Maamuzi ya ndani

Maamuzi ya ndani

4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMAG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU
 
Haya mambo hayataki hila. Lazima ukweli, uwajibikaji then maridhiano yafanyike. Kinyume chake kila njia za hila ku solve itazaa matatizo mengine makubwa zaidi. Tunahairisha matatizo na kusuka mengine! Italeta matatizo mengi

..sio hila tu, kuna udhalimu ndani yake.

..haiwezekani watu wameuwawa, ikiwemo watoto, halafu wahusika wanajikausha, na kudai tuko vizuri.
 
KOSWE ye ni kusinzia tu
Hapa anatafakari
FB_IMG_1756217929952.jpg
 
Pamoja na uzuri anaopambwa nao huyo Balozi, lakini kwa mwendo wake huo atalisalimisha jahazi tulilotaka lizame moja kwa moja.

CCM ilivyo sasa hivi kamwe haiwezi kufanyiwa ukarabati wa juu juu kwa matumaini ya kurudisha ile ya zamani.
Balozi anajaribu kuweka bandage kwenye donda ndugu, akifikiri litapona!
Anapoza maumivu ya muda mfupi tu, huku donda ndugu likiwa bichi kabisa ndani kwa ndani.

Acha nikupe na mfano hai kabisa kama bado unamashaka kuhusu ninaloeleza hapa.
CCM ya Magufuli; uliiona? Mara PAAAA, Samia kaingia,.... Donda likaanza kutoa usaha kabisa.

Balozi anaweza kulituliza kidogo. Haliponi hilo!
CCM kupona kwake ni kupigwa chini warudi kwenye drawing board wajifunze kuwa chama cha siasa maana kwa sasa siyo tena chama cha siasa bali ni genge maslahi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala. Bila kuwatoa nje hawa madhalimu wataendelea kuwa chinjachinja na kuzidi kuiharibu nchi.
 
Kumbe ndio maana Nchimbi ameanza kuimba mambo anayo pigania Lissu ili akitoka waje waseme kwamba mambo anayopigania Lissu ni hoja zao. Sasa nimeanza kumwelewa Mh. Nchimbi aliposema “ pambanieni katiba”. Ile ilitoka kimkakati ili wampiku Lissu huko mbeleni… taabu tupu…
 
Back
Top Bottom