Maalim Seif: Lowassa amerudi CCM kwa shinikizo la familia na Chadema kutotendea vyema

Seif anahusiana nini na Cdm ?!
Uliachwa lakini hawajakutoka moyoni !!.

Hivi unafikiri Maghufuli kutoka magogoni na kwenda kumpokea Lowassa kule Lumumba ilikuwa kazi ndogo na rahisi ?!. Hilo lilikuwa deal la system a k a wasiojulikana. Si swala Cdm

Sent using Jamii Forums mobile app
Jenga hoja kamanda, kwani harusiwi kutoa maoni kuhusu Chadema?
 
Ndugu zangu,

Karma inafanya yale unayomfanyia mwenzio, taabu wanazopata Chadema huenda ni malipo ya mabaya waliyofanyia waliowainua.

========

Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ametoa mtazamo wake kuhusu uamuzi wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda ‘Ukawa’, Edward Lowassa kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maalim Seif ambaye mwaka 2015 alikuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) kilichokuwa mshirika wa umoja huo, amesema yeye hawezi kumhukumu Lowassa kwa uamuzi wake ingawa anakiri amewaumiza na kuwaangusha wapinzani kwa uamuzi wake huo.

Amesema Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa na sababu nyingi za kumfanya arudi CCM ikiwa ni pamoja na msukumo wa familia lakini pia kutotendewa vyema na chama hicho kikuu cha upinzani.

Amesema kuwa Lowassa ni tofauti na yeye kwakuwa yeye ameweza kuvumilia mikikimikiki na matokeo ya kuwa mpinzani.

“Yule [Lowassa] ujue alikuwa Waziri Mkuu, na malupulupu yake yote ya Uwaziri Mkuu, kwahiyo baada ya kuona lile ambalo alilitegemea kupata katika upinzani hakupata, na akaona kwamba Serikali inamsindikiza…,” alisema.

“Na ninavyosikia mimi familia yake ilimshinikiza, kwamba kuna mmoja kati ya wakwe zake alikuwa gerezani na watoto wake walikuwa wanamwambia ‘baba unaona… baba yetu sisi anapata shida kwa sababu wewe uko upinzani. Kwahiyo, ile presha ya familia ilikuwa kubwa sana. Lakini vilevile tunasikia pia kuwa na Chadema hawakumtendea vyema vilevile… kwahiyo ana sababu nyingi na mimi sitaki kumhukumu, lakini tulivunjika moyo sana [Lowassa kurudi CCM],” Maalim Seif aliiambia Global TV.

Mwanasiasa huyo alikiri kuwa ujio wa Lowassa ndani ya Ukawa ulisaidia na kuongeza nguvu kubwa ya umoja huo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ingawa hawakufanikiwa.

Machi 1, 2019, Lowassa alirejea rasmi CCM aliyoihama mwaka 2015 baada ya kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kupata nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Chanzo: Dar 24

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee acha porojo kilichomrudisha Lowassa CCM ni Familia yake+Kesi+Mali zake hakuna cha kutendewa Vibaya na Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Lowasa kaondoka leo kwenda CCM? Mzee Lowasa aliondoka kistaarabu na alisema maneno mchache tu kuwa amerudi nyumbani na watu waliheshimu maamuzi yake wala hakuwa kutukanwa wala kukejeliwa. Mtu aliyeondoka kishamba ni Sumaye.

Sasa huyu Maalim naye sijui aliahidiwa nini huko Magogoni anajiropokea tu mbona hasemi ni jambo gani baya Chadema walimtendea Lowasa? Wote waliokwenda magogoni wametoka na maelekezo. Tutafahamiana tu mbele ya safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui seif kitu gani kimempata hata mimi nilipoona kwenye interview yake nilishangaa sana, anyway ndio maana cdm wanataka kwenda ikulu kama team na sio mtu mmoja maana chochote chaweza kutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ungejibu hoja bila kejeli kamanda
Naona mods wamekusaidia kuandika heading,mwanzo kabisa nilisema kwa tittle hiyo mtu asiposoma content anaingia cha kike!Naona mods wameliona hilo na wamekurekebisha na nia yako ya kupotosha,hahahaaaaa!Lumumba mnakwama sana kwenye propaganda!
 
Haya sasa jikite kwenye hoja usijichekeshe angali moyo unalia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi na Duni?

Jogoo wa kuazima siku zote akimaliza kazi anarudishwa au anarudi kwao.

Hizo za "nasikia" ni porojo tu.
 
Hayo n
Ndugu zangu,

Karma inafanya yale unayomfanyia mwenzio, taabu wanazopata Chadema huenda ni malipo ya mabaya waliyofanyia waliowainua.

========

Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ametoa mtazamo wake kuhusu uamuzi wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda ‘Ukawa’, Edward Lowassa kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maalim Seif ambaye mwaka 2015 alikuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) kilichokuwa mshirika wa umoja huo, amesema yeye hawezi kumhukumu Lowassa kwa uamuzi wake ingawa anakiri amewaumiza na kuwaangusha wapinzani kwa uamuzi wake huo.

Amesema Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa na sababu nyingi za kumfanya arudi CCM ikiwa ni pamoja na msukumo wa familia lakini pia kutotendewa vyema na chama hicho kikuu cha upinzani.

Amesema kuwa Lowassa ni tofauti na yeye kwakuwa yeye ameweza kuvumilia mikikimikiki na matokeo ya kuwa mpinzani.

“Yule [Lowassa] ujue alikuwa Waziri Mkuu, na malupulupu yake yote ya Uwaziri Mkuu, kwahiyo baada ya kuona lile ambalo alilitegemea kupata katika upinzani hakupata, na akaona kwamba Serikali inamsindikiza…,” alisema.

“Na ninavyosikia mimi familia yake ilimshinikiza, kwamba kuna mmoja kati ya wakwe zake alikuwa gerezani na watoto wake walikuwa wanamwambia ‘baba unaona… baba yetu sisi anapata shida kwa sababu wewe uko upinzani. Kwahiyo, ile presha ya familia ilikuwa kubwa sana. Lakini vilevile tunasikia pia kuwa na Chadema hawakumtendea vyema vilevile… kwahiyo ana sababu nyingi na mimi sitaki kumhukumu, lakini tulivunjika moyo sana [Lowassa kurudi CCM],” Maalim Seif aliiambia Global TV.

Mwanasiasa huyo alikiri kuwa ujio wa Lowassa ndani ya Ukawa ulisaidia na kuongeza nguvu kubwa ya umoja huo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ingawa hawakufanikiwa.

Machi 1, 2019, Lowassa alirejea rasmi CCM aliyoihama mwaka 2015 baada ya kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kupata nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Chanzo: Dar 24

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ni maoni yake binafsi,lakini ukweli ni kwamba yeye mwenyewe alisema utendaji kazi wa Rais JPM ndio umemfanya arudi kundini. Maana hakuna haja ya kukaa CCM B wakati CCM A inafanya yale ambayo wananchi wanayataka.
 
Back
Top Bottom