmeelewa hidden message hapo!
mi nimejiuliza swali moja tuu....kwa kutumia walimu wa sayansi hawa walioko mashuleni?
 
KUSOMA SAYANSI HADI KIDATO CHA NNE IWE NI LAZIMA. ACHENI UOGA NDUGU WANANCHI NI KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO. HIVI HAMJIULIZI KWANINI LEO HII UOGA UMESABABISHA TUKAWA NA RUNDO LA WALIMU WA SANAA MASHULENI NA KUWA NA UHABA WA WATAALAM WA SAYANSI?
 
Nilishasema toka awali kua huyu mama anakurupuka sana watu wakapinga vikali. Mpaka hapa sijaona mwelekeo wa mafanikio kwa uwepo wa huyu mama Wizara ya Elimu. Wizara ya ELIMU sio NECTA, sio taasisi ndogo! Hii wizara ndio moyo wa nchi.

Sijui mwaka huu vyuo vikuu vingapi vitakavyopokea wanafunzi wa fani za Sayansi. Utaratibu wa kizamani sana huu.
 
kwa hali hii kiingereza chetu kinaenda kufa kabisa maana hawa wa art walitusave sana
NDUGU HUJAELEWA MAADA AU?
MASOMO YA SANAA YANAENDELEA KINACHOONGEZEKA NI ULAZIMA WA KUSOMA PHYSICS NA CHEMISTRY TU PLUS MATHS NA BIOS AMBAYO NI LAZIMA TOKA AWALI SI KWAMBA MASOMO YA ARTS YANAFUTWA
 
KUSOMA SAYANSI HADI KIDATO CHA NNE IWE NI LAZIMA. ACHENI UOGA NDUGU WANANCHI NI KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO. HIVI HAMJIULIZI KWANINI LEO HII UOGA UMESABABISHA TUKAWA NA RUNDO LA WALIMU WA SANAA MASHULENI NA KUWA NA UHABA WA WATAALAM WA SAYANSI?
Nani atafaulu physics na chemistry kama hesabu anafeli?
 
KUSOMA SAYANSI HADI KIDATO CHA NNE IWE NI LAZIMA. ACHENI UOGA NDUGU WANANCHI NI KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO. HIVI HAMJIULIZI KWANINI LEO HII UOGA UMESABABISHA TUKAWA NA RUNDO LA WALIMU WA SANAA MASHULENI NA KUWA NA UHABA WA WATAALAM WA SAYANSI?
Ndugu, kuna watu wanafanya siasa hapa, kazi yao kupinga kila kitu, hakuna hoja inayoonyesha ni uamuzi mbaya bali kuna hoja zinazoonyesha kuna changamoto, ambacho si kitu kibaya. Ni lazima jitahida za maksudi zifanyike ili kizazi kijacho kiweze kupata wataalamu wa Sayansi wa kutosha.
 
kwa hali hii kiingereza chetu kinaenda kufa kabisa maana hawa wa art walitusave sana
chilumendo watu wa Sanaa wataendelea kuwepo kama zamani, tofauti tu soma la Physics na Chemistry halitakuwa tena la kuchagua, litakuwa la lazima kama yalivyo baadhi ya masomo mengine saivi kama Maths na Kiswahili.
 
HALAFU MI NAPENDEKEZA SERIKALI IWAPE MOTISHA KUBWA WALIMU WA SAYANSI ILI KIWE KIVUTIO MOJAWAPO CHA KUPATA WATAALAM WA HAYO MASOMO MAANA WAZAZI HUWA TUNAWASHAURI WATOTO WETU KUCHEPUA MICHEPUO YENYE MASLAHI SANA KAMA LAW NK. LAKINI KUKIWA NA MASLAHI MAPANA KWENYE HII SEKTA HATA HUYU ANAEOGOPA NA KUSHAURI WATOTO WAOGOPE SAYANSI ATAKUWA WA KWANZA KUMWAMBIA MTOTO WAKE KUZINGATIA HAYO MASOMO BAADA YA KUONA MASLAHI HAYO. SERIKALI ISIISHIE TU KUTOA MIKOPO 100% MAVYUONI KWA WATU WA SAYANSI BALI IONGEZEE UPENDELEO KWA HAWA WATAALAMU YAANI WALIMU WA HAYA MASOMO MAANA NDIO CHIMBUKO HASA
 
Back
Top Bottom