Victor wa happy
JF-Expert Member
- Apr 24, 2013
- 11,660
- 11,664
Profesa wa hisabat, awe wanakaa chini na kufikiri kabla ya maamuzi
Kwel aisee mzee wa mama yetu Tanzania James Mbatia,anamengi sana kuhusu elim sema ndo ivyo 2.Sijui nani atakuja kuikomboa elimu ya nchi hii maana kila anae kabidhiwa ofisi anakuja na yake kwa kumsikiliza mpiga zumali wake.
Sijui kwanini kuna kua na ugumu wa kuja na sera moja makini ya kitaifa iliyochambuliwa na wadau wote wa elimu na ikapitishwa na pasiwe na mwingine wa kuja kuivuruga.
Ndugu yetu kaililia wee "Mama Tanzania" wameishia kumpuuza badala ya kumshika mkono tupate mchango wake.
Hawa wasomi wetu sijui wanatupeleka wapi.
Soon tutasikia masomo yasiyokuwa ya sayansi yamefutwa!Sijui nani atakuja kuikomboa elimu ya nchi hii maana kila anae kabidhiwa ofisi anakuja na yake kwa kumsikiliza mpiga zumali wake.
Sijui kwanini kuna kua na ugumu wa kuja na sera moja makini ya kitaifa iliyochambuliwa na wadau wote wa elimu na ikapitishwa na pasiwe na mwingine wa kuja kuivuruga.
Ndugu yetu kaililia wee "Mama Tanzania" wameishia kumpuuza badala ya kumshika mkono tupate mchango wake.
Hawa wasomi wetu sijui wanatupeleka wapi.
Sijaona penye huo ULAZIMA maana ukimaliza form four utaendelea na choice yako.Primary ndio sayansi lazimaWengi mmeona habari ya leo kuwa sasa ni lazima wanafunzi wote wasome Sayansi kabla ya hiii zimekuwepo habari nyingi za kushangaza za wizara hii ya elimu. Siku Magufuli aliposema anashangaa fimbo kupigwa marufuku mashuleni, kesho yake tu Wizara hii ikatangaza 'fimbo kurudishwa mashuleni'
yaani halikuwa na mjadala wala kutolewa maelezo labda why fimbo zilizuiwa mwanzo au kuna watalaam gani walihusika kufikia maamuzi.
Halafu yakaja maamuzi ya kuongeza ufaulu ili kujiunga na vyuo, hili nalo limechukuliwa kama Tanzania ni kisiwa vile mpaka sasa wala hakuna maelezo iwapo mwanafunzi wa kitanzania akipata nafasi kusoma nje ya nchi kwa ufaulu ambao hapa nchini haumruhusu, vyeti vyake vitakuwa na 'status' gani hapa nchini mradi maamuzi ya wizara hii sasa ni kama vile Tanzania ndo 'The world'
na kila atakachoamua yeye ndo 'final'
Huyu mama na Mabosi zake wanasahau kuwa tuko katika 'global village' Maamuzi ya ajabu ajabu sanasana yatawaathiri watoto wa masikini tu
wengine wenye options za kusoma nchi jirani na nchi za mbali hayatawagusa na mwishowe watakao 'umizwa na maamuzi' haya ni watoto wa masikini.Sasa hili la lu kulazimisha Sayansi nalo unajiuliza nchi ngapi duniani linatumika?
Je mtoto wa kitanzania akisoma Kenya au Uganda au kwingineko
ambako hakuna 'maamuzi ya aina hii' huyu mama atafanyaje? Hivi why 'tuna invest kwenye kuongeza kero na vizingiti' vya kila aina kwa watanzania? Kwani Tanzania ni kisiwa? Si masuala ya elimu yanapaswa kuwa 'Universally acceptable'? Sasa huyu mama ndo mifano wa maprofessa wetu?
Anadhani kusoma Physics na Chemistry ndo kuweza kuoperate viwanda!
Kwanza machine za siku hizi siyo manual ni automated computerized.
Nimesoma mimi physics na chemistry lakini sijawahi kuiapply popote!, hata huko viwandani hawaangalii physics umefauluje
...ndio wasome sayansi...
ukizungumzia maskini,ungejua maskini ndio wanachimba(wanasoma Zaidi) ...usingesema wataumia Zaidi...
sayansi wakati ule,ilikua lazima kwa wote mpk form two,form three na kuendelea ndio wanaanza kuspecialize....
ssijajua alikua anamaanisha nini sasa hivi?mwenye kujua anifafanulie
Hapa kasi tuu
We inao
Wewe inaonesha kabisa umekimbia umande...
Hamna kitu, yaani mweupee... Empty kabisa.
Ingawa bandiko lako umelijaza Kiingereza bila ya sababu za msingi kuna hoja hapa umeianzisha naona na mimi nichangie. Kwenye mfumo wetu wa kufundishia darasani kuna tatizo kidogo. Mwalimu inaaminika anajua kila kitu wakati mwanafunzi anachukuliwa ana ubongo ulio wazi wa kujazwa kila kitu toka kwa mwalimu. Aina hii ya ufundishaji iko mpaka kwenye vyuo vyetu vikuu.Ofcoz vipo vichwa vingi ambavyo vitafeli Tanzania, hasa arts hua wanafeli sana pamoja na kua na idadi kubwa still wana kauvivu fulani wakiamini arts ni kitu rahisi.
Ni ubunifu mpya only in Tz. Hao walimu wa sayansi watatoka wapi? Nchi ina uhaba wa walimu wa hili somo halafu eti somo la sayansi lazima!Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?
Sema taratibu kabla hujasikia katazo la kutengeneza kitu kama hujapewa kibali na mamlaka husikaBasi mkuu physics uliitupa pembeni au hukuielewa vizuri au unachokifanya ni kuoperate vitu ambavyo ni already made na huna passion ya kubuni kitu chako mwenyewe, we unadhani hizo automation ya hizo machines anayefanya ni nani? ambaye hajasoma physics? tukitaka kuwa na viwanda tusitegemee tutanunua kila product nje, vitu vingine ni custom built lazima tuweze kuvitengeneza sisi wenyewe, we unataka hadi machine ya kupima vitu na kukata twende nje tukanunue huku its very basic physics?
Physics ni muhimu sana, mimi niliisoma na hadi leo hii ninaitumia kwenye kazi zangu mara kibao tu, siku nyingine narudi kuchimba vitabu vya university physics kuangalia principles nikiwa nimezisahau. Kama ni kutengeneza viwanda tunahitaji watu waliosoma physics, huwezi tengeneza engine ya gari bila physics, huwezi tengeneza game la computer, hata kiatu bora cha kuvaa unapima strength ya material, heat absorption na dissipation, hadi vitu basic kama rangi nyeupe inafanya reflection na nyeusi inafanya complete absorption ni concepts nyepesi lakini very important ikija kwenye decisions ya rangi ipi utumike sehemu flani. We idea yako ya viwanda kumbe ni kununua kila kitu nje alafu tukaoperate wenyewe? Hehehe mimi idea yangu ni mbali na kununua vichache nje, vingi tunatengeneza sisi wenyewe.
Kumbe bado mtoto mdogo!!!!?Mkuu ilinipata hii eti physics na chemistry ni somo moja🙁🙁