Kumtenganisha Lowassa na chadema ccm inajua bunge linajua na tume ya uchaguzi inajua kuwa haiwezekani

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,028
Hakika kwanza nianze na POLE nyingi sana kwa Familia ya Hayati Edward Lowassa,Rais Samia Ccm na CHADEMA.
Hayati Edward Lowassa alikuwa Mwanachama wa Ccm mpaka pale Chama chake kilipomkata jina kwa Chuki binafsi za mtu mmoja licha ya Wanaccm kwa Mamilioni kumtaka awe RAIS wao kwani alikuwa na SIFA walizozitaka kwa mujibu wa Katiba yao.Baada ya Kutoswa na CCM Hayati Edward Lowassa alijiunga na Chama Kikubwa cha Upinzani CHADEMA.

Chadema walimpa HESHIMA kubwa ya kuwa Mgombea wao wa URAIS.Yaliyotokea kwenye KAMPENI kwa Wagombea wote sote tunayajua CCM kiliendelea kumtukana kumbeza kumkejeli Majukwaani kipitia VIONGOZI wake.Uchaguzi ukafanyika Hayati LOWASSA alipata zaidi ya KURA MIL.6 Yaliyofanywa MASAKI wote tunayajua BAO la MKONO wote tuliliona.

Pamoja na yote Hayati LOWASSA aliwapa USHINDI MKUBWA wagombea wa CHADEMA Madiwani zaidi ya 2000 Majiji yote yaliongozwa na CHADEMA Wabunge zaidi Waliingia Bungeni.YOTE hayo CCM inayajua

BUNGE linajua na TUME ya Uchaguzi iliyotangaza Matokeo inajua.Tunaposema UKIMTAJA Hayati LOWASSA ktk Safari yake ya KISIASA kutoitaja CHADEMA Ni KUJIDANGANYA.Kwa mfano CCM ikiulizwa Je Lowassa baada ya kukatwa jina ilikuwaje alibaki kuwa mwanachama wa kawaida ,Aliacha siasa au Alienda wapi?

HISTORIA ya Hayati Lowassa Kiasiasa LAZIMA Uitaje CHADEMA kwani ndio Chama PEKEE kilichompa HESHIMA kubwa baada ya Chama alichokitumikia miaka yote kumtosa.PUMZIKA LOWASSA MWENDO UMEUMALIZA HISTORIA YAKO KISIASA ITAENZIWA PICHA ZAKO ZIPO VITUKUU WATAZIONA
 
Nimetoka kuona clip za lema.dah yeye tena ndio kaisema vibaya kweli malehemu. Rema temdio munafiki khasa
 
Back
Top Bottom